Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

“Fei Toto ni mchango wangu Yanga”-Mwigulu Nchemba

$
0
0

Katika story za hapa na pale na mdau wa Yanga lakini pia ni mlezi wa Singida United Dr. Mwigulu Nchemba nikamuuliza kama amewahi kuichangia Yanga kwa chochote kwa sababu mara kadhaa klabu hiyo imeomba kuchangiwa na wanachama na mashabiki wake.

Dr. Nchemba akasema usajili wa Fei Toto kutoka JKU kwenda Yanga aliufanya yeye ikiwa ni sehemu ya kuichangia Yanga na inaelezwa usajili huo uligharimu zaidi ya Tsh. 20 milioni.

“Fei Toto hakuwahi kuwa mchezaji wa Singida United, nilimsajili maalum kama mchango wangu Yanga”-Dr. Mwigulu Nchemba.

Full video tayari ipo #YouTube kupitia channel yangu #DaudaTV lakini pia subscribe channel yangu uwe wa kwanza kupata stories zote nazozi-post.


Andrew Robertson ana mioyo miwili akiwa Uwanjani

$
0
0

Robertson ni silaha ya Liverpool yenye mioyo miwili. Moyo wa kwanza unatumika kipindi cha kwanza, na moyo mwingine unatumika kipindi cha pili. Ule upande ambao anacheza Mane na Robertson, bila shaka ni upande ambao kocha Jurgen Klopp anautegemea sana.

Umewahi kuona ule upande unavujisha magoli ya kizembe? Umewahi kuona mapungufu yanaonekana dhahiri upande ule? Jibu ni hapana. Ule upande ni imara sana kwa sababu Sadio Mane hamchoshi Robertson, na Robertson hamchoshi Mane.

Wakati Liverpool hawana mpira, Unamuona Mane anaongeza mchango wa ulinzi pia hata Robertson anamsaidia Mane kushambulia. Robertson sio beki tu ila hata kushambulia yumo. Kasi yake anayoanza nayo kipindi cha kwanza huwa ni ileile anayorudi nayo kipindi cha pili. Hachoshi kumtazama, anatoa kila kitu alichonacho kwaajili ya timu. Ni moja kati ya wachezaji ambao hawakuangushi uwanjani.


Penati aliyofunga Mohamed Salah, inamaanisha kwamba timu hizi mbili za Arsenal na Liverpool, zimefungana idadi ya magoli mengi zaidi (154) kwenye historia ya mashindano.


Ndio maana ameshahusika kwenye kutengeneza nafasi kumi za kufunga magoli. Anajua kuisukuma Liverpool pale inapotakiwa kufika. Anacheza kwa hisia, haogopi hata kidogo. Naamini unaweza kuona utafauti wa upande wa anaocheza Salah na Trent- Aleksandar Anold na upande wa kulia anaocheza Robertson pamoja na Sadio Mane.

Wanapocheza akina Robertson Mane, inaonekana pana udhabiti wa hali ya juu kwasababu wote wanazuia na kushambulia kwa pamoja. Robertson sio sawa na jiko la gesi ambalo linahitaji uwe unapunguza moto na kuongeza. Ukiwasha umewasha, hakuna hofu unayokutana nayo kwa muda wote wa dakika tisini za mchezo

Bado ana miaka 24, maana yake bado damu ni changa. Ana sifa kuiongoza timu uwanjani, ndomaana amepewa kitambaa cha unahodha kule kwenye Taifa lake la Scotland. Nategemea kumuona siku moja akipewa majukumu ya kuiongoza Liverpool akiwa nahodha. Wachezaji wanaojitoa asilimia mia moja, wanafaa kuwa viongozi sababu wanakuwa na uchungu na timu.


Roberto Firmino mpaka sasa ameifunga Arsenal magoli 7 na kutoa assist 3, jumla magoli (10)

Kichaa Biesla anatisha kama ukoma

$
0
0

Jina la Leeds United sio geni sana miongoni kwa wafuatiliaji wa soka la nchini Uingereza, ni timu iliyokuwa na mafanikio makubwa mwanzoni kwa miaka ya 2000. Mafanikio yao kwa kiasi kikubwa yalichagizwa na ubora wa wachezaji walikuwa nao pamoja na muunganiko mzuri (mbinu).

Wachezaji kama Rio Ferdinand, Jonathan Woodgate, Lucas Radebe, Robbie Keane, Mark Viduka, Harry Kewell na Alan Smith walipata kuunganishwa vizuri na kocha David O’Leary na kufanya Leeds kucheza soka la kuvutia na kufika Hadi hatua ya Nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo hatimaye walitolewa na Valencia iliyokuwa katika kiwango bora wakati huo.

Miaka michache baadae Leeds ilipata changamoto za kiuchumi na kiutawala na kusababisha kuuzwa kwa wachezaji wengi bora na kisha timu ikashuka daraja na yangu hapo haijafanikiwa kupata tena. Na zaidi hakukuwa na dalili za kupanda daraja mpaka mwezi Juni mwaka 2018. Leeds walionekana kuwa makini zaidi na swala hilo kwani walimleta kocha Marcelo Biesla ambaye ni moja kati ya makocha wenye uwezo mkubwa wa kufundisha soka.

Mbinu zake za kushambulia kwa kasi bila woga zimempatia jina la “IL LOCCO” ikiwa na maana ya kichaa. Na hawakukosea sana kwani Biesla ni kichaa wa mbinu na ubinifu. Makocha kama Pep Guardiola, Diego Simeone na Maurizio Pochetino wamekiri katika nyakati tofauti kuwa wanamkubali Biesla na kuiga mbinu zake.

Guardiola alishawahi kusema kuwa “Biesla ndie KOCHA bora zaidi duniani” wakati huo Biesla akifundisha Athletic Bilbao ya kina Ander Herrera, Ikar Munian, Fernando Llorente na Javier Martinez huku Guardiola akiwa Barcelona. Mechi zilizowakutanisha, zilikuwa za kuvutia sana kwa wapenda mbinu. Biesla ameichukua Leeds na kuibadilisha kwa kiasi kikubwa, sio kwa kusajili wtu wenye uwezo mkubwa Bali ni kwa kuwekeza katika mbinu na kuwatengeneza wachezaji waendane na mbinu hizo.

Hadi sasa zikiwa zimechezwa mech 24 tayari Leeds inaongoza ligi (championship) ukiwa na jumla ya alama 51 na ikiwa imetokea kushinda mechi 7 mfululizo zikiwemo zote walizocheza katika kipindi cha sikukuu mwezi wa 12 ambao ni mwezi wenye mechi nyingi mfululizo.

Biesla hupendelea sana mfumo wa 3-3-1-3 na Mara nyingi hata kama hupadilisha muundo wa wachezaj uwanjani lakini dhana hubaki kuwa ile ile, na ndivyo alivyoifanya Leeds msimu huu katika championship ambapo licha ya mfumo wa 4-1-4-1 na 4-2-3-1 ambapo wamekuwa wakiutumia. Mmabeki wa pembeni huingia ndani kushambulia kisha kutafuta pembe tatu na kupiga pasi na kumfikia kiungo mshambuliaji ambaye waargentina wanamwita “Enganche”.

