Mchezaji wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka Jamie Carragher amemponda mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa kwa vitendo vyake vya ukorofi na utovu wa nidhamu awapo uwanjani.
Ni ghari au mkorofi? Ni swali ambalo makocha watajiuliza juu ya wachezaji wanaowapa usumbufu. Kuna watu kama Eric Cantona na Luis Suarez ambao unaweza ukawaweka kwenye kundi hili lakini wao wamezisaidia sana timu zao.
Wawili hao wao binafsi wamekuwa wakizisaidia timu zao kushinda uwanjani na kutoa mchango mkubwa kwa Sir Alex Ferguson na Brendan Rodgers walikubali baadhi ya mapungufu yao.
Sasa una mtu kama Diego Costa. Tabia alioionesha dhidi Arsenal siku kadhaa ilizopita zilimfanya yeye na Jose Mourinho kuwa kwenye headlines kibao.
Binafsi, nadhani itafikia wakati hatakuwa wathamani bali mkorofi. Alimkanyaga Amre Can, majeruhi aliyopata msimu uliopita na tukio la Gabriel unaweza kuona anaingia kwenye matatizo kila wiki.
Hivi ndivyo navyomuona Costa: ni mshambuliaji wa kati wa moja kati ya timu bora Ulaya na anaweza kupata nafasi ya kufunga magoli. Kufunga magoli 20 kwenye mechi 37 ndani ya miezi 12 baada ya kujiunga na Chelsea akitokea Atletico Madrid kilikuwa ni kitu kizuri. Lakini si mshambuliaji mwenye kasi anaeweza kukimbia na hawezi kupiga vyenga.
Kitu ambacho kinanipa wakati mgumu kuhusu Costa ni kwanini anaonekana anapenda kupigana na kila beki ambaye anakutana nae badala ya kufunga magoli.
Jose Mourinho anasema Costa ni bora, naelewa hilo wakati wengine wanasema alikuwa sahihi juu ya vitendo alivyofanya kwa Gabriel, lakini ni kweli alikuwa sahihi? Ni kwemli aliisaidia Chelsea kupata ushindi mnono lakini angalia katika picha kubwa. Kufungiwa kwake mechi tatu na kuchunguzwa kunafaida gani kwake na klabu yake?
Nafahamu kucheza na mtu wa aina yake. Suarez hakuhitaji kuambiwa kwamba amefanya kitu ambacho si cha kupendeza lakini unatakiwa kukubaliana nae kwasababu unatambua kitu atakachokifanya kwenye mechi.
Suarez alikuwa ni sababu kubwa ya Liverpool kuukaribia ubingwa wa ligi miaka mwili iliyopita, uwezo wake kwenye msimu ule ulifanana na Cantona kwa kiasi kikubwa hasa pale aliporejea akitoka kwenye adhabu ya kufungiwa na FA kwa miezi nane msimu wa 1995-96.
Huwezi kusema Costa huyu ni sawa na yule wa msimu uliopita. Eden Hazard, Fabregas na Nemanja Matic walichangia kwa kiasi kikubwa magoli yake msimu uliopita na yalikuwa ni muhimu.