Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

NBA ALL STAR 2018 YAPANGWA, LIJUE JIJI LITAKALOANDAA.

$
0
0

staples

Hatimaye shirikisho la mpira wa kikapu chini Marekani limetangaza mji utakaokuwa mwenyeji wa mashindano ya nyota wa mpira wa kikapu Marekani maarufu kama NBA ALL STAR GAME, utakaofanyika February 28 2018.

Mchezo huo utafanyika katika ukumbi na uwanja wa STAPLES CENTER ambao ni uwanja wa nyumbani kwa vilabu vya Los Angeles Lakers na pia Los Angeles Clippers. Hii inakuwa mara ya tatu kwa uwanja huo kuandaa mashidano haya ambao watendaji wa ligi na jiji walitangaza alfajiri ya Jumatano ya tarehe 23 kwa saa za Afrika.

Hii inakuwa mara ya sita kwa mchezo huu kuchezwa katika jiji la Los Angeles ikifuatiwa na New York ambayo imeandaa mara 5 huku majiji ya Philadelphia na Boston Celtics yakiwa yameandaa mara 4 kila moja. NBA ALL STAR ya mwaka 2017 itaandaliwa kunako jiji la Charlotte.

Kamishna wa NBA, AdamSilver, rais wa shirika la kimichezo linalomiliki kiwanja cha Staples na mtendaji mkuu Dan Beckerman, Meya wa jiji la Los Angeles Eric Garcetti na Rais wa kamisheni ya michezo na burudani ya Los Angeles Kathy Schloessman walitoa tamko la pamoja muda mfupi kabla ya mchezo kati ya Memphis Grizzlies dhidi ya Los Angeles Lakers.

Staples Center iliandaa mchezo wa NBA All-Star mwaka 2004 na pia 2011. Eneo lao jirani la Inglewood liliandaa All-Star mwaka 1972 na 1983, na uwanja unaokaribia kuvunjwa wa Los Angeles Sports Arena uliandaa mchezo wa 1963.

Katika michezo mitano iliyopita iliyoandaliwa katika jiji la Los Angeles, kanda ya Magharibi imeshinda mara tatu huku wachezaji watatu wa Los Angeles Lakers wakitwaa tuzo ya mchezaji bora mwenye thamani wa mashindano hayo. Wachezaji hao ni  Kobe Bryant, Shaquille O’Neal na Jerry West.

Shaq na Kobe wakionyesha tuzo ya MVP ya All Star
Shaq na Kobe wakionyesha tuzo ya MVP ya All Star
Shaq O'neal na Kobe Bryant wakiwa wote Lakers
Shaq O’neal na Kobe Bryant wakiwa wote Lakers

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>