Kisha baada ya kupokea mpira katika eneo hilo la uwazi, Biesla huwataka washambuliaji wake wa pembeni kutoa mapana, huku mshambuliaji wa kati mbele kuwa katikati na hiyo kumrahisishia “Engache” kazi kwa kupiga Pasi ya mwisho. Katika nafasi hii Biesla amemfanya Pablo Hernandez kuwa moto ambapo hadi sasa ametoa Pasi 10 za magoli katika Championship msimu huu.

Sambamba na hilo Leeds ina miliki mpira kwa sehemu kubwa ya michezo inayocheza, ukiwa na wastani wa zaidi ya 63% ya umiliki wa mpira kwa mechi (asilimia 5 zaidi yatimu yoyote katika mashindano hayo).
UUmiliki wa mpira unawafanya Leeds kuwa na mda mwingi wa kuamua nini wafanye wa Napoli wa na mpira na kwa uzuri tumeweza kuona Yale yaliyoandikwa na kocha Jed C.

Davies kwenye kitabu cha “THE PHILOSOPHY OF FOOTBALL: IN THE SHADOWS OF MARCELO BIESLA” ametulezea namna tatu za utengenezaji wa nafasi kwa Marcelo Biesla ambazo ni kutanua uwanja (mapana), Kuwavuta wapinzani kaajili ya kupata nafasi kati ya mistari ya wachezaji (between the lines) na pia kujaza watu upande mmoja na kisha kuhamisha upande wa ushambuliaji kwa haraka.

Haya yote yameonekana katika Leeds ya Marcelo Biesla. Vile vile katika kushambulia Biesla anaamini eneo ya mbele ya goli la upanzani likijulikana kama eneo la dhahabu au pembe C kwa baadhi ya makocha ambalo huzalisha zaidi ya 80% ya magoli yote yanayofungwa, ndio eneo linalofaha kushambuliwa zaidi. Mshambuliaji Kemar Roofe akiwa katika kiwango bora kabisa amefunga jumla ya magoli 13 na hayo yote ameyafunga ndani ya boksi katika eneo hilo.

Katika kuzuia, Leeds unaonekana kuzuia kama timu ambapo timu yoote hukaba kuanzia juu katika Muunganiko sahihi, ikijaribu kuupora mpira kwa haraka kutoka kwa wapinzani na kuuweka katika himaya yap kisha kutekeleza Yale ambayo KOCHA ameyakusudia kuyafanya timu inapokuwa na mpira, Leeds imefungwa magoli 22 katika mechi 24 za championship msimu huu wakiwa na jumla ya Clean sheet 10.

Mzunguko wa pili ukiwa umeanza, Leeds wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kurudi katika Ligi kuu ya uingereza na kuendelea kunogesha soka la uingereza kwani tutapata kushuhudia makocha wazuri na wabunifu wakikabiliana na hiyo kutoa burudani ya uhakika.


Makala na Robert Komba
0762283468, Robbiekomba@gmail.com

Barua ya 2018 haina utofauti sana na barua ya mwaka jana

$
0
0

Muda ndo kitu pekee ambacho hakisubiri huja na kuondoka ,muda ukitumika vizuri hujenga mipango na malengo mazuri ya kudumu usipotumika vizuri hauachi alama yeyote ile ya kukumbukwa, vyovyote vile muda utavyotumika mwisho wa siku huondoka mwaka 2018 kwenye maisha yetu ya soka la Tanzania haukua na tofauti yeyote ile na miaka iliyopita kilichobadilika kilionekana ni namba ya mwaka tu.

Ndani ya karibia siku 365 tuliyashudia matukio mengi yaliyoonekana hata miaka kumi nyuma vurugu katika mashindano ya ligi daraja la kwanza hakikua kitu kipya ndani ya mwaka huu kilichoonekana zaidi labda tumekataa kubadilika, viongozi ndani ya timu kuingilia majukumu ya benchi la ufundi kwa kuja na majina mfukoni kwao nani asajiliwe ndani ya timu bila kujali mahitaji ya msingi ya mwalimu nacho hakikua kitu kipya ndani ya mwaka huu la zaidi inasikitisha kwa nini mpaka leo tumekataa kubadilika any way ni maisha yetu acha tuendelee.

Bado katika siku hizo hatukuamua kujifunza kwa wenzetu ni nini wamefanya kuyafikia mafanikio yao tulishia kulitizima kombe la dunia likikatisha mitaa ya paris Ufaransa na tukageuza vichwa vyetu isharaya kuendelea na maisha yetu badala ya kujiuliza wafaransa wamefanya nini kabla hawajabeba kombe la dunia jitihada gani zimetumika na wao hatukutaka kabisa kufahamu kuwa klabu za ligi kuu ufaransa ndo mtaji wa yale yote tuliyoyaona kombe la dunia.

Tulifurahia kumwona varane jinsi anavyocheza lakini tukasahau namna alivyolelewa pale klabuni lens akiwa mtoto tukanogewa na kasi uwezo wa kipekee wa kylian mbappe lotin tukasahau wenzetu waliitambua uwezo wake akiwa na umri wa miaka tisa tu hakikua kitu kipya nacho ndani ya mwaka huu hata ukijiuliza sasa klabu gani ukiacha wauza juisi wana utaratibu mzuri wa kulea makinda na uhakika utabaki na swali lako.

Labda Ufaransa ni mbali sana ila hata kwa wenzetu Uganda tulioona tumetenganishwa nao kwa bahari kubwa sana ambayo hata kwa meli itatuchukua zaidi ya siku 365 kufika kunakoitwa Uganda ni nani alijiuliza kinachofanyika Uganda kwa nini wao kila itwapo leo timu yao ya taifa inafanya vizuri mbona ligi yao so maarufu kama yetu hakuna kiongozi aliyeenda maana angeenda angerudi na siri hii Uganda wamewekeza sana soka lao katika tasisi mbalimbali

Mfano katika tasisi ya elimu kuna uvunaji mzuri wa vipaji vya soka kupitia mashindano yaliyopo katika ngazi mbali mbali za elimu mfano kupitia idara ya vyuo vikuu kuandaa mashindano mengi imesaidia wachezaji wengi kupatikana walioleta matokeo chanya katika soka lao nalo hili halikua jipya kwenye soka letu maana kujifunza kwa wengine ni dhambi kwetu.

Labda kilichobadilika sana na cha kujivunia ni kuongezeka kwa hamasa ya wachezaji wetu wengi kwenda kucheza nje kwa hili angalau tunastahili pongezi vijana kama Kevin john wako nje .kitu ambacho kinaweza kuwa manufaa kwa baadae kama tutatengeneza wakina samatta wengi.
Nje ya hapo kwa mwaka unaokuja inatupasa tujipe tathimini kubwa ili yaliyotokea mwaka huu yasijirudie tena kwa manufaa ya soka letu karibu 2019.

Ujumbe kutoka kwa Meshack Melele.

Ramos 2018 aponea chupuchupu

$
0
0

Beki wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Hispania Sergio Ramos amemaliza mwaka 2018 bila kupata hata kadi moja nyekundu.

