Quantcast
Channel: ShaffihDauda

“Simba IMEFANIKIWA”-Amri Kiemba

$
0
0

Mchezaji wa zamani wa Simba Amri Kiemba anaitakia kila la heri timu yake kwenye game ya leo ya mwisho ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita. Endapo Simba itashinda mchezo huo, itafuzu hatua ya robo fainali.

Kiemba anasisitiza kwamba, hatua ambayo Simba imefika (kucheza makundi ya ligi ya mabingwa) ni mafanikio makubwa kwao hata kama hawatafuzu kucheza robo fainali.

“Mimi kama mtanzania mwana michezo ni hamu yangu kuiona Simba ikisonga mbele na kuwakilisha taswira ya soka letu japo sio kwa uhalisia.”

“Kwa hatua waliyofikia Simba mpaka sasa kwangu mimi wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa bila kujali matokeo ya mchezo wa mwisho dhidi ya As Vita, kiu yangu ni kuona wakiendeleza pale walipoishia namaanisha hii hatua ya makundi isiwe lengo bali ni sehemu ya timu kupumzikia kwaajili ya kuelekea kwenye hatua zinazofuata.”

“Kwa ajili ya afya kwa soka letu tunahitaji timu zetu zifuzu hatua hii au hata zaidi ya hapa ili kusaidia kubadilisha baadhi ya vitu.”

“Wana Simba nendeni uwanjani kifua mbele kwa hatua timu iliyofikia bila kujali matokeo ya mchezo yatakua mazuri au mabaya.”

KILA LA HERI SIMBA, KILA LA HERI TANZANIA.


This is Simba brother

$
0
0

Hongera Simba Sport club, kwa kupata ushindi muhimu dhidi ya As Vita, katika uwanja wa nyumbani jijin Dar es salaam, na kwenda hatua ya robo fainali kwenye michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika.

Simba, leo ulionekana kuwa bora katika idara ya kiungo mkabaji Kotei, na Mzamiru , wamefanya viungo wa klabu ya As Vita, kucheza chini zaidi kwa maana ya kujilinda Kotei,alitumika ni wa kati kwa maana ya kuwalinda mabeki wake pale wanapokuwa hawana mpira na kuziba mianya nyote ya kupitisha mpira.

Katika idara ya kiungo mkabaji leo Mzamiru muda mwingi alikuwa akitokea pembeni kwa maana ya kujaribu kuwapunguza kasi Vita ,ambao wamekuwa wazuri tukio pembeni muda mwingi Vita,walikuwa wakicheza kwa kujilinda.

Simba, katika idara ya kiungo mshambuliaji kumekuwa na matatizo bado Chama, muda mwingi amekuwa akishindwa kuendesha timu na na kufikisha mpira mbele kwa muda muwafaka hili ndo lilikuwa likiwasumbua Simba, kwenye mchezo wa leo.

Mwalimu Patrick Aussems,aliamini kuwa kipindi cha pili hana cha kupoteza alimtoa Emannuel Okwi,na kumuingiza Niyonzima Haruna, kwa nini ?alifanya hivo alihitaj kiungo mshambuliaji wenye spidi na uwezo wa kupelekea mpira unapocheza na timu yenye uwezo mkubwa katika idara hiyo kiungo unahitaji uwe na viungo wenye uwezo wa kushambulia kwa haraka na kutengeneza nafasi.

Sina maana Chama, hajui mpira hapana?ila mchezo wa leo ameshindwa kuendana na kasi ya mchezo huu.

Patrick Aussems,alivowatoa viungo wote wakabaji ? na kuingiza wachezaji washambuliaji kwenye kuongoza nguvu? kwa maana mda ulikuwa ushaisha na alihitaji matokeo.

Kwa nini?alipunguza viungo wakabaji kwa maana aliona kwa dakika hizi Vita wamejitoa na kuja kushambulia kwa kasi muda mwingine mwalimu unahitaji ujitoe na kufanya maamuzi binafsi.

Azizi Mtambo 15

Simba yaandika historia mpya ligi ya mabingwa Afrika

$
0
0

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994, klabu ya Tanzania inafika hatua ya robo fainali ya Ubingwa wa Afrika (Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa). Timu ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Simba, lakini ilitolewa na Nkana FC kwa jumla ya mabao 4-3.

