Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

KUELEKEA VPL 2015/16: SABABU ZA KUONDOA TIMU 24, KUTOKA 12 HADI 16 NDANI YA MIAKA 15…

$
0
0

YANGA BINGWA

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam  

Timu 16 baada ya miaka 10. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 ligi kuu bara ilikuwa na jumla ya timu shiriki 24. Timu hizo ziligawanywa katika makundi mawili kisha timu nne bora katika kila kundi zilicheza ‘ligi kuu ya 8 bora’ ili kupata bingwa. Mara ya mwisho ligi hiyo kuchezwa kwa mtindo huo wa makundi ni mwaka 2002, Yanga SC ya Dar es Salaam ndiyo ilitwaa taji hilo.

Mwaka 2003 timu mbili zilipungua na kufikia msimu wa mwaka 2005 ligi kuu ya Tanzania bara ilikuwa na timu 16. Timu mbili zikapungua katika ligi ya 2006 na kufikia msimu wa 2007/08 ni timu 12 tu zilikuwa katika ligi kuu.  

Kupunguzwa timu 12 ndani ya miaka 6 kulitokana na hali ya ukata. Timu kama Majimaji ya Songea, Milambo FC ya Tabora, AFC Arusha, CDA na Mji Mpwapwa za Dodoma, Toto Africans ya Mwanza, Lipuli na Nazarethi za Iringa, Bandari FC ya Mtwara, Kariakoo FC ya Lindi zilishindwa kuzunguka mikoani kucheza baadhi ya michezo ya ligi kuu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kipesa na ligi haikuwa na udhamini wa kukidhi mahitaji yote muhimu ya timu 24, 20, 16 na 14.

Ligi ilichezwa na timu 12 kuanzia msimu wa 2007/08 hadi msimu wa 2010/11 zipoongezwa na kufikia timu 14. Kuanzia msimu huu timu mbili zimeongezeka sasa ligi itakuwa na timu 16. Klabu nyingi ndogo zimeendelea kupata udhamini/ufadhili.

 Mbeya City FC ni timu ya Manispaa ya jiji la Mbeya haina ukata, inajiendesha kibiashara pia itaendelea kunufaika na udhamini mkubwa kutoka kwa Binslum. Stand United itakuwa ikicheza msimu wake wa pili katika ligi kuu. Ikiwa imeanzishwa mwaka 2012 timu hiyo ya mkoani Shinyanga imeingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya bilioni 2 za kitanzania na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA.

Majimaji imepata usafiri binafsi kutoka Mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Songea Mjini, Mheshimiwa, John Nchimbi. Hawatakuwa na ukata kama ilivyozoeleka. Msimu wao wa mwisho katika ligi kuu ( 2010/11) uliambatana na matatizo ya ukosefu wa pesa, sijui watamaliza vipi msimu huu.

Msimu wa mwisho wa Toto Aficans katika ligi kuu uliambatana na ‘tishio’ la timu hiyo kongwe kujitoa katika ligi kuu. Ratiba iliwanyima uhuru, iliwagharimu kiasi kikubwa cha pesa hivyo wakajikuta katika ‘ukata mkali’ msimu wa 2012/13. Wamerejea ligi kuu na tayari kuna dalili za kuendelea kwa mambo yale yale yaliyowashusha daraja.

Africans Sport watacheza ligi kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Coastal Union hazina matatizo ya usajili lakini zitapaswa kuepuka matatizo yao sugu, ucheleweshwaji wa posho, mishahara ya wachezaji na ‘kukamia gemu nne’ tu za msimu (dhidi ya Simba na Yanga) na kuwekeza mawazo katika mechi zote 30 za msimu.

Mwadui FC ni ‘ingizo’ jipya kabisa katika ligi kuu Tazania Bara, baada ya Mgambo JKT kupanda ligi kuu kwa mara ya kwanza mwaka 2012, Mbeya City FC mwaka 2013, Stand United na Ndanda FC ya Mtwara mwaka 2014, klabu hizo hazijateremka daraja. Je, itakuwa hivyo kwa Mwadui FC?. Ni timu ya ‘mgodi wa uchimbaji wa madini’ pale Kahama, haitakuwa na shida, njaa wala matatizo ya usafiri.

Ndanda walipigwa sana ‘tafu’ na udhamini wa Binslum msimu uliopita, walipata pesa za Vodacom na AzamTV lakini bado iliyumbishwa na matatizo ya kipesa. ‘Watasafa’ vipi bila Binslum?

Timu tatu tu za Jeshi zitacheza ligi kuu msimu huu, JKT Ruvu ambayo haijawahi kuteremka tangu mwaka 2002 ilipopanda daraja, Tanzania Prisons ya Mbeya yenyewe imeshuka mara moja tu katika kipindi cha miaka 15 sasa, timu ya tatu ni JKT Mgambo ya Tanga ambayo itakuwa ikicheza msimu wake wa nne mfululizo. Timu hizi tatu hazitakuwa na matatizo ya kambi ama usafiri kwa kuwa zinamilikiwa na idara za kijeshi.

Yanga SC, Simba SC, Azam FC klabu hizi tatu za Dar es Salaam zitaendelea kupeta katika suala la kipato, zimekamilika katika udhamini, hazitegemei pesa za wadhamini wakuu wa ligi tu, Vodacom Tanzania au AzamTv. Yanga, Simba, Azam FC, Coastal, City, Stand, Mwadui FC zikicheza mpira uwanjani zitasumbua. Mtibwa, Kagera, Coastal, zinaweza kufanya maajabu.

Majimaji, Prisons, JKT Ruvu, Mgambo zinauwezo wa kuzunguka nchi, wasiwasi ni Toto Africans, Ndanda FC na African Sports kama tu zitategemea pesa za wadhamini wa ligi pekee. Tutaraji ligi isiyo na ‘ukata’. 

0714 08 43 08


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>