Inaweza kushangaza, kutokana na beki huyo mwenye umri wa miaka 32 kuwa na kadi nyingi zaidi kuliko mchezaji yoyote kwenye historia ya Laliga. Ana kadi 24 nyekundu katika miaka yote 16 aliyocheza mpira. Ni mchezaji aliyetolewa nje mara nyingi zaidi kwa kupata kadi nyekundu kwenye historia ya Laliga. Katika kadi 173 alizopata, 19 ni kadi nyekundu.

Kwenye Ligi Kuu Hispania, amepata jumla ya kadi nyekundu 19, kwenye Ligi ya Mabingwa ulaya ana kadi nyekundu tatu, na kadi nyingine mbili kwenye Copa Del Rey. Kwenye timu yake ya Taifa ya Hispania hakupata kadi nyekundu.

Tangu ahamie Real Madrid mwaka 2005, ni miaka mitatu tu ambayo hakupata kadi nyekundu. 2011, 2015 na 2018

Mwaka 2005 kadi 3

Mwaka 2006 kadi 2

Mwaka 2007 kadi 1

Mwaka 2008, kadi 3

Mwaka 2009, kadi 1

Mwaka 2010, kadi 2

Mwaka 2011, hakupata

Mwaka 2012, kadi 2

Mwaka 2013 kadi 4

Mwaka 2014 kadi 1

Mwaka 2015 hakupata

Mwaka 2016, alipata kadi 2

Mwaka 2017, alipata kadi 3

Mwaka 2018, hakupata

Sipo upande wa Shaffih wala upande wa Simba

$
0
0

Kumekuwa na kauli moja maarufu sana hapa nchini, “Anataka kututoa kwenye lengo” au “anataka kutuvuruga”. Hii kauli hutumiwa zaidi kuzuia watu kuisema Simba iwe kwa uzuri au ubaya. Manara hana makosa hata kidogo kuisifia klabu yake, hiyo ndio kazi yake. Lakini kuna mambo huwa siamini hata kidogo. Kuwanyima watu uhuru wa kusema wanayojisikia kuhusu Simba.

Manara na baadhi ya mashabiki wa Simba wanaamini kuwa ubora wa klabu yao utadumu kama klabu yao haitasemwa. Wanataka ipetiwepeitiwe, safi kila mtu lazima apende chake. Lakini msije mkaamini kwamba vilabu vikubwa ili vidumu havipaswi kusemwa.

Awali ya yote niwatoe hofu baadhi ya mashabiki wa soka wa Simba, kuwa treni haisimamishwi na honi ya baiskeli.

Simba wapo klabu bingwa hongera kwa hatua kubwa. Cha kusikitisha hawataki kabisa kusikia chochote kibaya kuhusu klabu yao. Iwe kweli au lah. Wao wanaamini piga ua alama 9 za hapa taifa lazima wazipate. Wana imani wanaweza baada ya kuwafunga Nkana FC.

Lakini kumtoa Nkana kusiwabweteshe!!. Nkana ni klabu ambayo iliwahi kuwa na mafanikio kiduchu klabu bingwa. Kwa sasa inajaribu kurudisha heshima mjini. Nkana FC naweza kusema ni sawa na Inter Milan ya sasa. Kiwango cha Simba labda tuseme kinakuwa kama KRC Genk. Genk ikimfunga Inter kufuzu UEFA haamaanishi kuwa kama atapangwa na Juventus na Atletico basi hilo kundi kwake nae atapewa nafasi kubwa kupita, kisa alimtoa Inter.

Simba yupo kundi gumu sana hapa naungana na Shaffih Dauda.

Wakati fulani inabidi ukweli usemwe ili ujue udhaifu wako na uutumie kama kigezo cha kupata unachokita.

Hivi mnataka tuwaambie kuwa Simba na AS Vital na Al Ahly mpo sawa? Uwekezaji wa Al Ahly kwa wachezaji kadhaa tu unatosha kuendesha ligi kuu bara miaka. Klabu ya Al Ahly ina thamani ya kikosi cha bilioni 78 za kitanzania. Sasa tukiwaambia ukweli mnapovukwa? Tazama chati hapo chini

No Klabu alama
1
Al Ahly – Egypt
1611
2
TP Mazembe – Congo DR
1595
3
Esperance – Tunisia
1583
4
Vita Club – Congo DR
1563
43
JS Saoura – Algeria
1475
Data hizi ni kwa mujibu wa footballdatabase
379
Simba SC – Tanzania
1247

 


Walio wengi ligi ya Afrika haitufuatilii ndio maana ni rahisi sana mtu kukwambia Simba na Vita wapo hadhi sawa. Huko ni sawa na kumpa nafasi Maccabi Haifa nafasi mbele ya Barca.


Vita sio timu ndogo. Vita imecheza mechi 45 ambapo imefungwa na timu za Congo mechi mbili tu [Mazembe 3-2 tarehe 4 mwezi wa 11, na kabla ya hapo ilifungwa miezi 8 iliyopita na Don bosco 0-2] Vita ilicheza takribani mechi 13 mfululizo bila kufungwa au kutoka sare ndani ya ligi kuu Congo kuanzia Tare 31/05 – 12/7 mwaka huu.

AS Vita iliwapiga wababe wa Simba Al Masry magoli 4. Mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Raja Cassablanca mchezo wa awali walifunga 3-0 Lakini wakiwa pale Congo Raja alikufa 3-1. Mashabiki wa Simba hata tukiwaambia hivyo tunawaharibia lengo?

Savio Kabugu beki wa SC Villa na timu ya taifa ya Uganda amesajiliwa na AS Vita

Wapo wengine wanadanganywa na baadhi ya taarifa ambazo hazijakamilika kwamba Al Ahly wapo vibaya kisa wapo nafasi ya 6. Kwanini hampendi kuchutama wakati wa mnavuliwa nguo? Al Ahly yupo nafasi ya 6 akiwa amecheza mechi ngapi?

Al Ahly amecheza mechi 12 tu na amefungwa michezo miwili akiwa na alama 24. Anayeongoza ligi Zamalek amecheza mechi 15 akiwa na alama 38. Waliopo juu ya Al Ahly wengi wao wao wamecheza mechi 18. Kama Al ahly atashinda viporo vyake vitatu atakwenda hadi nafasi ya 2. Al Ahly mwezi wa 10 walikumbwa na tatizo wakati kocha wao anaondoka. Mwaka huu mwezi wa 12 wameleta kocha mpya wa Uruguay Martín Lasarte na jahazi limetulia.

# M W D L G P
Zamalek SC 15 12 2 1 33:10 23 38
Pyramids FC 15 8 6 1 25:13 12 30
Masr El Makasa 17 8 3 6 19:15 4 27
Arab Contractors SC 16 8 2 6 23:16 7 26
Entag El Harby 18 6 8 4 19:18 1 26
El Ahly Cairo 12 7 3 2 18:9 9 24
Tala'ea El Gaish 18 6 6 6 25:22 3 24

Kumbuka wamemsajilia aliyekuwa kiungo bora wa ligi za Uarabun msimu uliopita.

