Ureno kutwaa kombe la Euro mwaka 2016 iliwashangaza wengi.
Timu hii haikupata ushindi hata kwenye mechi moja katika hatua ya makundi, kitu ambacho kingewafanya utupwa nje ya mashindano kwenye fainali zilizopita.
Lakini walipambana hatimaye wakafanikiwa kufika hatua ya fainali na kuwashinda wenyeji wa mashindano timu ya taifa ya Ufaransa.
Ronaldo kwa upande wake amekuwa na historia ya aina yake kwenye michuano ya Euro.
Alizomewa baada ya mchezo dhidi ya Iceland, akakosa penati dhidi ya Austria, akafunga magoli mawili dhidi ya Hungary, akatupia goli la kichwa kwenye nusu fainali zikiwa dakika za maumivu, mashindano hayo yalikuwa kama movie kwake.
“Sasa tumekamilisha kazi”, ni hotuba aliyoitoa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na ilikuwa siri kwa kipindi chote hicho.