Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

YANGA HAIBEBWI, BALI INAJIBEBA YENYEWE NA MBINU ZAKE…

$
0
0

Yanga-ushindi

Na Baraka Mbolembole

YANGA SC inacheza vizuri zaidi ya vile unavyoweza kuandika msimu. Akianza na wachezaji wanne katika safu ya ulinzi ambao hawakutumika katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika siku ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Al Ahly.

Mkufunz mkuu wa Yanga, M-holland, Hans Van der Pluijm aligundua haraka udhaifu wa mlinzi wake wa kati, Pato Ngonyani. Golikipa, Deogratius Munish ‘Dida’ alicheza kwa dakika zisizopungua kumi baada ya kuumia kwa Ally Mustapha ‘Barthez’ katika pambano la Jumamosi iliyopita, alianza katika pambano Jumatano dhidi ya Mwadui FC.

Oscar Joshua alianza katika nafasi ya beki 3 badala ya Mwinyi Hajji aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Pato alicheza na majeruhi wa muda mrefu, nahodha, Nadir Haroub na walinzi hao wa kati walifanya makosa mengi ya kimchezo kwa dakika 45′ walizocheza pamoja kama ‘walinzi-pacha.’

Ni, Juma Abdul pekee ambaye naweza kusema mchezaji wa kikosi cha kwanza aliyeanza katika safu ya ulinzi katika game  dhidi ya Mwadui FC. Hans ilimbidi kuvuruga mipango yake ya ‘sub’ kwa kumpumzisha, Pato mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza na kumpa nafasi, Mtogo, Vicent Bossou.

Kulingana na ratiba jinsi ilivyo, Hans ataendelea kuwapumzisha wachezaji wake wa nafasi muhimu ili kuwapa mapumziko. Katika siku za karibuni ‘ushirikiano’ wa Kelvin Yondan na Bossou umeonekana kucheza vizuri licha ya kwamba wamekuwa pia wakiruhusu goli katika mechi.

Baada ya game dhidi ya Mwadui FC, kikosi cha Hans kitakuwa na mechi nyingine muhimu ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumamosi hii.

Umuhimu wa mechi hiyo unatokana na ukweli kwamba utakuwa mchezo wao wa mwisho wa kiporo na kutopata ushindi kutawafanya walingane pointi na vinara Simba na kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli (ikiwa matokeo yatakuwa sare.)

Hans kama kocha, wachezaji kama timu yenye malengo sawa, Yanga wanahitaji ushindi tu na kwa akili za Mdach huyu na vipaji alivyonavyo katika timu, Yanga watashinda tena dhidi ya Mtibwa. Hata kwa ‘mtazamo wa kubebwa’ ambao tayari umejengeka kwa wapinzani. Baada ya kufungwa goli la mapema dakika ya 3,’

Mwadui walitulia na kucheza vizuri mno katikati ya uwanja hadi kufanikiwa kusawazisha goli hilo dakika kumi baadaye kupitia kwa kiungo-mshambulizi, Kelvin Sabati. Anthony Matogolo, Razaq Khalfan, Jabir Aziz walionekana kumiliki zaidi mpira kuliko viungo, Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko wa timu ya Yanga.

Uwezo wao mdogo kiufundi na mbinu ndogo walizokuwa nazo ulipelekea timu ya Julio kushindwa kufunga magoli zaidi katika kipindi cha kwanza kufuatia uchezaji wa hovyo wa Pato na Nadir ambao walifanya makosa kadhaa ya kimchezo katika mashumbulizi yao yasiyozidi matano katika kipindi cha kwanza.

Walinzi hao wa kati wa Yanga walitengeneza nafasi kadhaa za wazi katika lango lao lakini safu ya mashambulizi ya kikosi cha Julio haikuwapo uwanjani. Mwadui ni kati ya timu zilizofunga magoli machache katika ligi (kabla ya game dhidi ya Yanga) walikuwa wamefunga magoli 22 tu katika michezo 23. Kufunga goli moja dhidi ya Yanga katika uwanja wa Taifa kwao ilikuwa ni mafanikio.