El Shahata

Kiungo huyo anatokea klabu ya Al Ain waliocheza fainali ya klabu bingwa ya dunia na Madrid El-Shahat, kwa ada ya bilion 9 za Kitanzania. El-Shahata alicheza 33 akiwa Al Ain, nakufunga magoli 15 pamoja na assists 17.

Kiungo wa zamani wa Stock na Huddersfield Ramadhan Soby nae amarudi Al Ahly hivyo msiwapoze wenzenu kwa kuwadanganya Al alhy ya sasa ni mbovu. Tunaposema haya hatuwatishi, ila tunataka wajiandae katika hayo.

Simba nina uhakika kuna alama 6 kati ya 18 ambazo ana uwezekano mkubwa wa kupoteza. Shaffih amesema Simba ni Underdog na sio Favourite, ni kweli wala hakuna ubishi hapo. Vital 2014 walicheza fainali ya klabu bingwa, 2018 wamecheza fainali ya shirikisho. Al Ahly sina haja ya kuwaongelea sana. Hizi mechi mbili sina uhakika sana kama Simba anaweza kuambulia hapo alama 6 za ugenini.

Najua kwenye soka kuna kitu kinaitwa package of surprise. Na naamini katika hilo pia. Croatia kwenda fainali ya kombe la dunia, Korea kumfunga Ujerumani, Sweden kuwaondosha Italia, Leicester kutwaa ubingwa. Lakini package of surprise haiji kama miujiza. Ni Mipango thabiti na sio makelele. BVB 2013 waliushangaza ulimwengu wa soka kufika hadi fainali ya UEFA lakini haikuwa miujiza. Wale Wachezaji wao walikuwa na viwango maradufu.

Cassablanca vs vita fainali

Simba wasitarajie Package of Surprise kama hawajajiandaa kwa hilo. Package of surprise ni mipango, huwezi kutegemea package of surprise kwenye mechi 9, lazima ujiandae. Kujiandaa ni pamoja na kuyajua madhaifu yako. Madhaifu huwezi kutegemea akili yako pekee yako ndio maana wanazuka akina Dauda ambao wanaponda ili kuwatia hasira nyie mfanye kweli.


Mgema akisifiwa sana tembo hutia maji. Hatuwezi kutumia muda mwingi kuwapaka mafuta ilhali hatujawaambia mnawe.


Simba inapaswa kucheza kwa tahadhari kubwa sana. Kwanza wahakikishe Vita na Al Ahly mechi zote hawapotezi zaidi ya alama 4. Wahakikishe mechi zote hizo mbili hawakosi 4 kati ya 12. Utanishangaa sana kwanini. Vita na Al Ahly watakutana watachinjana, iwe sare au mmoja kushinda. Ili Simba isonge mbele pia wanapaswa kuhakikisha mechi yao dhidi ya JS Saoura hawakosi alama 3.5 yaani ushindi na sare.Kama watafungwa na mechi 3 za ugenini hapa nyumbani pia wanapaswa kushinda zote.

JS Saoura

Nimeona baadhi wakijaribu kuwachukulia kiurahisi hawa JS kisa tu wameanza 2008. Ndugu zangu wale JS hawana mchezaji ambaye thamani yake ni chini ya Euro milion 100, tena wachezaji ambao thamani yao ni ndogo ni

Thomas Ulimwengu
1993 (25) Tanzania
Seydouba Bissiri Camara
1995 (23) Guinea

Kikosi chao kina thamani ya hela za kitanzania bilioni 21.

Watu wanasema mpira una dunda, lakini haudundi wenyewe hadi udundishwe. Ukiwaambiwa umelogwa nenda kwa mganga kalogue au nenda kwa viongozi wa wakidini wakuombee na sio unalalamika tuna wivu. Hatuwachukii tunakumbusha.

Simba wanaweza kupindua matokeo lakini sio kwa kuwasifia au kuwatia moyo ila kwa kujipanga kisawasawa. Tusiwadanganyane kundi lao sio jepesi.

Mkuu wa wilaya aipeleka Simba robo fainali CAF

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba Adam Mgoyi amesema Simba nj moja ya vilabu vitakavyofuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Mgoyi amesema kundi ilipo Simba ni gumu lakini imeonesha nia ya kufanya vizuri katika hatua zote toka inaanza mechi za hatua za awali za ligi ya mabingwa Afrika.
.
“Simba ni timu nzuri kwa kiwango cha mpira wa Tanzania nadhani ni timu bora na haya yaliyotokea hayajatokea kwa bahati mbaya kwa sababu viongozi walijipanga na wakaweka ahadi ya kufika hatua ya makundi kwa hiyo hawajaingia kwa bahati mbaya.”
.
“Aina ya timu ambazo zipo kwenye makundi lazima ziwe bora kwa sababu timu 16 Afrika nzima zilizoingia hakuna timu dhaifu kwa sababu hata sisi tumeingia kwa kuitoa timu bora Nkana kwa hiyo tunaenda kushindana na timu zenye uwezo kama sisi, kitakachotokea ni matokeo ya mpira.”
.
“Kwa uwezo wa mwalimu tuliyenae na kwa uwezo wa wachezaji wetu naimani tutaingia hatua ya robo fainali.”

Mgoyi amesema ukichunguza timu zilizofuzu hatua ya makundi utaona timu nyingi zimewahi kuwa mabingwa wa mashindano haya kama sio klabu bingwa basi ni kombe la shirikisho kwa hiyo timu ambazo zimepangwa kundi moja na Simba ni sawa na za makundi mengine.

Anasema Simba waliwahi kuitoa Zamalek pamoja na kuzifunga timu nyingine za kiarabu kwa hiyo hakuna shaka kikubwa ni kocha kuwaandaa wachezaji na wao wawe tayari kupambana.

Katibu Coastal Union ang’atuka

$
0
0

Katibu Mkuu wa Coastal Union Abdulatif Omary Samau ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miezi mitatu.

“Ni kweli nimejiuzulu kutoka kuwa katibu mkuu wa Coastal Union, nitabaki kuwa mwanachama wa kawaida. Nimehudumu tangu mwezi wa 9 mwanzoni mpaka mwishoni mwa mwezi wa 12 kwa hiyo nimeona niweke wazi kujiuzulu kwangu kwa sababu kwa siku napokea zaidi ya simu 10.

“Niliajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na niliwapa notice ya mwezi mmoja kabla (mwezi wa 12 mwanzoni) kwa kuwaandikia barua kuwa najiuzulu nafasi yangu ili watafute mtu mwingine ikifika December 31 nitakuwa si katibu tena wa Coastal Union.”

“Sababu zipo nyingi lakini kuna sababu moja kubwa, wakati naajiriwa Coastal Union nilikuwa nina shughuli zangu binafsi kama kijana, ikabidi niweke pambeni shughuli zangu ili nifanye shughuli za Coastal lakini sasa nimeona nirudi kwenye shughuli zangu kwa sababu zina dorora na waswahili wanasema mshika mawili moja humponyoka.”

Inasemekana viongozi hawazungumzi lugha moja ndani ya kamati ya utendaji na baadhi wamejigawa, kuna kundi la uongozi la Dar na kundi jingine la Tanga.


Taarifa kuhusu maendeleo ya Sanchez, Salah, Mane, Auba vitani.