Kuna watu huhesabia mafanikio ya Yanga 1998, na Simba 2003 kama robo fainali. Lakini ukweli hauko hivyo. Katika miaka hiyo, timu hizi zilifuzu kwa hatua ya makundi na wala siyo robo fainali.

KWANINI?

Mashindano haya yalianza mwaka 1965 yakiitwa Klabu Bingwa Afrika na yaliendeshwa kwa mtindo wa mtoano kuanzia raundi ya kwanza hadi fainali.

Mwaka 1997, CAF ilibadilisha mfumo na kuanzisha hatua ya makundi. Hapo ndipo jina la mashindano likabadilika kutoka Klabu Bingwa na kuwa Ligi ya Mabingwa.

Kulikuwa na makundi mawili ya timu nne nne. Mfumo huu mpya ulifuta hatua za robo fainali na nusu fainali na kukawa na makundi mawili ambapo vinara wa kila kundi walitinga moja kwa moja fainali.

MKANGANYIKO

Mfumo huu haukueleweka kwa wengi. Kwa mfano, mwaka 1998, Yanga ilipofuzu hatua ya makundi, Katibu Mkuu wa FAT, Ismail Aden Rage, alinukuliwa akisema kwamba Yanga wametinga nusu fainali. Yawezekana alikuwa hajaulewa vizuri mfumo mpya.

Mwaka 2001, CAF wakairudisha hatua moja ya nusu fainali, iliyofutwa 1996. Timu mbili za juu kutoka kila kundi zilifuzu kwa nusu fainali…na washindi kutinga fainali.

Mwaka 2017, CAF wakaongeza idadi ya timu za kufuzu hatua ya makundi kutoka 8 hadi 16 na kuongeza makundi kutoka mawili hadi manne.

Hapo ndipo hatua ya robo fainali iliporudishwa tena tangu iwepo mara ya mwisho 1996.

Msimu huu, 2018/19, Simba imetinga robo fainali…ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania tangu 1994!

© Zaka Zakazi

MEZA YA MAKUMBUSHO: Samatta tunakudai

$
0
0

Mbwana Samatta wewe nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania. Unacheza Genk na ni kinara wa mabao huko kwa wazungu, wazungu siku hizi wanakuimba lakini hapa kwetu Chama anaimbwa zaidi kwa siku za hivi karibuni kwa kusaidia Simba kwenda robo ACL.

Anaandika @Privaldinho (Instagram)

Samatta bado tunalilia rekodi ya mwaka 1980 ambapo tulishiriki hatua ya makundi AFCON kwa mara ya kwanza na ya mwisho kufikia sasa.

Kitambaa chako kimenikumbusha nahodha pekee aliyewahi kutuwakilisha katika mashindano hayo, naye si Mwingine ni Jella MtagwaMtagwa ndiye aliyehakikisha iwe kwa damu, jasho au moto lazima Stars inapata alama 1 au 3 pale Dag Hammarskjoeld jiji Ndola Zambia. Stars ilifanikiwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Chipolopolo na kufuzu.

Kama Mtagwa alipigana kufa na kupona kutupeleka Kule Lagos tena akiwa katika ardhi ya wazambia, Samatta utashindwa kweli kuongoza jeshi lako ndani ya uwanja wetu wa taifa?

Samatta umepata mafanikio makubwa sana ndani ya soka mara 100 ya bwana Mtagwa ambaye heshima yake inafifisha mafanikio yako kwenye mioyo ya wapenzi wa taifa stars na heshima ya taifa letu kwako.


Mechi ya kwanza Mtagwa aliwaongoza akina Raisi wa zamani Mh Tenga kuwafumua Chipolopolo pale uhuru kwa goli moja tu.

Mechi ya pili akaenda kulazimisha sare, tukafuzu,.. Samatta ukiwa na akina Msuva mlipata sare kule Uganda, hapa kwetu tunahitaji ushindi tu.

Hapa kwetu Clatous Chama ametawala midomo ya wengi, tunakuomba mwenye mji wako urudi…, Come oooooon Captain Diego

Huyu ndio Zana Coulibaly!

