Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

MASAU BWIRE AGOMEA KUFUNGWA NA SIMBA, AELEZA MIKAKATI YAO

$
0
0
Masau Bwire Afisa habari wa klabu ya Ruvu Shooting
Masau Bwire Afisa habari wa klabu ya Ruvu Shooting

 

Baada ya tambo nyingi kabla ya mchezo dhidi ya Simba na hatimaye kufungwa 2-1 jana, Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amejitetea kwa kusema kwamba, timu yake ilicheza vizuri sana lakini bahati haikuwa upande wao.

Msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi aliongeza kwamba, hii si kwa timu yake tu bali timu yoyote inaweza kucheza vizuri lakini kama bahati haipo kwao siku hiyo, basi ushindi hauwezi kupatikana.

“Nilisema tangu jana kwamba timu inaweza kucheza vizuri, ukawa na uwezo wa kushinda lakini kama bahati haikulalia kwako upande huo, hauwezi ukapata ushindi. Ni bahati ambayo imetufikisha katika matokeo haya ambayo si ya kufurahisha kwa upande wetu,” alisema

“Lakini hakika bado tunaendelea na mapambano na bado vijana wana ari, bado timu yetu tuna imani kubwa kwamba tutafanya vyema. Ni mchezo tu wa kwanza huu katika michezo mitatu tumepoteza, hatukupoteza tu kwasababu kwamba uwezo wetu ndiyo umefika hapa,

Bwire alisema kwamba, licha ya kipigo hicho lakini vijana wake walionesha ari na upambanaji mkubwa na kuongeza kuwa anaamini mwalimu ameyaona mapungufu na kuyafanyia kazi ili kuendeleza mapambano kwenye michezo ijao.

“Tumepoteza kama nilivyosema kwamba haikuwa bahati yetu, lakini mpira umeuona vijana wamepambana, vijana wameoesha na hiyo ndiyo staili yetu tutakayokwenda nayo,”

“Haya mapungufu yaliionekana katika Uwanja wa Uhuru hii leo (jana), mwalimu Seleman Mtungwe ameyaona na anakwenda kuyafanyia kazi na nina hakika kwamba marekebisho hayo yatafanyika kwa usahihi na tutakwenda kufanya vizuri,”


MANCHESTER DERBY- MATUKIO TISA YA KUKUMBUKWA YA MOURINHO VS GUARDIOLA

$
0
0

pep-vs-mouKuelekea pambano la mahasimu wa Jadi kati ya Manchester United na Manchester City, kuna vita kubwa kati ya makocha wawili mahasimu wakubwa Jose Mourinho na Pep Gaurdiola.

Mourinho na Guardiola ni makocha wenye upinzani pindi wanapokutana hasa wakati wakiwa nchini Uhispania, wakati huo Mourinho akiifundisha Real Madrid na Guardiola akiinoa Barcelona.

Sasa kuelekea mchezo huo wenye msisimko wa aina yake kuna matukio kadhaa ya kukumbukwa pindi wawili hawa walipokutana siku za nyuma.

INTER 0-0 BARCELONA | Septemba 2009 | Champions League | Hapo ndipo upinzani wao ulipoanza. Maswahiba hao wawili wa zamani wakati wakiwa Barcelona kwa mara ya kwanza kabisa, walikutana kama wapinzani katika dimba la San Siro kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2009-10. Katika mchezo huo Barcelona walitawala kwa kiasi kikubwa lakini wakashindwa kupata goli.

BARCELONA 2-0 INTER | Novemba 2009 | Champions League | magoli ya mapema kabisa kutoka kwa Gerard Pique na Pedro Rodriguez yalimpa Guardiola ushindi wa kwanza dhidi ya mpinzani wake huyo. Hapakuwa na maneno yoyote ya kejeli, lakini ni Xavi tu ndiye alisema: “Tulipata nafasi nyingi sana za kufunga, Inter hawakuwa na kitu.”

INTER 3-1 BARCELONA | April 2010 | Champions League | Barca walisafiri mpaka Milan kwaajili ya nusu fainali Champions League dhidi ya Inter Milan. Licha ya kuwa waliwapa ugumu Inter wakati wa michezo ya hatua ya makundi, Wakatalunya hao walijikuta wakitokota na kuchapwa vijana hao wa Mourinho na kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu.

BARCELONA 1-0 INTER | April 2010 | Champions League | Haukuwa mchezo mgumu kwa Mourinho na Inter yake kwani tayari walikuwa na hazina ya mabao 3-1. inter walitumia muda mwingi kucheza mchezo wa kujilinda katika dimba la Camp Nou. Thiago Motta alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Sergio Busquets. Baada ya hapo Barca waliendelea kutawala mchezo lakini wakafanikiwa kupata bao moja tu lililofungwa na Gerard Pique na kutupwa nje. Mourinho alishangilia mithili ya mtu aliyechanganyikiwa.

BARCELONA 5-0 REAL MADRID | November 2010 | La Liga | Kitendo cha Mourinho la kuwazuia Barca kushinda taji la Champions League kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu akiwa Inter kikampa kazi Real Madrid. Alipewa jukumu madhubuti kwaajili ya kuondoa utawala wa Wakatalunya hao katika La Liga, lakini mwanzo wake haukuwa mzuri. Wakati wakikutana katika mchezo huo Madrid walikuwa hawajafungwa huku wakiwa wanaongoza ligi. Katika mchezo huo, Barcelona walionesha kiwango ambacho kinasemekana ni bora kuwani kutokea kwenye mechi za muda wote za El Classico.

REAL MADRID 1-1 BARCELONA | April 2011 | La Liga | Wakati timu hizi zikikutana, mbio za ubingwa zilikuwa bado zinaendelea. Huu ulikuwa ni mchezo wa El Clasico uliofanyika ndani ya siku 18 baada ya El Clasico nyingine. Mchezo huu ulikuwa mgumu kwasababu kila timu ilikuwa ikisaka nafasi ya kutwaa La Liga, Copa del Rey na vilevile nafasi ya kutinga fainali ya Champions League, ambapo katika mechi zote hizo, timu hizo zilikuwa zinaenda kukutana.