$
0
0

Dirisha la usajili limefunguliwa rasmi leo na klabu ya West Ham imekamilisha dili la kumrejesha Samir Nasri EPL tena!

Ole Gunnar amethibitisha kurejea kikosini kwa nyota wa United Alexis Sanchez. Sanchez anatarajia kujumuishwa kikosini kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Newcastle united.

Beki wa klabu ya Napoli Kalidou Koulibally ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa nchini Senegal. Koulibaly amewabwaga, Sadio Mane , Youssof sabaly…

Kinyang’anyiro cha Mchezaji bora wa mwaka CAF 2018 kimefikia fainali. Majina matatu yamethibitishwa na CAF.

Nyota hao watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika 2018

1. Mo Salah – Liverpool / Misri
2.Aubameyang – Arsenal / Gabon
3. Sadio Mane – Liverpool / Senegal .

Chelsea yatupilia mbali ofa ya Bayern, Vardy aweka rekodi

$
0
0

Klabu ya Chelsea imekataa ofa ya Paundi milion 20 kutoka kwa klabu ya Bayern Munich kumsajili kinda wao Callum Hudson Odoi.

Chelsea wamesema kuwa kinda huyo anapatikana kwa dau la Paund milion 40. Imeripotiwa pia klabu ya BVB nayo inawinda saini ya kinda huyo wa kiingereza.


Goli la kwanza kila tarehe 1 ya mwaka mpya: EPL
:
2011 – Wayne Rooney
2012 – Victor Anichebe
2013 – Dimitar Berbatov
2014 – Fernandinho
2015 – Ryan Shawcross
2016 – Michail Antonio
2017 – Harry Kane
2018 – Anthony Knockaert
2019 – Jarmie Vardy


Leicester Kristmasi – Mwaka mpya:

Dec 22: Chelsea (A) W1-0 ✅
Dec 26: Man City (H) W2-1 ✅
Dec 29: Cardiff (H) L0-1 ❌
Jan 1: Everton (A) W1-0 ✅

🦊 alama 9 ndani ya siku 11 🔥


Tuzo

Unadhani nani anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa 12 katika Klabu ya Manchester United?

1. Paul Pogba

2. Marcus Rashford

3. Jesse Lingard


Miaka miwili imepita tangu Olivier Giroud alipofunga goli la Scorpion kick akiwa na klabu ya Arsenal, lililopelekea kushinda tuzo ya Puskas award


Fowadi wa Bayern Munichen Roberto Lewandowski amesema atamalizia soka lake ndani ya klabu yake. Roberto ambaye mkataba wake unatamatika 2021 msimu uliopita alifunga mabao 22 na kuisaidia klabu yake kutwaa ubingwa.


Isco amesema haondoki Madrid na ana furaha sana klabuni hapo. “Siendi popote majira haya. Nina furaha wala sina tatizo” Isco


“Ronaldo ni mtu mwenye roho ya kipekee. Kuna kipindi tulisafiri kwende nchini Marekani, Ronaldo aliwanunulia wafanyakazi wote wa Madrid tuliosafiri nao (15) simu za gharama” Kaka

Taarifa kuelekea mchezo wa United vs Newcastle

$
0
0

Newcastle Vs Manchester United, mchezo huu utapigwa majira ya saa 23:00 usiku katika dimba la St.James park.

Newcastle, walimfunga Manchester United, bao 1-0 msimu uliopita katika uwanja wa nyumbani St.James park kwenye ligi kuu pia hajawahi kushinda michezo miwili mfululizo katika uwanja wa nyumbani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1987.

Manchester United, wamepoteza mchezo moja kati ya michezo nane dhidi ya Newcastle, ameshinda mara 5 na sare 2 mara ya mwisho kupoteza mchezo dhidi ya Newcastle ilikuwa katika uwanja wa St.James Park mwezi February 2018 kwa bao 1-0.


Claude Makelele amesema kitendo cha Pogba kufunga bao na kucheza ni kudharau wapinzani wake aliowafunga. Mambo kama hayo amemshauri ayafanye kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

“Kumfunga mpinzani wako goli 4 kisha unacheza mbele yake sio jambo la hekima hata kidogo” Makelele


Rafael Benitez, ameshinda michezo minne ya mwisho katika uwanja wa nyumbani akiwa kocha wa timu tofauti alizowahi kuzifundisha pale Uingereza.

Manchester United, wameshinda michezo 67 kati ya michezo 99 waliyocheza mwezi wa Kwanza kwenye ligi kuu England.

Newcastle,wamepoteza michezo 7 kati ya michezo 10 ya ligi kuu katika uwanja wa nyumbani msimu huu ameshinda mara 1 na sare mara 1 pia msimu wa mwaka 2012-13 walipoteza michezo 9 na msimu wa mwaka 2013-14 walipoteza michezo 8.


Ole Gunnar Solsjker, anaangalia uwezekano wa kuwa kocha wa pili wa Utd, katika historia kushinda michezo minne ya ligi kuu baada ya Matt Busy, mwaka 1946.

Uchambuzi na Azizi Mtambo


KWINGINEKO

” Tuna matatizo mengi kulinganisha na timu nyingine lakini ni wajibu wetu kuyageuza matatizo yetu kuwa furaha. Daima huwa nawaambia wachezaji hii ni timu ya ushindi hivyo lazima tuilinde hiyo dhana kwa kutafuta ushindi kila mechi” – Mwinyi Zahera Kocha mkuu Yanga SC


Ligi kuu KENYA itaendelea hivi leo!: #KPL

2:30 PM
Mount Kenya Utd Vs Kariobangi Sharks

4 PM
Mathare Utd Vs KCB
Nzoia Sugar Vs Ulinzi Stars
Posta Rangers Vs AFC Leopards
Zoo Vs Bandari FC
Western Stima Vs Sofapaka
Sony Sugar Vs KK Homeboyz
Tusker FC Vs Vihiga Utd

5 PM
Gor Mahia Vs Chemelil Sugar

Uchambuzi wa Chelsea vs Southampton

$
0
0

Mtanange huu utachezwa saa 22:45 usiku ndani ya Stamford Bridge.


Soton leo wana mtihani mzito sana. Kocha mpya wa Southampton anatarajia kuhakikisha klabu yake leo inarudia rekodi ga mwaka 2017 ya kushinda mechi mbili mfululizo za ugenini. Mara ya mwisho kushinda ilikuwa mwaka 2017 walimfunga Sunderland na Watford.


Nafasi ya 4 imekuwa ngumu sana msimu huu. United nao wanakuja kwa kasi, Arsenal pia hawakati tamaa. Chelsea na Spurs bado wanavutana mashati.

Soton kwa Kipind cha hivi karibuni wamekuwa vibonde wa Chelsea. Chelsea wameshinda michezo yote 7 ya mwisho waliocheza dhidi yaSouthampton. Soton watajaribu leo kushinda Stamford baada ya kufanya hivyo ilikuwa October 2015 Chelsea iliyokuwa chini ya Jose Mourinho, kwa mabao 3-1.

