Wakati fulani msimu uliopita katika tukio la hisani, Kocha wa Manchester United Louis van Gaal alipewa listi ya wachezaji ambao kijana mmoja shabiki wa United alitaka wasajiliwe katika dirisha la usajili lilopita. Van Gaal alitabasamu na kupokea karatasi hiyo. Kuna tofauti kati ya wachezaji ambao ni wazuri na wachezaji ambao unaweza kuwapata kwa bei yenye kueleweka. Ni ngumu kuamini kwenye listi ya yule mtoto jina la mchezaji kipenzi cha Old Trafford Cristiano Ronaldo – halikuwemo.
Ronaldo amekuwa kwenye mawazo ya kila shabiki wa United tangu siku alipoondoka kujiunga na Madrid. Na sasa mambo yakiwa yameanza kubadilika ndani ya Santiago Bernabeu, inataarifiwa kwamba Ronaldo anaweza kuwa njiani kurejea Old Trafford kwa mara nyingine tena. Kocha Van Gaal nae ameonekana kulikuza jambo hilo wakati alipoulizwa juu ya mreno huyo wikiendi iliyopita.
Angewezaje kuacha kulikuza jambo hilo? Kwa kocha wa Man United kulikataa wazo la Ronaldo kurejea nyumbani, ni kosa la jinao mbele ya mashabiki wa klabu hiyo. Inawezekana akawa na mapungufu mengi katika utawala wake lakini Van Gaal sio mpumbavu wa kupinga ujio wa Ronaldo hadharani.
Lakini kurudi kwa Ronaldo Old Trafford kunaweza kuwa sio sahihi kwa pande zote mbili.
Kwa kuanzia, Raisi yoyote anayetaka kumuuza Ronaldo inabidi ajihakikishie anafanya biashara ya kueleweka upande wake. Ikumbukwe hii ni biashara ambayo itakuwa inamhusisha mchezaji ambaye atakuwa na umri wa miaka 31 mwakani mwezi wa Pili, dili la aina hii likiwa zuri ni ngumu kulikataa. Kiasi cha £60million kimetajwa na kinaonekana kuwa sahihi, ukizingatia dili itahusisha muda wa miaka mitatu au minne. United wana fedha za kutosha, lakini je watataka kufanya biashara hii? Watu matajiri hawanaga utaratibu wa kununua bidhaa ambayo itakuwa haina faida kubwa ya kuuza baadae, hata kama kurudi kwa Ronaldo kutamaanisha labda kushinda ubingwa wa ligi.
Then kuna upande wa pili wa Ronaldo katika usajili huu. Anasema kila mara kwamba anaipenda United, klabu yenyewe na mashabiki wake, lakini tunafahamu kwamba sababu ya kweli ya mapenzi haya: Ni Sir Alex Ferguson, baba yake kwenye soka.
Ronaldo hatorejea na kumkuta Ferguson Carrington.
Atarudi na kumkuta Louis Van Gaal, meneja ambayo staili ni tofauti kabisa na Iliyokuwepo wakati Ronaldo alipokuwa OT. Chini ya Van Gaal, United hawana mfumo mzuri wa uchezaji, na wachezaji nao inabidi wafuate maelekezo ya mwalimu wao. Ukiangalia kwamba moja ya sababu zinazotajwa kuwa sababu ya kumfanya Ronaldo atake kuondoka ni mfumo wa kocha Rafael Benitez, sasa atakuwaje na furaha Old Trafford ambako hakueleweki zaidi ya Santiago Bernabeu ya Benitez?
Inaonekana ni jambo lisiloingia akilini kuzungumzia kurudi kwa Ronaldo kunaweza kusiwe uamuzi sahihi. Ikiwa Ronaldo atafunga magoli japo nusu ya anayoyafunga akiwa na Madrid, United watashinda ubingwa wa EPL, lakini ‘timing’ ni kila kitu katika soko la usajili. Ukiangalia masuala ya kiuchumi, na vitu vingine vyote – suala la kurudi kwa kipenzi cha OT linaweza kuwa sawa lakini ni kamari kubwa – na safari hii siamini kama italipa kwa pande zote mbili.