Manchester United ipo kwenye anguko, staili ya soka lao haivutii na pia timu haipati matokeo mazuri pamoja na uwezekazeji mkubwa uliofanyika.
Takwimu zilizotolewa leo zinaonyesha hakuna timu yoyote ya Kiingereza katika madaraja manne ya juu kabisa ya nchi hiyoambayo imezidiwa kupiga mashuti langoni mwa adui katika viwanja vyao nyumbani na Manchester United msimu huu.
Vijana wa Louis van Gaal mpaka sasa wamefanikiwa kupiga mashuti 35, wastani wa mashuti 3 kwa kila mechi wanayocheza Old Trafford – japo katika mchezo wa juzi vs Southampton walifanikiwa kupiga shuti moja tu.
Idadi ya mashabiki wanaoingia Old Trafford kwa mechi ni watu 75,330 kwa kila mechi msimu huu – watu 15,000 zaidi ya idadi wanayopata vilabu vingine 92 vya ligi za juu England – Idadi ya watazamaji wa United inawazidi mara 73,832 ile wanayopata Accrington – timu ambayo inashiriki ligi ya daraja la pili – ambao uwanja wao wa nyumbani huingiza watu 1,498.

Hata hivyo Accrington imekuwa ikiwaburudisha sana washabiki wake wachache kwa kushambulia zaidi wapinzani wakiwa wamepiga mashuti 64 msimu huu – mara 29 zaidi ya Manchester United.
Kwa upande wa Premier League, vijana wa Maurico Pochettino Tottenham wana wastani wa kupiga mashuti 7 kwa mchezo wa nyumbani, zaidi ya mara mbili ya idadi ya wanayojaribu United.
Viongozi wa League One Coventry City — ambao hawakuwa hata na uwanja miaka miaka miwili – wakiwa chini ya boss Tony Mowbray wamefanikiwa kupiga mashuti 93 yaliyolenga goli.