Kocha wa Soton Ralph Hasenhuttl amethibitisha kuwa James Ward-Prowse atakuwa nahodha wa kikosi cha Southampton kitakachowavaa Chelsea baada ya nahodha Pierre-Emile Hojbjerg kukumbwa na marufuku.


Klabu ya Chelsea imekubalia kutoa dau ya Paundi 64 milioni kumnasa nyota wa BVB Christian Pulisic

Swali ni je Soton wanaweza kuvunja rekodi ya Chelsea ya kutokufungwa mechi 2 mfululizo za nyumbani? Kwank Chelsea, hawajawahi kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye ligi kuu katika uwanja wa nyumbani. Mara ya mwisho kutandikwa mechi 2 mfululizo pale darajani ni miaka 7 iliyopita 2011 ambapo walipokea kichapo kutoka kwa Arsenal, na Liverpool. .

Lakini bado rekodi mbovu wa Southampton dhidi ya timu za London inazidi kutia wasiwasi kwa Soton kupata matokeo hivi leo. Soton wamepoteza michezo 9 kati ya michezo 11 ya ligi kuu dhidi ya timu za zinazotokea mji wa London wameshinda michezo 2 tu.


Christian Pulisic Bundesliga :
15/16: 👕09 ⚽2
16/17: 👕29 ⚽3 🅰8
17/18: 👕32 ⚽4 🅰6
18/19: 👕11 ⚽1 🅰2

Je anathamani ya £58m?


Kidokezo: Hii ni kwa mara nyingine tena Chelsea wanacheza mchezo wao wa Kwanza ndani ya mwaka 2019 katika uwanja wa nyumbani. Mara ya mwisho kufanikiwa kuanza mwaka mpya wakiwa nyumbani ilikuwa mwaka 2013. Lakini katika mtanange huo wa mwaka mpya Chelsea walibamizwa na QPR, kwa bao 1-0 huku nyota wao wa zamani Shaun Wright Phillips akitandika msumari huo.


Taarifa za kikosi Chelsea

Majeruhi: Cesc Fabregas (Shingo), Ruben Loftus-Cheek (mgongo), Pedro (nyama za paja) and Callum Hudson-Odoi (nyama za paja)

Grioud pia anasumbuliwa na kifundo cha mguu

Utabiri: Kepa, Azpilicueta, Luiz, Rudiger, Alonso, Kante, Jorginho, Kovacic, Willian, Morata, Hazard.

Waamuzi wa kitanzania wapata hadhi ya kuchezesha mechi kubwa za FIFA

$
0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limetuma orodha ya Waamuzi wa Tanzania watakaochezesha mechi za kimataifa wakiwa na beji ya FIFA.

Katika orodha hiyo wapo waamuzi wa katikati na Waamuzi wasaidizi wa Kiume na wa Kike.

Aidha wapo pia waamuzi watakaochezesha soka la Ufukweni.

Waamuzi wa katikati Wanaume
1 NASSORO Mfaume Ali
2 SASII Hery Ally
3 MWANDEMBWA Emmanuel Alphonce
4 SAANYA Martin Elifhas


Katika fainali ya kwanza ya Ndondo Cup2014 waamuzi walikuwa Hery Sasii, Helen Mduma, Idd Lila na Shafii Moh’d wakati huo hawakuwa na “badge” yoyote

Waamuzi hawa wamechezesha tena Fainali ya 5 Ndondo Cup2018 watatu kati yao (Hery Sasii, Helen Mduma, Idd Lila) wana badge za FIFA


Waamuzi Wasaidizi

1 CHACHA Ferdinand
2 KINDULI Mgaza Ally
3 LILA Soud Iddi
4 KOMBA Frank John
5 MKONO Mohamed Salim
6 HAULE Mbaraka Haule

Waamuzi wa Soka la Ufukweni

1 MSILOMBO Jackson Steven
2 MWAMBONEKO Geofrey Tumaini

Waamuzi wa katikati Wanawake

1 KABAKAMA Jonesia Rukyaa
2 CHIEF Florentina Zabron

Waamuzi wasaidizi Wanawake

1 MDUMA Hellen Joseph
2 WAMALA Grace
3 BALAMA Janet Charles
4 MTWANA Dalila Jafari
.
.

Wanampokea Pulisic lakini Hazard atabaki msimu ujao?

$
0
0

Chelsea wamekamilisha usajili wa winga Christian Pulisic kutoka Borussia Dortmund kwa pauni milion 64. Pulisic anawasaidia kwanza Dormund kuwania ubingwa wa Bundesliga na ubingwa wa Uefa Champions League, halafu msimu ujao aanze mikimiki ya Ligi Kuu Uingereza.Chelsea wameamua kumaliza mapema, hawataki usumbufu kwenye majira yajayo ya kiangazi. Lakini moja ya swali kubwa ni kwamba, Hazard anabaki msimu ujao? Ingekuwa kombinesheni nzuri kuona Pulisic akitokea kulia na Hazard akitokea kushoto.Hazard amekuwa muhimu sana kwa Chelsea kwenye kutengeneza nafasi, kufunga, na kuamua matokeo.


Pedro (31, mkataba unaisha 2020)Willian (30, mkataba unaisha 2020)Hazard (27, mkataba unaisha 2020)
Msimu huu, Chelsea wamewategemea sana Hazard na Ngolo Kante katika kutengeneza nafasi za kufunga. Bila Hazard kuna tatizo kwa Chelsea. Itakuwa nafuu zaidi wakimbakisha Eden Hazard msimu ujao kuliko akiondoka.
Orodha ya sajili za gharama katika historia ya klabu ya ChelseaKepa Arrizabalaga (£71.6m)Álvaro Morata (£70m)Christian Pulisic (£57.6m)Jorginho (£57m)Fernando Torres (£50m)(Chanzo: Sky Sports)
Ukiona ujio wa Pulisic, tambua Willian au Pedro, kuna mmoja atatafuta mlango wa kutokea. Ni rahisi kukubali Willian aondoke lakini sio Hazard. Tatizo la Chelsea sio kwenye idara ya winga wa kulia ambalo wanacheza Willian na Pedro, ila hata kwenye idara ya ushambuliaji ni tatizo kubwa sana tangu Diego Costa ende zake Hispania.Kuna mechi niliona Maurizio Sarri akimpanga Hazard eneo analocheza Alvaro Morata. Hii ni kwasababu haridhishwi na idara ile ambayo wapo Morata na Giroud. Kumpanga Hazard namba tisa ni sawa na kumchezesha Ngolo namba saba.
Roberto Martinez- “Hazard ni mchezaji anayejali sana wachezaji wenzake sana. Ana roho ya kiupekee sijui kama akienda sehemu nyingine ataweza kuishi vizuri kama anavyoishi na wenzake Chelsea. Chelsea wanampenda sana. Mfumo wa Sarri na uwezo wake umeiviana sana. Hapaswi kuondoka” Hazard akicheza winga wa kushoto, Chelsea inakuwa bora zaidi maana nafasi nyingi za kufunga zinapatikana na timu inaonekana bora zaidi.Wakati Sarri anaendelea kuongeza ubunifu ndani ya uwanja na kutafuta mshambuliaji ambaye hawaangushi walioko nyuma yake, basi aombe Hazard abaki. Najua Hazard anaweza kuondoka na maisha yakaendelea lakini lazima upate shida kupata mbadala. Pulisic bado kijana mdogo aliyezaliwa mwaka 1998. Ana miaka 20 bado, hakuna anayewaza kwamba anakuja kuwa mbadala wa Hazard.Kila mtu anafikiria namna muunganiko utakavyokuwa endapo Pulisic na Hazard wakishirikiana kupika magoli pamoja na kufunga.Makala na Patrick Admila
Kidokezo: Kane amebakiza goli moja tu kuvunja rekodi ya Dwight Yorke ya mabao EPLHary Kane (Mechi 174 – Magoli 122)Dwight Yorke (Mechi 375 – Magoli 123)Yorke amecheza mechi 201 zaidi ya Hary KaneKane vs Mafowadi wengineKane 122 ⚽ Mechi 174Yorke 123 ⚽ Mechi 375Anelka 125 ⚽ Mechi 364Keane 126 ⚽ Mechi 349Hasselbaink 127 ⚽ Mechi 288
Wachezaji bora wa BVB waliouzwa kwa gharama kubwa ndani ya miaka 3:📅 16/17:❌ Mkhi, Hummels, Gundogan, Blaszczykowski.💰 €111m.📅 17/18:❌ Dembele, Aubameyang, Ginter, Mor, Bender, Ramos.💰 €251m.📅 18/19:❌ Pulisic, Sokratis, Yarmolenko, Merino, Castro.💰 €114m.