$
0
0

Baada ya kuonesha kiwango kizuri na kuwashika mashabiki wa Simba, wakala wa Zana Coulibaly Faustino Mukandila amefunguka mambo kibao ikiwa ni pamoja na sababu za mchezaji wake kuanza kwa kusuasua alipojiunga na Simba.

KWA NINI ZANA ALIANZA KWA KIWANGO DUNI?

“Zana alikuja Simba akiwa hajafanya maandalizi ya pre season baada ya kuondoka Asec Mimosas. Zana ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kucheza nafasi zaidi ya moja na hujitoa 100% muda wote anapocheza.”

“Nadhani mashabiki sasa wameanza kumuona Zana mwenyewe japo hata watu ndani ya klabu hawakuwa na imani naye. Nafarijika kuona kijana anatoa mchango kwenye timu, anaipenda timu na mashabiki. Alibezwa sana na ilikuwa inaumiza lakini ukiwa mchezaji mzuri Mungu hakutupi wakati wowote.”

AMEWEZAJE KUREJEA KWENYE KIWANGO CHAKE LICHA YA KUZOMEWA NA MASHABIKI?

“Zana ni kijana anayejitambua, hata wakati alipobezwa alibaki kwenye malengo yake kwa sababu alikuwa anatambua muda wowote kiwango chake kitarejea. Hata sasa ambapo mambo yameanza kwenda sawa lakini bado hachukulii vitu poa. Mara kwa mara namkumbusha asimame kwenye malengo.”

ZANA ANAMAJUKUMU!!

“Anapendwa na mashabiki lakini kijana mwenye mke na mtoto ambao wanamfanya kuwa kijana mwenye majukumu.”

Maajabu ya Chama dakika za usiku

$
0
0

Chama alifunga goli vs Nkana dakika ya 88, Simba ikafuzu kucheza hatua ya makundi ya CAF Champions League.

Chama amefunga goli vs AS Vita dakika ya 89, Simba imefuzu robo fainali ya CAF Champions League.

Chama anapenda kufunga dakika za kuku kurudi bandani!

Article 3

$
0
0

#SportsRoundUp AMRI KIEMBA AISHAURI SIMBA

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba Amri Kiemba ameishauri mambo kadhaa klabu yake mara baada ya kufanikiwa kuifunga AS Vita na kufuzu robo fainali ya ligi ya vilabu bingwa Afrika.

Kiemba pia ameipongeza Simba kwa kuvuka malengo yake iliyokuwa imejiwekea kabla ya kuanza mashindano, malengo ya Simba yalikuwa ni kufika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika lakini wamefuzu robo fainali.

“Kwa kuwa malengo yamevukwa, wasiwasi wangu ni kwamba, haya matokeo yanaweza kutusahaulisha tulipo na tunapotaka kwenda.”

“Tunaweza kujiona tayari ni wakubwa wa kiasi hiiicho tukashindwa kuendelea na misingi ambayo tumeianzisha na tulipanga ya kwenda kuwa wakubwa.”

“Watu wanaweza kuona tayari Simba ni kubwa wakati mumbe ndio inaandaliwa kuwa kubwa. Tumevuka malengo lakini tusisahau level yetu ipo wapi.”

“Kufika hatua hii isiwe kama bahati bali iwe kawaida kwa Tanzania kupeleka timu hatua hizi.”

Walichofanyiwa AS Vita cha mtoto!

$
0
0

Timu ya AS Vita haikuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakidai kumepulizwa dawa ya kuwanyong’onyeza wachezaji kabla ya mechi yao vs Simba ya hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika.

Sasa mchezaji wa zamani wa Simba Amri Kiemba anasema vitu ambavyo wanavilalamikia Vita ni cha mtoto ukilinganisha na matukio ambayo amewahi kukutana nayo enzi zake akiwa mchezaji.

“Kwa experience yangu ya kuzunguka Afrika nikiwa mchezaji, vitu vinavyofanyika Tanzania ni vidogo mno. Hivi vitu ambavyo AS Vita wanalalamika wamefanyiwa (nje ya uwanja) ni vidogo ni vidogo sana kwa soka la Afrika.”

