Stephen Curry alifunga pointi 41 katika robo tatu , huku akiiongoza Warriors kupata mitupo 22 ya point 3 katika majaribio 38 na wakifunga pointi nyingi zaidi kwao kwa msimu huu. Klabu ya Warriors iliibuka na ushindi wa 135-116 na kupeleka kilio kwa Phoenix Suns siku ya Ijumaa usiku.
Golden State Warriors walikosa mtupo mmoja tu wa pointi 3, kuweza kufikia rekodi iliyowekwa na Orlando Magic, March 9, 2009. Lakini walifikia rekodi ya Houston Rockets ya Feb 3, 2013 waliyoweka dhidi ya wao Warriors.
“Kwa sasa tunayo makali ,” alisema Curry, ambaye anajaribu kutetea tuzo yake ya NBA MVP aliyoshinda msimu uliopita . “Tunapenda sana suala la muda wote kuwa na hisia ya kushinda , na ujasiri wetu waa khali ya juu hivi sasa. Hilo ni jambo kubwa kwetu na ndilo linalotusukuma.”
Draymond Green alifunga pointi 14, akadaka rebound 10 na kutoa pasi 10. Hii inakuwa triple double yake ya tatu huku mbili zikiwa zimekuja msimu huu. Leandro Barbosa alifunga pointi 21 akipata mitupo 8 kati ya tisa huku akifunga mitupo yote 5 ya pointi 3.
T.J. Warren alifunga pointi 28 ambazo ni nyingi zaidi katika maisha yake ya kikapu akiifungia Suns. Phoenix suns wamepoteza michezo mitatu mfululizo, huku ikiwa ni minne kati ya mitano.
Brandon Knight na Eric Bledsoe aliongeza pointi 21 kila moja kwa Phoenix. Klay Thompson alifunga 15 kwa Warriors.
CURRY AWEKA REKODI DHIDI YA LEBRON
Stephen Curry sasa amempita Lebron James katika watu waliopata mitupo mingi zaidi ya pointi tatu. Amepanda mpaka nafasi ya 35, akifunga pointi 3 1278 dhidi ya 1276 za James. Lebron katumia mechi 927 wakati Curry kazipata ndani ya michezo 433 tu.
HIGHLIGHTS