Taarifa kuelekea Man City dhidi ya Liverpool

$
0
0

Manchester City Vs Liverpool, mchezo huu utapigwa majira ya saa 23:00 kamili usiku katika dimba la Etihad stadium.

Manchester City, wameshinda mchezo moja kati ya michezo 11 waliyokutana na Liverpool, kwenye michuano yote sare 3 amepoteza 7 mchezo huo ambao City, alimfunga Liverpool, ilikuwa msimu uliopita kwa mabao 5-0 kwenye ligi kuu katika dimba la Etihad.

Liverpool, wameshinda mchezo moja kati ya michezo sita waliyocheza katika dimba la Etihad sare 3 kupoteza 5 pia mechi ya Kwanza Jurgeon Klopp, kwenda Etihad, alishinda kwa mabao 4-1 tangu awe kocha wa Liverpool, kwenye ligi kuu pia Liverpool, katika hiyo michezo 6 wameruhusu mabao 20.


Hata kama tutafungwa leo bado hakuna kitakachotuzuia kutwaa ubingwa msimu huu”

Pep Guardiola, amepoteza michezo mingi mbele ya Klopp amepoteza michezo 7 ndo kocha aliyepoteza michezo Mingi mbele ya Klopp.

Mara ya mwisho City, kupoteza michezo miwili mfululizo katika uwanja wa nyumbani kwenye ligi kuu ilikuwa dhidi ya Leicester City na Tottenham pia Pep Guardiola, ajawahi kupoteza michezo miwili mfululizo katika uwanja wa nyumbani.

Aguero amefunga mabao sita dhidi ya Liverpool, katika uwanja wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu England.

Mo Salah, amehusika katika upatakanaji wa mabao 5 katika michezo minne dhidi ya City, kwenye michuano yote amefunga mabao 3 na assist 2.

Mchezo uliopita Roberto Firmino, alifunga mabao 3 dhidi ya Arsenal, amekuwa Mbrazil, wa Kwanza kwenye ligi kuu kufunga mabao 43 pia amehusika kwenye upatikanaji wa mabao 6 katika michezo 7 dhidi ya City, mabao 3 na assist 3.

Makala kutoka kwa Azizi Mtambo


KWINGINEKO

Klabu ya Chelsea bado haijatosheka.. Wanamtaka kinda wa PSV fundi mmoja matata Hrving Lozano kwa kitita cha Paundi milioni 36.
:
Kinda huyo mwenye miaka 23 anatarajia kuvaa viatu vya Alvaro Morata ambaye kiwango chake kimezorota.
:

:
Takwimu zake: Hirving Lozano PSV Eindhoven 2018:

• 41 Mechi
• 21 Magoli
• 11 assists


Liverpool yatoa ofa ya mkataba kwa nyota wake, Ramsey na Fabregas wanasepa

$
0
0

Klabu ya Liverpool inaangalia uwezekano wa kumuongezea Daniel Sturridge (29) mkataba mpya.


Klabu ya Watford imesema haipo tayari kumuuza ya kiungo wao mahiri Abdoulaye Doucoure kwa dau la Paundi milion 50 kwa klabu ya PSG.


Monaco na Chelsea wako mbioni kukamilisha dili la Cesc Fabregas. Fabregas amekosa namba ya kudumu klabuni hapo hivyo yupo mbioni kutafuta makazi mapya


Spurs wamesema hawapo tayari kumuuza Christian Eriksen kwa dau lolote. Klabu yake imesema ipo tayari kumuongeza mkataba na mshahara mnono. Kwa sasa Eriksen analipwa 70k kwa wiki.


“Ozil yupo tayari kubaki Arsenal hata baada ya mkataba wake kuisha” Wakala wa Ozil


Mkurugenzi wa michezo wa Juventus amekiri kweli klabu yake inaangalia uwezekano wa kumnasa Aaron Ramsey.


Unamtaka Kalidou Koulibaly? Andaa Bilion 302.6 za Kitanzania. Unadhani klabi gani inaweza kutoa hili dau United? Barca? Arsenal?


Romelu Lukaku ameonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi kadhaa za mwishon

v Bournemouth
⬆ 70 dakika
⚽ 72 dakika

v Newcastle
⬆ 63 dakika
⚽ 64 dakika


City na Liverpool nani apongezwe zaidi?

$
0
0

Makala na Patrick Admila

Niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja shabiki mkubwa wa Liverpool anaitwa Nasri. Hakuwahi kuamini maneno yangu hata siku moja. Nilimwambia Liverpool haiwezi kubeba taji ikiwa na Henderson pamoja Lovren. Leo ameamini maneno yangu.Nilivyoona kikosi cha Liverpool kinaongozwa na Henderson, Milner pamoja na Wijnaldum nilisubiri kuona watakavyoteseka kwenye eneo la kiungo. Mara nyingi tumezoea kuona Pep Guardiola akitumia mabeki wa pembeni wenye kasi na uwezo wa kupandisha timu, lakini leo aliamua kuwapanga Laporte na Danilo.

Alijua Salah na Mane watapitia upande ule. Mwisho wa siku Firmino akaangukia kwa miguu ya Fernandinho, Kompany na Stones. Ukiona ule utatu wa Salah, Mane na Firmino unahangaika kutafuta mipira basi ujue akina Henderson na Milner hakuna kazi wanayoifanya.


Mane pasi 18 dakika 77Salah pasi 20 dakika 90Xhakiri pasi 20 dakika 18Chanzo © whoscored


Liverpool walipotea katikati ya kiwanja. Henderson, Wijnaldum, na Milner kuna hata kiungo yoyote pale anayeweza kuituliza timu? Hakuna. Henderson anapiga zile pass za pembeni tu ambazo sio za kuifanya timu iwe mchezoni. Nilifikiri Fabinho angeanza maana ndiye kiungo pekee wa Liver mwenye uwezo wa kuifanya timu itulie na imiliki mpira katikati.