BARCELONA 0-1 REAL MADRID | April 2011 | Copa del Rey | Akiwa katika msimu wake wa kwanza, Mourinho aliipa Real Madrid taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993 kwa bao pekee lililofungwa kwa kichwa na Cristiano Ronaldo katika muda wa ziada. Iker Casillas aliwanyima kabisa nafasi za kufunga Andres Iniesta na Pedro kwenye kipindi cha pili. Angel Di Maria alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

REAL MADRID 0-2 BARCELONA | April 2011 | Champions League | Huu ulikuwa ni moja ya michezo ya iliyojaa jazba ya kubwa kuwahi kutokea kwa timu zinazofundishwa na Guardiola and Mourinho. Katika mchezo huo Pepe aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa nne wa Real Madrid kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika michezo minne mfululizo za El Clasico, na Mourinho pia alitolelewa kwenye benchi lake. Kutolewa kwa Pepe kuliwapa nafasi nzuri Barca na ndipo Lionel Messi akawawasha mara mbili, huku goli la pili likiwa ni moja ya magoli bora kwenye historia ya Champions League. Kipigo hiko cha Madrid kilipelekea Mourinho kuwakashifu Barca, UEFA na Unicef wakati wa mkutano na wanahabari baada ya mchezo huo.

BARCELONA 1-1 REAL MADRID | May 2011 | Champions League | Huu haukuwa kama mchezo wa awali ambapo Real walilala 2-0. Huu ulikuwa ni mchezo uliokuwa umejaa burudani ya aina yake na usiokuwa na utata wowote. Mourinho hakuwa kwenye benchi la ufundi kutokana na kufungiwa kwenye mchezo wa awali. Aliamua kupanga kikosi kilichokuwa ni ‘attacking minded’ ili kupata matokeo dhidi ya Barca. Gonzalo Higuain alifunga goli la mapema lakini lilikataliwa kutokana na kufanya madhambi kabla ya bao hilo kupatikana. Pedro aliifungia Barca goli la kuongoza, kabla ya Real kusawazisha kupitia Marcelo licha ya goli licha ya goli hilo kutokuwa na manufaa yoyote kwa timu yake na Barca wakatinga moja kwa moja fainali nyingine ya Champions League.

FLAMINI APATA SHAVU LINGINE EPL BAADA YA KUACHWA ARSENAL

$
0
0

1Crystal Palace wamethibisha kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa Arsenal Mathieu Flamini kwa uhamisho huru.

Flamini (32), amekuwa mchezaji huru tangu alipoachwa na Arsenal katika dirisha la kiangazi lililofungwa hivi karibuni, akiwa ameichezea tu hiyo mechi 24 tu msimu uliopita.

Baada ya kukamilisha usajili huo, Flamini alisema: Crystal Palace ni klabu yenye matarajio makubwa ikiwa na wachezaji wazuri na nasubiri kwa hamu kutoa mchango wangu klabuni. Ni changamoto nzuri kwangu na kwa hakika nina furaha kubwa kuwa hapa.

Nimekuwa na wasaa mbalimbali wa kujadili juu ya kujiunga na klabu hii na Alan Pardew na amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kufikia maamuzi haya.”

Alan Pardew, ambaye hapo awali alionesha dhamira ya wazi kumhitaji kwa mkopo kiungo Jack Wilshere kutoka Arsenal kabla ya kuelekea Bournemouth, amesema: “Nilihisi kulikuwa na umuhimu mkubwa sana kupata mchezaji mwingine kwenye eneo la kiungo. Uwezo wake mkubwa uwanjani utasaidia lakini pia uwezo wake wa kuwa kiongozi uwanjani, kupiga pasi na kukaba utakuwa msaada mkubwa kwa timu.

WENGER ADHIHIRISHA CHUKI ZAKE DHAHIRI DHIDI YA MOURINHO

$
0
0

1Arsene Wenger na Jose Mourinho bado wanaonekana kuwa na bifu zito baada ya kuzua tafrani kwenye mkutano wa UEFA maalum kwaajili ya makocha wa timu mbalimbali wenye mafanikio makubwa uliofanyika wiki iliyopita.

Gazeti la michezo la Marca kutoka nchini Uhispania limeripoti kuwa Wenger alikataa kuruhusu Mourinho akae mbele yake wakati Sir Alex Ferguson akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo huko Nyon.

This handout picture released by UEFA shows (LtoR, front row) Juventus' coach Massimiliano Allegri, Manchester United's coach Jose Mourinho, UEFA Coaching Ambassador Sir Alex Ferguson, UEFA interim General Secretary Theodore Theodoridis, Bayern Munich's Carlo Ancelotti, Paris Saint Germain's coach Unai Emery and Real Madrid's coach Zinedine Zidane. (LtoR second row) UEFA Chief Refereeing Officer Pierluigi Collina, Gent's head coach Hein Vanhaezebrouck, Newcastle United's coach Rafael Benitez, FC Zenit's coach Mircea Lucescu, Arsenal's coach Arsene Wenger, FC Barcelona's coach Luis Enrique, Wolfsburg's coach Dieter Hecking, Dynamo Kiev's coach Serguei Rebrov, UEFA director of competitions Giorgio Marchetti and UEFA chief technical officer Ioan Lupescu posing for a picture during a session of the Elite football Club Coaches Forum at the UEFA headquerters in Nyon, on August 31, 2016

Akiwa amewasili kwenye mkutano huo kwa kuchelewa, meneja huyo wa Manchester United aliuliza kama angeweza kukaa kwenye moja ya baadhi ya siti zilizokuwa wazi na hapo ndipo Wenger alipoingilia kwa kusema: “Hapana, haiwezekani.”

Baada ya tukio hilo ilibidi Mourinho aangalie sehemu nyingine ya kukaa kwa usaidizi wa watu waliokuwa wakitoa huduma mkutanoni hapo.

Ikumbukwe kwamba, Mourinho na Wenger wamekuwa hawana uhusiano mzuri kwa kipindi kirefu.