“Kwa mfano ukienda kucheza na Al Merrikh ya Sudan mashabiki wao wanavurugu sana, kuanzia kwenye mazoezi, basi likipita linapigwa mawe. Hampati muda wa kujiachia wakati mwingine inabidi mazoezi mfanyie kwenye bustani za hotelini.”

“Kwa hiyo vita hawana kisingizio, walizidiwa ndani ya uwanja na mechi zao nyingi za ugenini hawana rekodi ya kupata matokeo.”


Ushindi wa Simba ni ushindi wa Tanzania”-Joseph Kusaga

$
0
0

Mkurugenzi wa Clouds Media Joseph Kusaga amesema ushindi iliopata Simba ni wa taifa zima kwa sababu walikuwa wanawakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika na kufanikiwa kuingia robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

“Utake usitake ushindi wa Simba SC ni ushindi wa taifa na tukiangalia kwa ukubwa wake ni ushindi utakaosaidia taifa kwa mambo mengi sana kama utalii na vitu vingine kwa sababu kila mtu anaulizia Tanzania.”

“Ulimwengu wa sasa mtu atatafuta vitu vingi kuhususiana na Tanzania, ata-google rasilimali zilizopo, michezo, utalii, kwa hiyo ushindi wa Simba umetuweka katika ramani nzuri sana duniani.”

“Jitihada na bidii lazima ziongezeke, watanzania tuiunge mkono Simba, wana kikosi kizuri sana na watu wameona mpira walioucheza.”

“Nimpongeze sana Mohammed Dewji na uongozi mzima wa Simba kwa kazi nzuri ambayo wameifanya pamoja na watanzania ambao wamekuwa nyuma ya Simba.”
.
.
Kusaga anasema yeye ni shabiki wa Pan Afrika😂😂 lakini kwa sababu ya utaifa yeye na Clouds Media walijitolea kuhakikisha Simba inapata support kadiri inavyowezekana.

Kusaga katoa tiketi 100 kuishuhudia Taifa Stars

$
0
0

Katika kuhakikisha mashabiki wanaujaza uwanja wa taifa kuishangilia Taifa Stars itakapocheza dhidi ya Uganda Jumapili ijayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Joseph Kusaga ameahidi kutoa tiketi 100 bure kwa mashabiki.

Kupitia #HiliGame ndani ya #PowerBreakfast PJ na KP walimuomba Kusaga kutoa tiketi 100 kwa ajili ya mashabiki na mchongo huo ukatiki.

“Hizo tiketi 100 zishatoka, nitazitoa kabisa. Naomba shabiki atakaepiga simu ili kujishindia tiketi aanze kwa kusema #NaiombeaUshindiTaifaStars.

“Jana niliongea na wakuu wa vipindi Shaffih na Sebastian na tumekubali kwa moyo wa kizalendo kama vijana wa kitanzania ambao tumepata nafasi ya kuwa na platform ya kusaidia maendeleo na mambo mengine nguvu zetu zote tunazielekeza kuhamasisha watanzania kwenda mbele kwenye mambo mengi sio mpira pekeyake.”

Utatengenezwa utaratibu halafu mashabiki watajulishwa jinsi ya kujishindia tiketi hizo zitakazowapa fursa ya kushuhudia mechi uwanja wa Taifa wakati Taifa Stars ikiwa kwenye harakati za kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya AFCON 2019.

Ruvu Shooting mikononi mwa Simba

$
0
0

Simba baada ya kufanya yake Jumamosi iliyopita kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, leo inarudi kupambania kombe la ligi kuu Tanzania bara kwa kucheza na Ruvu Shooting palepale kwenye uwanja wa taifa.

Wakati bado Simba ikiwa inasherekea kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa itakuwa pia ikihitaji pointi 3 kutoka kwa Ruvu Shooting ili kuendelea kuzikimbiza Azam na Yanga kwenye mbio za ubingwa.

Mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilipokutana October 28, 2019 Simba ilishinda 5-0 mbele ya Ruvu Shooting.

Ruvu Shooting haina matokeo mazuri siku za hivi karibuni, katika mechi 8 zilizopita imeshinda mechi mbili, sare 5 na kupoteza moja. Wakati Simba imeshinda mechi 7 za ligi kuu zilizopita.

