Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Kauli ya Yanga kuhusu kuondoka kwa Vicent Bosou

$
0
0

dsc_0013

Klabu ya Yanga imethibitisha kwamba mlinzi wao wa kati Vicent Bosou yupo nchini Vietnam ambako ameenda kuiangalia familia yake na si kama inavyoelezwa kwamba beki huyo wa Togo amepata timu huko.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedith amesema, Bosou aliomba ruhusa kwenda Vietnam kuiangalia familia yake na klabu ya Yanga haijapata taarifa yoyote rasmi kutoka kwa klabu ya Vietnam kama inavyoelezwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.

“Bosou aliomba ruhusa kwamba anarudi mwanzoni mwa Disemba, tarehe 4 atakuwepo hapa. Bosou wakati anasajiliwa na Yanga alitokea Vietnam na familia yake aliiacha kule, alipoondoka hapa wakati wa mapumziko alikuwa na majukumu ya kitaifa aliporudi hapa akaomba ruhusa akaione familia yake,” hayo ni maneno ya Baraka Deusdedith wakati akikanusha kuhusu Bosou kupata timu nchini Vietnam.

“Tunaona taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Bosou amepata timu lakini sisi kama klabu hatuna taarifa rasmi kutoka klabu yoyote kutoka Vietnam inayomtaka Bosou.”

Taarifa zimekuwa zikienea kwa kasi kwamba beki huyo raia wa Togo amepata timu nchini Vietnam ambako kwa sasa anafanya majaribio na huenda akarejea nchini mwanzo mwa Disemba akiacha vilabu vimalizane, endapo vitafikia makubaliano huenda Bosou akaachana na Yanga.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles