Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

WAKATI CHELSEA INASULUBIWA NA AGUERO, HAZARD ALIKUWA ‘BUSY’ NA ICE CREAM

$
0
0

Hazard-busy

Eden Hazard amekuwa kwenye kiwango kibovu ndani ya Chelsea tangu kuanza kwa msimu huu, akitoka kuwa mchezaji bora wa EPL msimu uliopita lakini hadi sasa ameshindwa kuonesha makali yake.

Mashabiki wa Chelsea wanasababu lukuki za kumchukia Hazard msimu huu ikiwa ni pamoja na kutojituma uwanjani ambayo imepelekea kushindwa kuisadia timu yake uwanjani. Mpaka sasa ndiye mchezaji mwenye kiwango kibovu kati ya wachezaji wa Chelsea kwenye msimu huu.

Kwa sasa Hazard yuko nje ya kikosi kutokana na majeruhi, lakini wakati wa mchezo wa ligi kuu ya England siku ya Jumamosi kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City, nyota huyo wa timu ya taifa ya Ubeligiji alikuwa jukwaani akishuhudia pambano hilo pamoja na familia yake.

Camera za TV zilimnasa Hazard akigonga ice cream ambayo alikuwa akilishwa na mwanaye mdogo.

Kitendo hicho kimepelekea mashabiki wa Chelsea kumpiga madongo mchezaji huyo kupitia mitandao ya kijamii.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>