Umekuwa ukiwaona ndani ya jezi wakiwajibika uwanjani lakini baada ya filimbi ya mwisho wanabalika na kuingia kwenye ulimwengu mwingine wa kawaida kuishi maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya ma-star wa soka wako vizuri hasa linapokuja suala la ‘mitupio’, mtandao wa sokkaa umetoka na story ya wanasoka 10 ambao wanaonekana kufanya vizuri linapokuja kwenye ulimwengu wa mavazi na fashion.
10. Memphis Depay
Mchezaji huyo mpya wa kikosi cha Manchester United si tu kwamba naongeza kasi kwenye kikosi cha ‘Mashetani wekundu’, lakini jamaa huyu anatembea kwa kujiamini linapokuja suala la mavazi.
Amekuwa kivutio kila kona anayokanyaga nje ya uwanja kutokana na aina ya mavazi ambayo kijana huyu ananyuka.
9. Mario Gomez
Inawezekana anaweka akawa amepotea mara baada ya kuihama klabu yake ya zamani Bayern Munich lakini anabaki kwenye akili za watu wengi kutokana na kuwa miongoni wa watupiaji wazuri akitwaa tuzo ya ‘sense of style.’
8. Claudio Marchisio
Claudio Marchisio ni mcheza soka wa kitaliano anayecheza soka safi. Ni mchezaji mwenye aina yake ya uvaaji ambayo inamfanya aonekane ‘bomba’ style yake ya uvaaji inamfanya avutie ndani na nje ya uwanja.
7. Gerrard Pique
Mlinzi wa Barcelona na timu ya taifa Hispania kitu kingine cha ziada mbali na soka, ni namna jamaa anavyoweza kuonekana smart. Aina yake ya uvaaji pamoja na style ya nywele inamfanya Gerrard kuwa kivutio kwa mashabiki wake.
6. Sergio Ramos
Muonekano wake nje ya uwanja unafanana sana na ule wa mchezaji mwenzake wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Sijui nani anayemuiga mwenzake, lakini inawafanya waonekane poa.
5. Daniel Sturridge
Daniel Sturridge ameripotiwa na jarida moja ‘Vice’ kwamba, ni mcheza soka anayependa sana fashion na mavazi yanayokwenda na wakati. Hata katika Instagram yake amekuwa aki-post picha nyingi za fashion.
4. Lionel Messi
Mchezaji bora mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani mara zote ameonekana akisubiri nyuma ya mpinzani wake Cristiano Ronaldo kwenye upande wa mavazi. Hiyo haijalishi sana kwasababu tayari yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaofanya vizuri kwenye nyanja hiyo.
3. Andrea Pirlo
Kiungo huyu mchezeshaji wa New York City FC amekuwa kama wine, anakuwa vizuri kadiri miaka inavyosonga mbele. Kama si uwezo wake mkubwa wa kupiga free kicks na penati basi umaarufu wake angeupata kwenye stage ya fashion. Muonekano wake umekaa kama mcheza movies unawafanya wengi watamani kupiga nae picha.
2. Xabi Alonso
Kiungo huyu wa Hispania si mahiri tu katika kuusoma mchezo haraka, uwezo wake wa kaba wala kupiga pasi zenye macho akiwa kwenye pitch, lakini pia huyu mzee yuko vizuri kwenye fashion.
Mwaka 2010 vyombo vya habari vya Hispania vilimpigia kura kuwa ndiye mcheza mpira anayetupia zaidi duniani. Kipindi cha nyuma alikuwa model wa wa kampuni za mavazi za Polo Ralph Lauren, Prada, IWC Schaffhausen, na Adidas.
1. Cristiano Ronaldo
Hana mpinzani linapokuja suala la kuonekana nadhifu. Anamuonekano, umbo, anajiamini lakini juu ya yote jamaa ni mchangamfu vitu ambavyo vimekuwa vikiwachanganya kinadada wengi mitaani.