Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

OKC bila Durant yaanza vyema, Westbrook hatari

$
0
0

2_westbrook_76ers_jdg_161026

Wengi walikuwa wanasubiri kuitizama kabu ya Oklahoma City Thunder itacheza vipi msimu ila ya kuwa na mchezaji wake bora wa kipindi kirefu, Kevin Durant aliyetimkia kunako klabu ya Golden State Warriors huku mahusiano yake na mchezaji wao nyota kwa sasa Russell Westbrook yakiingia dosari.

Tofauti na Durant, Westbrook ameanza vyema michuano ya mwaka huu baada ya kuiongoza OKC kuishinda Philadelphia 76ers kwa pointi 103-97. Westbrook alifunga pointi 32 na kudaka rebound 12.

Klabu ya Philadelphia ililazimika kumtoa uwanjani shabiki mmoja aliyekuwa amevaa jezi ya Allen Iverson baada ya kumpigia kelele kwa dharau na kumuonyesha ishara ya vidole viwili vya kati mchezaji Russell Westbrook, hali ambayo haivumiliki kwenye NBA.

“Usiku wa ajabu sio?” alisema Westbrook. “ilibidi nishuke tu maana msimu uliopita ilinisababisha kulipa kiasi cha $25,000. Nahisi shabiki atakuwa anaendelea vyema tu, wanaweza kusema na kufanya chochote wanachojisikia.” Westbrook alipigwa faini msimu uliopita kutokana na matumizi ya lugha isiyofaa kweye michezo ya mtoano msimu uliopita.

Mchezaji aliyesubiriwa kwa muda mrefu na klabu hiyo kucheza mchezo wake wa kwanza, Joel Embiid alifunga pointi 20 katika dakika 22 alizocheza ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu Sixers wamchague katika namba  3 kwenye uchaguzi wa wachezaji wa mwaka 2014. Embiid alikaa nje kwa misimu miwili kutokana na majeraha ya mguu na mashabiki walimshangilia kila alipotupa mtupo na hata wakati anatambulishwa uwanja ulizizima.

Mashabiki waliimba “Trust The Process” ikiwa na maana kuwa na imani na utaratibu wa utendaji kitu kila ambapo  Embiid alikuwa akienda kurusha mitupo huru.

HIGHLIGHTS


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>