Huu ni mchezo wa 21 kwa Simba msimu huu na endapo itashinda itafikisha pointi 54 lakini itaendelea kubaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam yenye pointi 59 baada ya kucheza mechi 28 lakini pia vinara wa ligi Yanga wenye pointi 67 baada ya kucheza mechi 28.

“Tanzania inakwenda AFCON”-Amunike

$
0
0

Taifa Stars inaendelea na maandalizi ya mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 dhidi ya Uganda mchezo ambao umepangwa kufanyika siku ya Jumapili March 24, 2019 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 12:00 jioni.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amesema mbele ya waandishi wa habari kwamba anafahamu kiu ya watanzania pia amesema kwa morali aliyoiona kwa wachezaji wake siku za karibuni anaamini watanzania watafurahi na kupata wanachotegemea.

Takwimu za Simba na TP Mazembe hatua ya makundi

$
0
0

Draw ya ligi ya mabingwa Afrika hatua ya robo fainali imepangwa, watu wengi walikuwa wanataka kujua nani anakutana na nani hatimaye wameshajua. Mnyama anarudi tena Congo DR baada ya kupangwa na TP Mazembe.

Mechi za kwanza zitachezwa kati ya April 5 na 6 halafu marudiano ni kati ya April 12 na 13, 2019. Simba itaanzia nyumbani na kwenda kumalizia ugenini.

TAKWIMU

SIMBA SC (Kundi D)
-Imecheza mechi 6
-Imehinda mechi 3
-Imepoteza mechi 3
-Sare 0
-Pointi 9 (imemaliza nafasi ya pili kwenye kundi)

Magoli⚽
-Imefunga magoli 6
-Imefungwa magoli 13

TP MAZEMBE (Kundi C)
-Imecheza mechi 6
-Imeshinda mechi 3
-Imepoteza mechi 1
-Sare 2
-Pointi 11 (imeongoza kundi)

Magoli⚽
-Imefunga magoli 13
-imefungwa magoli 4

Makocha waliokimbia/kutimuliwa ligi kuu

$
0
0

Msimu wa ligi kuu Tanzania bara 2018/19 ukiwa unaelekea ukingoni kuna vilabu vingi havipo tena na makocha ambao walianzanao msimu huu kutokana na sababu mbalimbali.

Waliotimuliwa

Mohamed Abdallah Bares (TZ Prisons)
Ally Bushiri (Mbao)
Dragan Popadic (Singida United)
Hans van Pluijm (Azam FC)

Walioondoka/Kukimbia wenyewe

Mbwana Makata (Alliance)
Soccoia Lionel (African Lyon)
Amri Saidi (Mbao)
Hemed Morocco (Singida United)
Hitimana Thiery (Biashara United)
Niyongabo Amas (Stand United).

Waliosimamishwa

Bakari Shime (JKT Tanzania)

CHUKUA HII…

Singida United na Mbao FC zikiajiri makocha wapya, zitakuwa zimefundishwa na makocha watatu tofauti ndani ya msimu mmoja!!

Kumbe wachezaji wa Singida walikuwa wanapigwa!!

$
0
0

Mkurugenzi wa Singida United amesema miongoni mwa sababu za kuachana na aliyekuwa kocha wao Dragan Popadic ni pamoja na kocha huyo kuwapa vichapo wachezaji wakiwa mazoezini.

“Kukosekana mahusiano mazuri kati ya kocha na benchi lake la ufundi pamoja na wachezaji. Alikuwa akilalamikiwa na wenzake kwamba hapokei ushauri. Wachezaji walimlalamikia kwamba anawapiga wanapokuwa mazoezini pia mchezaji akikosea kwenye mechi anatolewa fasta.”

“Tumeachana naye akiwa hatudai lakini sababu kubwa ya kuachana naye ni uhusiano mbovu kati yake na wasaidizi wake pamoja na wachezaji.”

Kwa sasa timu ipo chini ya Fred Felix Minziro.


Mbao yamdondosha Salum Mayanga

$
0
0

Uongozi wa Mbao FC umefikia makubaliano na Salum Mayanga kuwa kocha wao mkuu kuchukua nafasi ya Ally Bushiri ‘Benitez’ ambaye amesitishiwa mkataba kutokana na mwendelezo wa matokeo mabovu ya klabu hiyo.

