Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

HAWA NDIYO WANAUME 9 WALIOPIGA HAT-TRICK NDANI YA EPL HADI SASA, WA-AFRIKA WAWILI NDANI

$
0
0

hat 9

Mwezi November ulikuwa ni mgumu kwa timu nyingi za EPL. Hat-trick moja tu ulifungwa ndani ya mwezi huo na hiyo inaashiria ni kwa kiasi gani timu zilipambana kusaka goli. Lakini mshambuliaji wa Everton Arouna Kone ndiye mchezaji pekee aliyefunga hat-trick ndani ya mwezi huo.

Hii ni orodha ya wachezaji tisa ambao wamefanikiwa kufunga hat-trick ndani ya EPL msimu huu hadi sasa huku orodha hiyo ikijumuisha wachezaji wawili kuoka bara la Afrika.

9. Callum Wilson-Bournemouth

hat

Ilikuwa ni August 22, 2015 mechi kati ya West Ham dhidi ya Bournemouth. Cullum Wilson aliweza kufunga hat-trick yake, alifunga goli mbili kwenye kipindi cha kwanza (dakika ya 11 na 28) kisha akaikamilisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 79 na kuipa ushindi timu yake ushindi wa magoli 4-3.

8. Steven Naismith-Everton

hat 1

September 12, 2015 Everton ilicheza dhidi ya Chelsea, siku hii ilikuwa ni nzuri kwa Steven Naismith baada ya kufanikiwa kurudi kambani mara tatu dakika ya 17, 22 na 82 na kuikata maini Chelsea kwa Everton kushinda mchezo huo kwa magoli 3-1 huku Chelsea ikirejea London bila ya pointi.

7. Alexis Sanchez-Arsenal

hat 2

Ilikua ni September 12, 2015 mchezo kati ya Leicester City dhidi ya Arsenal. Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Chile hakutambua ubora walionao Leicester msimu huu pale alipotumbukiza goli tatu kutoka mguuni mwake. Magoli ya Sanchezi yalifungwa dakika ya 33, 57 na 81, The Gunners wakapata ushindi wa bao 5-2 kwenye mchezo ambao walifanikiwa kuvuna ushindi kwa magoli mengi hadi sasa tangu kuanza kwa msimu huu.

6. Sergio Aguero-Manchester City

MANCHESTER, ENGLAND - AUGUST 16:  Sergio Aguero of Manchester City celebrates scoring the opening goal during the Barclays Premier League match between Manchester City and Chelsea at the Etihad Stadium on August 16, 2015 in Manchester, England.  (Photo by Alex Livesey/Getty Images)

Ilikua ni mechi kati ya Manchester City dhidi ya Newcastle United iliyopigwa October 3, 2015. Aguero alikamilisha hat-trick ndani ya dakika 50 za mchezo, alianza kufunga dakika ya 42, 49 na 50. Hakuishia hapo aliongeza bao nyingine mbili dakika ya 60 na 62 na kumaliza kazi ya kukivuruga kikosi cha Steve Mc Laren. Vijana wa Pllegrini wakaibuka na ushindi wa goli 6-1.

5. Raheem Sterling-Manchester City

hat 4

Siku hii inawezekana ndiyo ikawa siku nzuri kwake katika maisha yake ya soka hadi sasa. October 17, 2015 kwenye mechi kati ya Manchester City dhidi ya Bournemouth star huyo wa zamani wa Liverpool alipachika bao tatu akianza dakika ya 7, 29 na 43 na kuipa timu yake pointi zote tatu kwa ushindi wa magoli 5-1 ilioupata dhidi ya vijana waliopanda ligi msimu huu.

4. Georginio Wijnaldum-Newcastle United

hat 5

Ilikua ni tarehe 18, October 2015 siku ambayo ilikuwa ni njema kwa mashabiki wa Newcastle United msimu huu. Mshambuliaji wao Georginio Wijnaldum akatuma salamu za kuwashtua wengi kwenye ligi ya England baada ya kupiga hat-trick wakati timu yake ikipambana na Norwich City. Maoli yake yalikuja dakika ya 14, 26 na 66 huku akiongeza jingine moja dakika ya 85 wakati Newcastle ilipoibuka na ushindi wa magoli 6-2.

3. Harry Kane-Tottenham Hotspur

hat 6

Lilikua ni jibu tosha kwa walionza kuhoji uwezo wake wakisema alikua ni mchezaji aliyefanya vizuri kwenye msimu mmoja tu lakini star huyo wa England si lolote si chochote. October 25, 2015 ilikua niku ambayo Kane aliwafunga midomo wale wote waliombeza baada ya Kane kufunga hat-trick dhidi ya Bournemouth. Kane alianza kufunga kuanzia dakika ya 9, 56 na 63 na mechi hiyo kumalizika kwa Spurs kuibuka na ushindi wa magoli 5-1.

2. Arouna Kone-Everton

hat 7

November 1, 2015 striker wa Everton Arouna Kone aliwakumbusha mashabiki ni jinsi gani yuko vizuri kufuatia kupiga hat-trick kwenye mchezo kati ya Everton dhidi ya Sunderland. Kone alipiga goli hizo wakati Everton ikiipa kisago Sunderland cha goli 6-2 kwenye dimba la Goodson Park, Kone alianza fujo dakika ya 31, 62 na kuhitimisha dakika ya 76.

1. Riyad Mahrez-Leicester City

hat 8

Wakati kila mtu akidhani huenda vinara hao wa EPL wangedondosha pointi, Riyad Mahrez alisimama kidete na kutimiza malengo ya Claudio Ranielri kukaa kileleni mwa Premier League kwa mara ya pili msimu huu . magoli mawili ya mapema dakika ya 5 na 22 yakaongeza presha zaidi kwa kocha wa Swansea Garry Monk Jumamosi iliyopita December 5, 2015.

Jamie Vardy hakuhitaji kufunga ilikuwa ni siku ya Mahrez kwani alikamilisha hat trick yake dakika ya 67, Leicester City ikashinda kwa bao 3-0 wakati huo ikiwa imetoka kuibana Manchester United kwa sare ya kufungana goli 1-1.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>