
Timu ya taifa ya tanzania ‘Taifa Stars’ imeendelea vyema na maandalizi ya kuwania kufuzu kwa michuano ya Afrika AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Chad itakayochezwa March 28 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Taarifa za ukamilifu wa Stars zimetolewa na afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto ambaye pia amesema timu ya Chad inasuasua kuingia nchini huku timu hiyo ikigoma kuzungumzia safari yao licha ya TFF kuiuliza mara kadhaa.

Ili kukiimarisha vyema kikosi cha Stars, kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa amemuongeza mchezaji mwingine wa kimataifa kikosini Adi Yusuf mbaye anayecheza Mansfield Town ya England anayeifanya Stars kuwa na wachezaji watatu wa kimataifa akiungana na Samatta pamoja na Thomas Ulimwengu.

Stars ipo kundi moja na Nigeria, Misri na Chad ambapo jana Nigeria ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Misri na kuifanya Misri kuongoza kundi ikiwa na pointi saba, Nigeria ikifuata ikiwa na pointi tano huku Stars ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi zake nne na Chad ikibuzuza mkia bila ya pointi.
Picha zaidi…