Miaka miwili iliyopita, Mourinho, wakati huo akiwa meneja wa Chelsea alimbandika jina Wenger kwamba ni mtaalamu wa kufeli “specialist in failure” baada ya kukaa Arsenal miaka tisa bila kuchukua taji lolote.

Baadaye tena alikataa kuomba radhi mpaka pale Arsene Wenger alitangulia kuomba radhi kwa kumwambia mreno huyo kwamba ni muoga wa kufeli.

Mwaka 2005, kipindi chake cha mwanzo akiwa Chelsea, Mourinho alimkandia sana Wenger na hata kufikia hatua ya kumfananisha na mpiga chabo “voyeur” baada ya kuwa anaizungumzia Chelsea kupita kiasi, licha kwamba baadaye aliomba radhi.

Hiki ndio Kisa cha Madrid kuwapeleka mahakamani Benfica 

$
0
0

Real Madrid wameripotiwa kuwapeleka mahakamani klabu ya Benfica juu ya mauzo ya mchezaji wa kiargentina Ezequiel Garay kwenda Zenit Saint Petersburg.

Madrid, ambao walimuuuza Garay kwenda Benfica mnamo mwaka 2011, walikuwa na haki ya kupata 50% ya mauzo yoyote ya mbeleni ya Garay na wanaamini  mauzo yake ya kwenda Zenit yalikuwa chini ya thamani. 

Ripoti kutoka gazeti la Diario De Noticias kwamba Los Blancos wamegundua kwamba Bayern Munich walitaka kumsajili Garay akiwa Benfica, na waliweka ofa ya €15m mezani, ofa iliyokataliwa na klabu ya Ureno. 

Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Garay akauzwa kwenda Zenit kwa ada ndogo ya 6 million euros.
Benfica walikuwa na haki ya kupata asilimia 40% tu ya mauzo ya mchezaji, asilimia 10 ilikuwa haki ya mmiliki wa 3 – Benfica Stars Fund. 
Garay, 29, ambaye aliihama Madrid kama sehemu ya dili la Madrid kumsaini Fabio Coentrao, Garay alijiunga na Madrid akitokea Valencia kwa €20m.
Kesi hii ya Madrid vs Benfica itatolewa maamuzi baadae mwezi huu na mahakama ya michezo duniani – CAS. 

Sanchez anaamini anaubora sawa na Ronaldo na Messi

$
0
0

messi-ronaldo-sanchez

Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez asema yupo katika daraja moja na mastaa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Akikaririwa na gazeti la kila siku la Spain, Sport, Sanchez alisema: “Nimefikia kiwango ambacho ninaweza kushindana na wachezaji mahiri. Sijioni mnyonge kwa yeyote yule”

“Ninalinganisha ubora wangu na Messi na Ronaldo. Nina uwezo sawa kama wao”

Sanchez alijiunga Arsenal akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho wa Paundi Milioni 30 miaka miwili iliyopita na ameweza kuisaidia Arsenal kushinda makombe mawili ya FA na pia kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Premier League msimu uliopita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile pia ameweza kuisaidia nchi yake kushinda kombe la Copa America lililoisha hivi karibuni, ikiwa ni mafanikio ya kushinda kombe hilo mara mbili mfululizo, walipoifunga Argentina ya Lionel Messi kwa michumo ya penati.

Sanchez, 27, alikuwa nahodha wa Chile walipotoka suluhu na Bolivia, Jumanne hii iliyopita. Huo ukiwa ni mwendelezo wa matokeo mabaya kwa timu yao katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia.

Chile wameshinda mechi tatu tu katika mechi zao nane zilizopita za kufuzu na wapo pointi mbili nyuma kutoka katika nafasi ya kufuzu kwenda Urusi (Kombe la Dunia), Sanchez alisema alikasirishwa na kitendo cha Bolivia kupoteza muda.

“Sikukubali! Walinifanya nitake kuwazuia na niendelee kucheza”, alisema. “Hizo ni dakika unazopoteza. Na mwisho, walituweza.”

Striker wa Simba aelekea uarabuni kufanya majaribio

$
0
0

img_0025

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Danny Lyanga amesafiri kuelekea Oman kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye timu ya Oman Club.

Haji Manara amethibisha taarifa za kuondoka kwa Lyanga na kusisitiza mchezaji huyo amefuata taratibu zote na kuruhusiwa na klabu yake.

“Danny Lyanga amekwenda Muscat, Oman kwa ajili ya kufanya majaribio kwa muda wa wiki mbili kwenye timu ya Oman Club na kama atafanikiwa sisi Simba hatuna tatizo katika kumwachia mchezaji kwenda kucheza soka la kulipwa”, amethibitisha Haji Manara afisa habari wa klabu ya Simba.

“Oman Club ni timu kubwa, ni kama Simba au Yanga kwa Tanzania, kama atafanikiwa ni faida kwake, kwa klabu na taifa. Ameonfoka kwa kufuata taratibu zote za Simba.”

Lyanga amekuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na uwepo wa wageni Hamisi Kiiza (msimu uliopita), Mavugo, Blagnon na mzawa Ibrahim Ajib (msimu huu).

Jicho la 3: Simba ya Omog na pointi 7 ni afadhali ya msimu uliopita… 

$
0
0

img_0069

Na Baraka Mbolembole

Uliona goli ambalo Vicent Angban alilofungwa na Wazir Junior katika game ya Simba SC 0-1 Toto African msimu uliopita? Uliona goli la Omari Mponda alilomfunga golikipa huyo raia wa Ivory Coast katika mechi ya kufungua msimu huu, Simba 3-1 Ndanda FC? Umeona namna Abdulrahiman Musa alivyomchungulia kipa huyo wa Simba na kufunga goli la umbali kiasi katika game ya Simba 2-1 Ruvu Shooting?