Hans alimpumzisha haraka Pato kwa kuhofia kupoteza mechi-si malengo yake. Kumuingiza Bossou kulisaidia kurudisha utulivu kwa safu yao ya ulinzi. Na timu iliyokuwa ikicheza taratibu na vibaya mno kipindi cha kwanza ilianza kupandisha spidi kadri dakika zilivyokuwa zikisonga mbele.

Kumbuka, Geofrey Mwashuiya aliingia kuchukua nafasi ya Mniger, Issouf Boubacar dakika 46. ‘Hans alitaka timu yake ikapandishe spidi ili kupata matokeo mazuri.  Hadi kufikia dakika ya 57’ wakati Julio alipoamua kufanya ‘sub’ yake ya kwanza, Mwadui walikuwa wakicheza vizuri kwa kupasiana pasi za uhakika katikati ya uwanja.

Kati ya wachezaji waliofanya vizuri katika mchezo huo ni kijana, Kabunda ambaye alimpisha mzoefu, Nizar Khalfan katika eneo la kiungo. Nizar aliingia wakati ambao wachezaji wa Yanga walikuwa na presha ya kupata goli la pili, hivyo walicheza kwa kukimbiza mpira. Kama si ustadi wa golikipa, Shaaban Kado basi Msuva angefunga dakika ya 58.

Dhana ya Yanga kubebwa inatokea wapi? Timu ambayo ilifanya mashambulizi zaidi ya 16 katika kipindi cha kwanza ilikosa makali kwa kuwa wachezaji wake walikuwa wakicheza kwa spidi ya chini.

Kupandisha kasi kwa Yanga kulipelekea mlinzi, Iddy Mobby kumuangusha mshambulizi, Donald Ngoma na hivyo kuadhibiwa kwa kadi ya pili ya manjano na kuondolewa uwanjani. Ilikuwa sawa tu, hata mimi au wewe ungekuwa mwamuzi ulipaswa kumpa kadi ya njano Mobby.

Bila shaka Yanga inabebwa ndiyo maana imekuwa ikishinda baadhi ya mechi baada ya timu pinzani kubaki pungufu uwanjani. Lakini inabebwa zaidi na mbinu za kiuchezaji na akili binafsi za wachezaji wake.

Mfano, Ngoma amekuwa sababu ya baadhi ya wachezaji wa timu pinzani kuondoshwa uwanjani kwa kadi nyekundu msimu huu. Mbinu za Mzimbabwe huyu na akili ya kocha wake katika kumtumia ndiyo sababu kubwa ya Yanga kubebwa katika baadhi ya mechi zilizoonekana ngumu upande wao.

Timu bingwa ni lazima ibebwe ili ipate mafanikio, lakini si kubebwa na ‘mbereko’ ya waamuzi bali na mbinu binafsi za wachezaji na ubora wa benchi la ufundi katika kuusoma mchezo.

Tusidanganyane, Yanga haibebwi na waamuzi, ukweli inajibeba yenyewe na mbinu zake, ufundi na ubora wao. Hata kabla ya timu yake kufungwa jana, Julio alisema katika moja ya kituo cha radio kwamba, anaamini Yanga watashinda VPL hivyo anaomba timu yake ikutane na Azam FC katika nusu fainali ya FA ili awafunge na kukutana na Yanga katika fainali.

Kauli alimaanisha kwamba, Kikosi chake hakina uwezo wa kuitoa Yanga katika michuano ya FA wala kuishinda katika fainali kwa kuwa alisema pia Mwadui FC itapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Shirikisho Afrika wakifungwa fainali.

Julio alisema maneno haya kabla ya kupangwa kwa ratiba ya nusu fainali, pia alikuwa anajua kwamba timu yake ingekuwa na game ya VPL dhidi ya Yanga… Kusema Yanga wanabebwa na wapewe tu kombe lao, Julio amechemka. Yanga inabebwa na mbinu zake si waamuzi.

NB: Kwa ukaribu zaidi unaweza ku-LIKE Page yangu BSports tukajuzana mambo ya mpira kama hapa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>