Inaelezwa kuwa, Mayanga amesaini mkataba wa kuifundisha mbao hadi mwisho wa msimu huu. Imebakiza mechi 8 za ligi kuu (tayari imecheza mechi 30) na kufanikiwa kukusanya pointi 36.

Kabla ya kutua kwa ‘Wabishi’ Salum Mayanga alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Mtibwa Sugar huku pia akiwa amewahi kuwa kocha timu hiyo pamoja na Tanzania Prisons kwa nyakati tofauti.

Mayanga amewahi kufundisha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kabla ya kocha wa sasa Emmanuel Amunike.

Gyan “Mimi ni chui, waandishi hawanitishi”

$
0
0

Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan ameviomba vyombo vya habari vya Ghana kuwa vitumie muda kuhamasisha timu yao ya taifa na mashabiki kwa ujumla katika safari yao ya Misri kuliko kuwekeza muda mwingi kuchimba madhaifu pekee.

Timu ya taifa ya Ghana ina ukame wa miaka 37 tokea itwaje taji la mataifa huru Barani Afrika.

“Najua mapungufu ni mengi sana katika timu yetu ya taifa. Nafahamu piaa media zimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya soka hapa nchini lakini wasikatishwe tamaa na changamoto ambazo zinaibuka kila kukicha.” Gyan


“Mimi nina roho ya chui sitetereki hata kama nikikosolewa, nishazoea. Hofu yangu kubwa ni kwa vijana wapya kwenye kikosi hawajakomaa kuvumilia matatizo.”

“Sijasema media zisikosoe, la Hasha! Wakosoea lakini washauri pia. Lengo letu sote ni moja, kuhakikisha tunanyakua taji hilo.” Gyan

Mchezaji apoteza maisha kwenye ajali ya gari

$
0
0

Kiungo wa klabu ya Free State ya nchini Afrika Kusini, Sinethemba Jantjies amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30.

Sinethemba amepata ajali ya gari wakati gari lake lilipogongana na gari lingine mapema hivi leo asubuhi.

Msimu huu Sinethemba alicheza michezo 23 na kufunga magoli 4 pamoja na kutengeneza goli moja.

Alianzia soka lake kunako klabu ya Mbombela, kabla hajajiunga na Free State.

Hata hivyo Sine alisaini mkataba wa awali na klabu ya Bidvest ambayo alipaswa kujiunga nayo mwezi julai mwaka huu.

Mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA yazinduliwa rasmi Manyara

$
0
0

Mashindano ya mwaka 2019 ya Copa Coca-Cola UMISSETA yamezinduliwa rasmi mkoani Manyara leo ikiendeleza juhudi za Kampuni ya Coca-Cola kuunga mkono michezo mashuleni hapa nchini.

Uzinduzi huo umefanyikia katika Uwanja wa Kwaraa wikiendi hii, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akisubiria kuvalishwa kitambaa cha Scarf mara baada ya kuwasili mkoani Manyara kwa ajili ya kuzindua mashindano ya mwaka 2019 ya Copa Coca-Cola UMISSETA.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa Serikali, maofisa michezo, walimu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Manyara.

Akizundua michezo hiyo mkoani Manyara, Waitara aliishukuru Coca-Cola kwa kuwezesha michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA kuzinduliwa rasmi mkoani humo kwa mara ya kwanza huku akiwahimiza vijana wa Manyara kuthibitisha vipaji vyao dhidi ya mikoa mingine kupitia mashindano hayo.

“Ningependa kuwahimiza vijana wa mkoani hapa kuifanya hii michezo kuwa sehemu ya kujifunza zaidi na njia ya kuongeza ushiriki katika shughuli za nje ya masomo. Tofauti na siku za nyuma, Michezo siku hizi ni biashara yenye thamani kubwa, na kila mmoja wenu hapa anaweza kuwa shahidi ya hili,” alisema.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola kwa mwaka 2019 iliyofanyika mkoani Manyara hivi karibuni.