Simba tayari wamefanikiwa kukusanya alama 7 katika michezo mitatu waliyokwisha cheza msimu huu! Ni kiwango pungufu ukilinganisha na namna walivyoanza msimu uliopita mwaka mmoja nyuma. Ushindi dhidi ya Ndanda ulikuwa ni wa ‘wasiwasi mwingi,’ na suluhu-tasa mbele ya JKT Ruvu ukaanza kuleta mashaka kama kweli timu hiyo inaweza kumaliza ukame wa miaka minne bila taji la VPL.

Nilishasema kwamba timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi inahitaji vipaji bora zaidi ili kushinda taji hilo waliloshinda kwa mara ya mwisho msimu wa 2011/12.

Ukilinganisha na wapinzani wao wa sasa katika mbio za ubingwa, timu za Yanga SC iliyoshinda mataji matatu katika misimu minne iliyopita ( 2012/13, 2014/15, na 2015/16) na Azam iliyoshinda taji lake pekee 2013/14 (pasipo kupoteza mechi,) utaona Simba haina ubavu wa kushinda taji hilo.

Matatizo ya kiutawala yaliinyima timu hiyo nafasi ya ubingwa msimu uliopita, na badala ya kuanzia pale walipoishia msimu uliopita wameanza upya kabisa na matokeo yake yanaanza kujidhihirisha mapema.

Walipata ushindi kwa mara ya kwanza baada ya kupita kwa miaka mitatu katika uwanja wa Mkwakwani, Septemba 2015. Ilikuwa ni dhidi ya timu dhaifu na ambayo ilicheza zaidi ya michezo 8 pasipo kufunga goli-African Sports ambayo ilikuwa ikicheza Ligi kuu kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa miaka 23.

Ushindi huo wa 2-0 uliambatana na utambulisho wa mshambulizi mpya (wakati huo,) Mganda, Hamis Kiiza. Wakaifunga kwa mara ya kwanza JKT Mgambo katika uwanja wa Mkwakwani baada ya kushindwa kuifunga timu hiyo katika misimu mitatu ya nyuma.

Wakaondoka, Tanga wakiwa na alama 6, na kurejea Dar es Salaam kucheza na timu ‘inayowasumbua’ sana, Kagera Sugar. Kiiza akafunga ‘Hat-trick’ na kufikisha goli tano katika game tatu. Msimu huu, mechi zote 3 wamecheza Dar na watacheza pia na Mtibwa Sugar wikendi hii, kisha Azam na Yanga. Nini kitatokea?

Ni kuanza kupoteza mwelekeo wa kikosi cha kocha Mcameroon, Joseph Omog na msaidizi wake, Mganda, Jackson Mayanja. Itazame, Simba inavyocheza, wapo ‘legelege,’ hawana ubunifu katikati ya uwanja, huku benchi la ufundi likishindwa kujua ni yupi anafaa kuwa straika namba moja kati ya Mrundi, Laudit, Mavugo na Ibrahim Ajib.

Omog hajui ni kwanini timu yake inashambulia vizuri akiwepo, Mudhamir Yassin katikati ya uwanja na inapwaya asipokuwapo. Mayanja hamwambii chochote, golikipa Vicent kuhusu makosa yake ya kutoka hovyo na kuwa mbali na goli lake.

Hernandez anawasoma, Hans atawaadhibu, Salum Mayanja anatamani muendelee kucheza hivyo hata ykatika game yenu ya Jumapili ijayo.

Mimi si kocha, ila katika ‘lugha ya miili’ ya wachezaji wengi wa nafasi ya ulinzi katika VPL wanamuhofu sana, Ajib kuliko mchezaji mwingine yeyote yule.

Lakini nilishangazwa na Omog pale alipoamua kumuweka benchi kijana huyo katika game dhidi ya JKT Ruvu na kumuanzisha, Muivory Coast, Federick Blagnon sambamba na Mavugo kisa tu mchezaji huyo wa kulipwa alifunga goli la kufungua ugumu dhidi ya Ndanda akitokea benchi katika game ya ufunguzi.

Nilishangazwa zaidi na mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakimshutumu Ajib na kumuita ‘mbinafsi.’ Kwa mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji, ili kuwa bora na makini anapaswa kupiga mashuti mengi zaidi golini kwa kipa wa timu pinzani.

Bila kushuti golini hamtapa goli, na kama uwezo wenu ni mdogo kiufungaji hamuwezi kushinda mechi. Ajib ni kijana mdogo na bahati nzuri kila mechi amekuwa katika kiwango kipya kinachopanda. Huyu ndiye anapaswa kuwa mshambuliaji namba moja na ili Simba ipate magoli inapaswa imtazame Ajib katika mifumo yote ya kiuchezaji. Vinginevyo hakuna magoli.

Mavugo vs Ajib, kwa kocha yeyote chaguo la kwanza kiufungaji ni Ajib. Anatisha sana kwa walinzi wa timu pinzani, anakasi, mjanja wa kutafuta mikwaju ya penalti, ana penda kushuti golini, na amekuwa na mtazamo wa kufunga tu kila anapokuwa uwanjani. Wote, yeye na Mavugo wamefunga magoli mawili mawili katika game 3 za mwanzo wa msimu.

Wakati, Mzimbabwe, Justice Majabvi alivyotangaza kuachana na timu hiyo kwa sababu za kifamilia, niliamini Simba ‘itasafa’ kumpata kiungo makini wa ulinzi ambaye ni kiongozi shupavu kwa wenzake. Lakini naona wamempata haraka sana, lakini Omog ni kama ilivyo kwa wachezaji wake Mwinyi Kazimoto na nahodha, Jonas Mkude ni ‘vipima joto.’

Leo vipo juu lakini kesho havipo juu, hali ya hewa na mabadililo yake yanapelekea tofauti hiyo. Uliona Simba ilivyocheza dhidi ya Shooting baada ya kuingia kwa Mudhamir? Uliona nini? Nitawaambia siku nyingine, ila katika kikosi cha kocha makini, Mudhamir hakai benchi.

Bado hakuna beki makini zaidi ya Juuko Murishid katika safu ya kati. Baada ya mechi 3 zijazo mtamuona yule ‘kibabu’ wenu, Method Mwanjali alivyo dhaifu. Vicent endelea kutoka golini, Omog endelea kubahatisha katika upangaji wa timu, mashabiki endeleeni kumuita, Ajib ‘mchoyo!.’ Msimu uliopita na sasa takwimu zimeanza kuwahukumu.


Picha 5: Juma Abdul alivyoamua kuja na mwonekano mpya

$
0
0

img_0183

Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul amekata nywele zake na kuacha zikiwa ndogo (unga) tofauti na aliyozoeleka kuonekana akiwa anayoa za pembeni na kuzifuga za katikati ya kichwa.

Kuna wakati mchezaji huyo aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita, aliweka rasta (dread) ikiwa ni moja ya style yake ya nywele.

Lakini kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ndanda FC uliochezwa mjini Mtwara, Juma alionekana kwa mara ya kwanza akiwa na nywele fupi kichwa kizima huku akiwa ameachia ndevu kwa mbali kama kawaida yake.

Hizi hapa picha tofauti zikionesha mwonekano mpya wa Juma Abdul.
img_0178 img_0179 img_0181 img_0185 img_0184

Nnauye ndani ya TFF

$
0
0

img_0051

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) kesho Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiwa TFF kuanzia saa 4:30 asubuhi, Waziri Nape atazungumza na Mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na Sekretarieti kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ambao TFF imewaalika katika ziara hiyo.

Katika ratiba hiyo, Nape ataoneshwa maendeleo ya michezo hususani mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya Airtel na kuratibiwa na TFF ambako kwa mikoa mbalimbali iliyofanya vema, kesho timu za wanawake na wanaume zitacheza hatua ya nusu fainali kabla ya fainali za Jumapili ambazo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Imetolewa na TFF

Ratiba ya VPL weekend hii

$
0
0

IMG_0515

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.

Miongoni mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui FC itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Mbali ya michezo hiyo, pia Young Africans itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati Azam FC ambayo itakuwa mgeni tena kwenye Uwanja wa Sokoine ikicheza na Mbeya City na kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Ndanda itaikaribisha Kagera Sugar ya mkoani Kagera.

Ligi hiyo itaendelea Jumapili Septemba 11, 2016 kwa Simba kuikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, lakini uliokuwa uzikutanishe timu za African Lyon na Mbao hapo kesho umesogezwa mbele hadi Jumatatu Septemba 12, 2016. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru baada ya African Lyon kubadili uwanja kutoka Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

GUARDIOLA AMJAZA UPEPO ZLATAN KUELEKEA MANCHESTER DERBY

$
0
0

pepBosi wa Manchester City Guardiola ameelezea heshima yake juu ya Zlatan Ibrahimovic na kusema kuwa ni moja ya wachezaji bora kabisa duniani licha ya kutokuwa katika maelewano mazuri wakati wakiwa Barcelona.

Guardiola alimpeleka Ibrahimovic kwa mkopo AC Milan baada ya wawili hao kushindwa kuelewana mwaka ambao Guardiola aliipa Barca makombe matatu (2009-10).

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Sweden (34), amekuwa akionesha chuki za wazi kutoka moyoni dhidi ya Guardiola na kumuita muoga na asiyejiamini.

Kuelekea mchezo huo wa Manchester derby, wakala mbwatukaji wa Ibrahimovic Mino Raiola amemtuhumu Guardiola kwa kusema ni kocha anayefundisha soka lisilovutia, lakini Guardiola amemsifu straika huyo wakati akiongea na wanahabari.

“Nina heshima kubwa sana kwa kile ambacho Zlatan amefanya katika soka,” amesema.

“Ni moja ya washambuliaji bora sana na bila shaka wachezaji bora huleta matokeo ya moja kwa moja pale wanapowasili kwenye timu.

“Baadhi ya wachezaji husubiri mpaka waizoee ligi husika, lakini wachezaji bora hufanya hivyo mapema sana.”

Kilimanjaro Queens yaelekea Uganda

$
0
0

Twiga 1

Baada ya jana Septemba 8, 2016 kuilaza Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’, inatarajiwa kuondoka leo kwenda Jinja, Uganda kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) maarufu kama Kombe la CECAFA itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016.

Burundi pia inakwenda Uganda ambako imepangwa makundi tofauti katika michuano hiyo. Tanzania kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda,.

Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016 kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16, 2016. Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14, 2016 wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.

Michezo mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazocheza Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza na Uganda. Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.

Nusu fainali itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na nne.

Mashindano ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania inatarajiwa kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini moja kwa moja tayari kwa safari ya Uganda.

Imetolewa na TFF

Mkongwe wa Stars azikwa Morogoro

$
0
0

mohammed-msomali

Kocha na mchezaji mahiri wa zamani wa Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mohammed Msomali amezikwa leo Septemba 9, 2016 kwenye makaburi ya Kola yaliopo barabara ya zamani ya Dar es Salaam-Morogoro.

Mbali ya wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) waliohudhuria mazishi hayo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi katika maziko hayo ya Msomali aliyefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 74.

Kocha Mohammed Msomali anaelezwa kuwa ‘gwiji’ la kandanda la Tanzania, alifariki dunia jana Septemba 08, 2016 saa saba mchana akiwa nyumbani kwake akisubiri kupata mlo wa mchana.

Katika nafasi ya kucheza, historia inaonesha kuwa Msomali nyota yake ilianza kuonekana kwenye timu mahiri ya Cosmopolitan ya Dar es Salaam kabla ya kuchezea klabu nyingine za Young Africans pia ya Dar es Salaam, Mseto ya Morogoro, Timu ya Mkoa wa Morogoro ‘Moro Stars’ na Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kadhalika timu ya Bara ambayo ni maarufu kwa jina la Kilimanjaro Stars.

Wakati wa uhai wake, Msomali amepata kuzifundisha Mseto na Tumbaku za Morogoro ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Klabu Bingwa Tanzania) mwaka 1975. Pia alizinoa Young Africans, Timu ya Mkoa wa Morogoro ‘Moro Stars’ na kwa muda mrefu timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ sambamba na ile ya Bara ambayo ni maarufu kwa jina la Kilimanjaro Stars.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Mohammed Msomali mahala pema peponi.