Alibainisha kuwa, kumbukumbu zinaonyesha kwamba kuna idadi kubwa ya vijana mkoani Manyara ambao vipaji vyao viligunduliwa kupitia michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA na sasa wanashiriki katika ligi za juu tofauti tofuati.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bonite Bottlers mkoani Manyara, Samwel Bitalian alisema, kupitia michezo, Coca-Cola imedhamiria kuwafika wanafunzi wengi nchini kadri iwezekanavyo ili kuwapa fursa ya kushiriki katika michezo hiyo na kuvumbua vipaji.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akifurahia jambo na Mwakilishi wa Kampuni ya Coca-Cola, Pamela Lugenge wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA kwa mwaka 2019 yaliyofanyika mkoani Manyara hivi karibuni.

Kama sehemu ya udhamini wa mashindano hayo, Kampuni ya Coca-Cola itasambaza vifaa vya michezo zaidi ya 2000 katika shule za sekondari nchini.

Uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA, katika ngazi ya mkoa katika mkoa wa Manyara ni wa tano tangu kuanzishwa kwa michezo hiyo mkoani Dodoma kasha Tanga, Zanzibar na Mtwara. Katika ngazi ya Kitaifa michezo hiyo itafanyikia Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara mwaka huu.

Abdi Banda Mwamba wa Chuma usiotingishwa na kutu

$
0
0

::
📅Tarehe kama ya leo Abdi Banda “Mwamba wa Chuma” alizaliwa. Ni mmoja kati ya mabeki wenye uwezo wa hali ya juu. Katika mambo makubwa aliyojaliwa ni uwezo wake wa kucheza nafasi tofauti uwanjani. Ana uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto, beki wa kati na hata kiungo mkabaji. kabla ya yote heri ya mwaka mpya mwamba.
::
📈Katika ligi ya Afrika Kusini kicha ya Abdi Banda kucheza mechi chache ndiye beki namba 5 aliyesafisha mashambulizi hatari zaidi akiwa na wastani wa kufanya hivyo mara 15 kila mchezo huku akiwa amecheza mechi 13 pekee.
::
📉Aina yake ya uchezaji na umbo lake kwa mbali unaweza ukaona miondoko ya Virgil Van Djik wa Liverpool. Van Djik amekuwa na wastani mkubwa wa kuondosha mipira ya kichwa kutokaba na Umbile lake, huku Abdi Banda akishilikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu katika ligi ya Afrika Kusini, ambaye ameondosha mipira ya juu kwa asilimia 70.
::
📊Abdi Banda huyo kumbuka anasumbuliwa sana na majeraha. Msimu wake wa kwanza alicheza mechi 28 na kufunfa mabao matatu, msimu huu mechi 13 na kufunga bao 1
2019: ⚽ vs Black Leopard (1 – 2)
2017: ⚽ vs Orlando Pirates ( 1 – 1) Mechi yake ya 2 ligi kuu tokwa asajiliwe.
2017: ⚽⚽ vs Bloemfontein (2 -2 )
::
🥾NJE YA SOKA: Mbali na soka Abdi ni mchezaji nadhifu sana ambaye inasemekana anaweza kuwa miongoni mwa nyota watano wanaotupia pamba kali sana. Banda ni shemeji wa mwanamuziki nguli nchin hapa Ali Kiba.
::
💰THAMANI: Thamani ya Banda inakadiriwa kuwa yeye ni mchezaji wa tatu kwa thamani hapa bongo. Banda beki mwenye thamani kubwa sana Tanzania ikikadiriwa kufikia Shilingi bilion 2, thamani hiyo inamfanya kuwa beki mwneye thamani kubwa Afrika Mashariki. Katika kikosi cha Baroka Banda ndiye mchezaji wa pili mwenye thamani kubwa.
::
🔋MAENDELEO YAKE: Huu ni msimu wake wa pili katika kikosi cha Baroka na tayari amekwisha kuaminika kiasi cha kukaimu mara kadhaa kitambaa cha unahodha.
::
⚠KWANINI HAJACHEZA SANA: Msimu huu mambo yake hayajaenda sawa mara baada ya kupatwa majeraha akiwa na kikosi cha timu ya taifa mwezi novemba mwaka jana, lakini pia alilazimika kukaa nje miezi mitatu baada ya kuumia nyonga mwezi wa 1 mwaka huu.
::





Latest Images