VIDEO- LEWANDOWSKI AFUNGA BAYERN IKISHINDA UGENINI BUNDESLIGA

$
0
0

lewaRobert Lewandowski alifunga goli lake la nne kwenye mechi mbili za Bundesliga na kuisaidia Bayern Munich kushinda ugenini dhidi ya Schalke 04.

Mabingwa hao wa Ujerumani mapema kabisa walionekana kama wamekata tamaa baada ya mshambuliaji wao tegemezi Lewandowski kukosa goli kwenye eneo la sita.

Lakini baadaye aliifuta makosa yake baada ya kufunga goli murua dakika ya 81 kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Javier Martinez na kutoa tena pasi ya goli la pili lililofungwa na Joshua Kimmich.

Mshambuliaji wa Schalke Klaas-Jan Huntelaar alikarabia kufunga lakini mpira wake uligonga mwamba wakati huo timu zote zikiwa hazijafungana.

Mchezaji aliyetokea benchi Kimmich, 21, amefunga leo baada ya kutoka kuifungia timu yake ya Ujerumani kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Norway kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia. Goli lake kwenye mchezo huu ni la kwanza tangu aichezee Bayern.

Kiungo wa Bayern Renato Sanches (19), ambaye aliisaidia Ureno kushinda ubingwa wa Euro Euro 2016, alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi ya Bundesliga baada ya kusajiliwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi akitokea Benfica.

Mpaka sasa Bayern wamefikisha alama sita chini ya meneja wao Carlo Ancelotti kufuatia kushinda michezo yao yote miwili.


Kabla ya Manchester derby, wafahamu wachezaji 7 waliowahi kucheza Man United na Man City

$
0
0

Ni marachache kushuhudia wachezaji kuhamia kwenye klabu hasimu hususan kama timu ni za mji mmoja. Lakini tangu Bob Milarvie alipovichezea vilabu vyote vya Manchester United na Manchester City, wachezaji 24 wameshacheza kwenye vilabu vyote vya jiji la Manchester.

Idadi hiyo ya wachezaji wameiwakilisha Manchester United na Manchester City kwa miaka kadhaa, lakini mchezaji maarufu zaidi ni anabaki kuwa Denis Law.

Billy Meredith, Peter Barnes na Brian Kidd, ni miongoni mwa wachezaji waliozichezea timu zote za Manchester.

7. Peter Beardsley – Mshambuliajicarlos-tevez2

peter-beardsley2

Manchester United: 1982-1983

Mechi: 0 Magoli: 0

Manchester City: 1998 (kwa mkopo kutoka Bolton)

Mechi: 6  Magoli: 0

Peter Beardsley aliitumikia Manchester United msimu wa 1982-83 lakini hakufanikiwa kucheza mechi yoyote ya ligi (wakati huo First Division)

Tangu alipoondoka Old Trafford, nyota huyo wa England alicheza kwenye vilabu vingine sita ikiwa ni pamoja na Liverpool kabla ya kujiunga na Manchester City kwa mkopo akitokea Bolton Wanderers.

6. Carlos Tevez – Mshambuliaji

carlos-tevez2Manchester United: 2007-2009

Mechi: 63  Magoli: 19

Manchester City: 2009-2013

Mechi: 105  Magoli: 57

Carlos Tevez kwa mara ya kwanza alijiunga na Manchester United kwa mkopo akitokea West Ham na akafanikiwa kuonesha uwezo mkubwa, na kujizolea idadi kubwa ya mashabiki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupambana.

Uhamisho wake kutoka United kwenda kwa majirani zao Man City kulifanya awe mchezaji wa kwanza kutoka Old Trafford moja kwa moja tangu Terry Cooke alipofanya hivyo mwaka 1999.

5. Owen Hargreaves – Kiungo

owen-hargreaves2Manchester United: 2007-2011

Mechi: 27  Magoli:2

Manchester City: 2011-2012

Mechi: 1  Magoli: 0

Owbwen Hargreaves ulikuwa ni usajili mkubwa kutoka Bayern Munich na aliisaidia United kutwaa taji la mabingwa Ulaya lakini majeraha yaliharibu maendeleo yake ndani ya Old Trafford.

Baada ya mkataba wake kumalizika alifanya maamuzi magumu ya kujiunga na wakali wa Etihad Stadium lakini alifanikiwa kucheza mchezo mmoja tu wa Premier League kabla ya kustaafu kutokana na sababu za majeruhi.

4. Andy Cole – Mshambuliaji

andy-cole1Manchester United: 1995-2001

Mechi: 195  Magoli: 93

Manchester City: 2005-06

Mechi: 22  Magoli: 9

Andy Cole alikuwa ni mfungaji wa aina yake kwenye kikosi cha United baada tu ya kusajiliwa akitokea Newcastle United mapema mwaka 1995.

Ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi kilichotwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja (Treble), alifunga bao dhidi ya Tottenham na kuisaidia United kutwaa taji huku mshambuliaji huyo mzaliwa wa Nottingham akatimkia Blackburn Rovers na Fulham kabla ya kujiunga na Manchester City mwaka 2005.

3. Terry Cooke – Kiungo

terry-cooke2Manchester United: 1994-1999

Mechi: 4  Magoli: 0

Manchester City: 1999-2002

Mechi: 37  Magoli: 7

Cooke ni zao la timu ya vijana ya Manchester United, mwaka 1995 alifunga mkwaju wa penati ulioipa ubingwa wa FA timu ya vijana. Alicheza mechi nne za Ligi kuu England akiwa kwenye kikosi cha wakubwa.

Cooke was a part of the Old Trafford youth Class of ’92 alongside David Beckham, Paul Scholes, Gary and Phil Neville, Nicky Butt and Ryan Giggs.

Cooke alikuwa ni miongoni mwa vijana waliolelewa Old Trafford miaka ya 1990 na wachezaji kama David Beckham, Paul Scholes, Gary and Phil Neville, Nicky Butt pamoja na Ryan Giggs.

2. Andrei Kanchelskis – Winger

andrei-kanchelskis3Manchester United: 1991-1995

Mechi: 123  Magoli: 28

Manchester City: 2001 (kwa mkopo kutoka Rangers)

Mechi: 10  Magoli: 0

Andrei Kanchelskis alisajiliwa na United akitokea Shakhtar Donetsk na kuisaidia United kutwaa taji la EPL mwaka 2093 na jingine msimu uliofuata.

Mwaka 1995 aliuzwa kwenda Everton lakini muda mfupi baadaye alihamia Fiorentina. Klabu hiyo ya Serie A ilimtoa kwa mkopo kwenda City mwaka 2001 na akacheza mechi 10.

1. Peter Schmeichel – Golikipa

peter-schmeichel2Manchester United: 1991-1999

Mechi: 292  Manchester: 0

Manchester City: 2002/03

Mechi: 29  Magoli: 0

Peter Schmeichel alikuwa nahodha wa United wakati kikosi hicho kikitwaa mataji matatu mwaka 1999 huku akitajwa kuwa golikipa bora katika historia ya klabu hiyo.

Raia huyo wa Denmark alijiunga na Sportinglakini baadaye akarudi kutoka Lisbon na kutua Aston Villa miaka kadhaa baadae.

Chakushangaza, alijiunga na Manchester City na kuendeleza rekodi ya kutofungwa kwenye mchezo wa Manchester derdy.

Wachezaji 10 wanaoongoza kutupia Manchester derby

$
0
0

magoli-man-united-vs-man-city

Pambano la Manchesster derby hatimaye limewadia, leo September 10 Manchester United itakuwa mwenyeji wa majirani zao Manchester City kwenye uwanja wa Old Trafford mechi inayotajwa kuwa ni ya wachezaji wenye gharama zaidi kwenye ulimwengu wa soka.

Habu tuangalie wachezaji 10 wenye historia ya kufunga magoli mengi kwenye historia ya Manchester derby.

10. Dennis Viollet (England) – Manchester United – magoli 7 mechi 15 

dennis-viollet10. Paul Scholes (England) – Manchester United – Magoli 7

paul-scholes9. Joe Spence (England) – Manchester United – Mechi 14, Magoli 8.

joe-spence8. Brian Kidd (England) – Katika mechi zote za Manchester United na Manchester City – mechi 19, magoli 8 

brian-kidd-man-utd-man-city7. Eric Cantona (Ufaransa) – Manchester United – mechi 7, magoli 8

eric-cantona6. Colin Bell (England) – Manchester City – magoli 8

colin-bell5. Sergio Agüero (Argentina) – Manchester City – magoli 8

aguero_3093194b4. Bobby Charlton (England) – Manchester United – magoli 9, mechi 27 

bobby-charlton3. Francis Lee (England) – Manchester City – magoli 10, mechi 19

francis-lee2. Joe Hayes – Manchester City – magoli 10, mechi 17 

English professional footballer and forward with Manchester City FC, Joe Hayes (1936-1999) pictured at Arsenal's Highbury Stadium in London circa 1959. (Photo by Rolls Press/Popperfoto/Getty Images)

1. Wayne Rooney (England) – Manchester United – magoli 11, mechi 24 

17-8-8-4-271-png2-png3-png4-png5

NI KUFA AMA KUPONA MANCHESTER UNITED VS MANCHESTER CITY LEO

$
0
0

1Manchester United na Manchester City leo wana shughuli pevu katika Uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa Ligi Kuu England utakachezwa 8:30 kwa majira ya Afrika Mashariki.

Hii ni vita ya makocha wawili ambao ni mahasimu wa muda mrefu Jose Mourinho na Pep Guardiola, ambapo kwa mara ya kwanza wanakutana katika historia ya soka la England baada ya kuwahi kukutana wakiwa La Liga kwenye vilabu vya Real Madrid na Barcelona.

Kwa upande wa Manchester United, wachezaji wao Luke Shaw na Henrikh Mkhitaryan wamepona majeraha yao, hivyo wanaweza kujumuishwa kwenye mchezo wa leo.

Antonio Valencia pia takuwepo baada ya kutoka kuitumikia timu yake ya taifa na kuondoa hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Manchester City kwa upande wao, mshambulizi wa Sergio Aguero hatakuwepo kutokana na kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu, Bacary Sagna anaweza kuanza baada ya kupona majeraha yake ya maumivu ya misuli ya paja.

Leroy Sane na Ilkay Gundogan wako fiti kabisa tayari kwa mchezo wa leo na wanaweza kupewa nafasi ya kuanza kwa mara ua kwanza kwenye ligi, vivyo hivyo kwa upande wa kipa Claudio Bravo.

Nahodha Vincent Kompany amepona na jana amefanya mazoezi kamili na wenziwe baada ya kukaa muda mrefu akiuguza majeraha ya paja, lakini leo hatakuwepo kwenye kikosi.

Kauli za mameneja wa timu zote mbili

Jose Mourinho juu ya kukosekana kwa mshambulizi wa City Sergio Aguero: “Ni vigumu zaidi kwetu. Inaonekana kutakuwa na hali ngumu kwenye mchezo wa leo, lakini bila ya Aguero ni vigumu zaidi.

“Aguero akiwepo, tunajua namna gani hucheza. Tunakuwa tunafahamu vizuri mfumo wao, namna wanavyocheza na hakuna shaka juu ya hilo.

“Wana options nyingi sana mabazo kwetu ilibidi tufanyie mazoezi sana, twende hatua kwa hatua, kuangalia kila namna ya kukabiliana nao ili kuzuia sintofahamu katika mchezo.”

Pep Guardiola: “Ngoja kwanza nicheze huu mchezo wa derby na baada ya hapo naweza kutoa tathmini ya kuangalia kama kuna ufanano na ila ya Hispania na Ujerumani. Kwa upande wa vyombo vya habari sijaona utofauti na Uhispania.

“Nimeona michezo minne rasmi ambayo United wamecheza na kwenye kila mchezo wamekuwa wakicheza vizuri zaidi. Kama ilivyo kwetu.

“Tuna kazi kubwa ya kuwadhibiti kwenye mipira ya juu, ni warefu kuliko sisi. Ni timu ya kiwango cha juu sana kama ambavyo miaka yote imekuwa.”
Head-to-head

  • City wanaingia uwanjani wakitafuta ushindi wa 50 katika mechi za mashindano kwenye Manchester derby (wameshinda mara 49, droo 51, kufungwa mara 71).
  • Baada ya kupoteza michezo minne mfululilizo ya derby, Manchester United sasa hawajafungwa na City kwenye michezo minne (ushindi mara 2, droo mara 1). walipata clean sheets kwenye michezo yote waliyokutana msimu uliopita.
  • United wamepoteza michezo mitatu kati ya mitano ya lligi dhidi ya Man City kwenye Uwanja wa Old Trafford (wameshinda mara 1, sare 1).
  • Jose Mourinho ameshinda michezo mitatu ya ushindani kati ya 16 aliyokutana na Pep Guardiola (droo 6, amepoteza mara 7), ukiwemo ule wa ligi alioshinda dhidi ya Barca mwaka 2012 akiwa Real Madrid.

YANGA ITAKAYOIVAA MAJIMAJI LEO HII HAPA

$
0
0

1Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC leo wanawakaribisha Majimaji ya Songea, mchezo unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo jioni.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu na Ndanda ya Mtwara, mchezo uliochezwa Jumatano katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, wakati Majimaji hawana kumbukumbu nzuri kutokana na kutofanya vyema katika michezo yao ya awali.

Kuelekea mchezo huu, Yanga wanahitaji matokeo ya ushindi ili kuanza kujiwekea mazingira mazuri mapema ya kutetea taji lao.

Kocha wa Yanga Hans Van der Pluijm ameendelea kumuanzisha langoni kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, kufuatia kipa namba moja wa klabu hiyo Deogratius Munishi ‘Dida’, kurejea siku moja tu kabla ya mchezo huu kutoka Moshi alipokwenda kumzika baba yake aliyefariki hivi karibuni.

Kikosi cha Yanga kipo hivi;

Kikosi kinachoanza: Ally Mustapha ‘Barthez”, Juma Abdul Jaffar Mnyamani, Haji Mwinyi, Andrew Vincent ‘Dante’, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’, Thabani Scara Kamusoko, Simon Happygod Msuva, Deus David Kaseke, Amissi Jocelyn Tambwe, Donald Dombo Ngoma na Obrey Chirwa.

Akiba: Beno Kakolanya,Oscar Fanuel Joshua, Juma Mahadhi, Kelvin Patrick Yondani ‘Cotton’, Matteo Anthony, Yusuph Muhilu na Hassan Ramadhan Kessy.

Maagizo 5 ya Nnauye alipotembelea TFF kwa mara ya kwanza

$
0
0

img_0054September 10 Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye amezitembelea ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwa ni ziara fupi ya kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo utendaji wa shirikisho hilo ambalo linaongoza soka la Bongo.

Katika ziara hiyo, Mh. Nnauye alikutana na Rais wa TFF Jamal Malinzi pamoja na watumishi wengine wa wa TFF, Nnauye ametoa maagizo kadhaa kwa Malinzi kuhakikisha yanatafutiwa ufumbuzi na kutekelezwa.

img_0041

Maagizo aliyoyatoa Waziri Nnauye ni pamoja na;

Ukaguzi wa kina TFF

Nilimwagiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo amtumie mdhibiti na mkaguzi wa mkuu wa serikali afanye ukaguzi wa kina wa rasilimali watu ili tujue ukweli wa mambo ili watanzania waujue halafu ytuondokane na mambo ambayo wakati mwingine hayana msingi.

Kwahiyo utafanyika ukaguzi mkubwa pengine ambao haujawahi kufanyika muda mrefu kuangalia rasilimali fedha na rasilimali watu kuangalia uwezo wa utendaji.

img_0046

Mishahara ya watumishi

Nimekuwa nikitumiwa message nyingi na watumishi wakidai hawajalipwa mishahara.watumishi wadai wanakaa muda mrefu wakati mwingine miezi mitatu minne hawajalipwa mishahara, manung’uniko yamekuwa mengi.

Rushwa kwenye uchaguzi

img_0050

Niliahidi kwamba tutasimamia uchaguzi ndani ya TFF uwe uchaguzi wa haki usiogubikwa na matendo ya rushwa ili tupate viongozi wafasi.

Kupitia kikao hiki, nawaagiza TAKUKURU kote waliko, wahakikishe uchaguzi unakuwa wa haki kwa dhibiti vitendo vya rushwa. Kumekuweko na malalamiko mengi sana, sasa kuanzia mikoani wahakikishe uchaguzi unakwenda kwa haki.

Tukikuta mla rushwa tumkamate bila kujali cheo chake wala anatoka wapi, kusiwepo visingizio.nadhani hapa pakibanwa vizuri tutapata viongozi wasafi ambao wameshinda kwa uwezo wao na si kwa pesa zao.

img_0086

Mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji wa vilabu

Michakato inayoendelea Simba na Yanga na timu nyingine ya kubadilisha mifumo ya uendeshaji. Serikali tunaunga mkono mabadiliko na mijadala. Michakato hii lazima iongozwe isije ikafata shor-tcut, lazima iwe ya uwazi pasiwe na mambo yanayofichwafichwa lazima sheria zifuatwe. Katika hili serikali tutakuwa wakali kwasababu likikosewa litavuruga amani ya nchi.

Thamani ya vilavu hivi inaangaliwa kabla ya mtu hajajipangia bei ya kujinunulia, kujikodishia  au kumiliki? Serikali tuko tayari kushirikiana na vilabu kufanya tathmini ya vilabu kabla ya kufikia hatua ya kumilikishana.

Ni vizuri kujua hadhi ya waliokuwa na vilabu hivi kwa miaka yote, wapo wanachama, mashabiki na wapenzi, hadhi na haki zao katika mchakato huu inaangaliwa vipi?

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>