BEST UNBEATEN :38 Michezo – Arsenal (2003/04)24 Michezo – Man Utd (2010/11)22 Michezo – Man City (2017/18)21 Michezo – Liverpool (2018/19)


Mwisho wa siku tumeona Fernandinho na Bernado Silva wakitakata uwanjani. Bernando hata kama hana mpira unamfurahia namna anayokimbia uwanjani dakika zote tisini. Kiukweli yeye na Fernandinho wameifanya safu ya kiungo ya Liver ionekane nyanya. Vijana waliokuwa na kazi kubwa usiku wa leo, walikuwa ni Robertson pamoja na Trent Anod.


Salah aligusa mpira mara 32 tu idadi ndogo zaidi kwa wachezaji wote katika mchezo huo

Walijitahidi sana kupambana ila mtu pekee aliyewaangusha ni Lovren. Lovren mara nyingi anakuwa ( out of position) hakai kwenye nafasi yake sahihi. Ukiona beki anafanya makosa yanayojirudia kila wakati, usitegemee atabadilika.Pamoja na hayo yote, kila timu ilijaribu kufanya kile ilichoagizwa na mwalimu lakini mwisho wa siku lazima tuwape sifa Man City ambao walikuwa bora uwanjani na waliamua hii mechi ya leo, waicheze kama fainali.


Tumepata matokeo kutoka kwa timu ngumu sana. Mapambano yanaendelea” AgueroKWINGINEKOBeki wa Klabu ya Spurs aliyekuwa akiwindwa na United Tobby Ardeweilld ameongeza mkataba mpya mpaka 2020

Wachezaji waliowahi kupoteza unahodha kwa sababu za Kinidhamu kama Yondani

$
0
0

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amemvua kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yondani na kumteua Ibrahim Ajibu kuchukua nafasi hiyo kwa madai kuwa Yondani alichelewa kuripoti mazoezini baada ya siku tano za mapumziko walizopewa kumalizika.


WILIAM GALAS

Baada ya msimu mbaya mwaka 2008 Galas aliwafokea sana na kuwatuhumu wachezaji wenzake kuwa wana viwango vibovu.

“Wakati wa mechi wachezaji wanakuja kwangu kama nahodha na kuniambia kuwa kuna wachezaji wanazingua. Ukimfuata mchezaji husika anayelalamikiwa anakutukana. Siwezi kutaja majina lakini kuna wachezaji wengi hawajielewi” Galas.

Baada ya kauli hizi Galas alivuliwa unahodha.


SAMUEL ETO’O

baada tu ya kuvuliwa unahodha, Etoo nae aliamua kujiuzulu kuichezea timu ya taifa. Nafasi yake ya unahidha ilichukuliwa na Stephane M’bia mwezi agosti mara baada ya kombe la dunia 2014.

Samuel Eto’o alinyang’anywa kitambaa kutokana na dharau na kauli chafu kwa uongozi wa soka wa taifa hilo. Mwaka 2012 Eto’o alishtumiwa sana na kocha Denis Lavagne na kutaka avuliwe unahodha. Eto’o alipigwa marufuku ya kutokucheza miezi 8 alipowachocheza wenzake kutokucheza mechi ha kirafiki dhidi ya Algeria baada ya wachezaji kutokulipwa posho na shahiki zao.


GRAZIANO PELLE

pelle anaweza kuwa kipenzi kikubwa sana cha klabu ya Southampton lakini kule Uholanzi anaweza kuwa wakati mgumu zaidi katika klabu yake ya Feynoord. Baada ya mchezo wao dhidi ya FC Twente kwenda sare ya 2-2 alionekana kuwa na jazba kubwa huku akipiga teke jukwaa dogo la makocha uwanjani. Baadae kwenye mkutano wa waandishi wa habari alisikika akiwaponda wachezaji wenzake huku akiongea kauli chafu kuhusu kiwango cha klabu. Baadae kocha mkuu alimvua unahodha na kipigwa marufuku ya kucheza mechi 4.


MTUKUTU JOE BARTON

Baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwemye mchezo wa QPR dhidi ya Man City Barton alivuliwa unahodha wake. Barton alimpiga Carlos Tevez kiwiko. Baadae alimoiga Aguero akiwa anajaribu kumpiga kichwa nahodha wa City Vicent Kompany. Baada tukio Barton alivuliwa kitambaa na kuondoka klabu hapo kwenda Rangers.


JOHN TERRY

Baada ya kutembea na mke wa mchezaji mwenzake Owen Bridge, Terry alivuliwa unahodha wa timu ya taifa ya England na kocha Fabio Capello.

Zahera ambwaga Yondani, Himid atakata

$
0
0

Kuelekea Machi kwenye mchezo wa kufuzu Afcon kati ya Tanzania na Uganda, Kiungo Himid Mao ameiwezesha timu yake ya Petrojet ya Misri kuingia nusu fainali ya Egypt Cup wakishinda 2-1 dhidi ya ENNPI


MSHAMBULIAJI wa Yanga Heritier Makambo amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019,Makambo alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Miraji Athumani wa Lipuli na Idd Selemani wa Mbeya City alioingia nao fainali


Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa mwezi Desemba akiwashinda Kocha Mkuu wa Lipuli, Samuel Moja na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime aliongia nao fainali.

Taarifa zote na TFF


Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amemvua kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yondani na kumteua Ibrahim Ajibu kuchukua nafasi hiyo kwa madai kuwa Yondani alichelewa kuripoti mazoezini baada ya siku tano za mapumziko walizopewa kumalizika.

Taarifa na Azam


“Waalgeria wameshaanza kuogopa mwamko mkubwa wa mashabiki wa Simba. Tunawaomba mashabiki mjae kwa wingi. Kama timu na uongozi mzima tumejipanga kuwapa raha watanzania. Wale wanaosema hatutafuzu robo fainali sisi hatuna maneno, vitendo vitaongea” Haji Manara

Simba vs Yanga Klabu Bingwa

🦁Simba S.C
🎽Mechi – 71
⚽Magoli ya kufunga – 86
🎯Magoli ya kufungwa – 91

🔰Yanga S.C
👕Mechi – 79
⚽Magoli ya kufunga – 120
🎯Magoli ya kufungwa – 108

Chanzo © Wikipedia

Ramsey kutua Juventus, Pogba apata majeraha.

$
0
0

Juventus yamtengea Aaron Ramsey mshahara mnono wa Tsh Bilion 21.1.Takwimu za Ramsey Arsenal🎽Mechi 389✅Magoli 65🎯Assists 66


📝Wachezaji waliosajiliwa bure na Juventus✅ 2009: Fabio Cannavaro✅ 2011: Andrea Pirlo✅ 2012: Paul Pogba✅ 2013: Fernando Llorente✅ 2014: Kingsley Coman✅ 2015: Sami Khedira✅ 2016: Dani Alves✅ 2018: Emre Can⏳ 2019: Aaron Ramsey
Kocha mkuu wa Dorados de Sinaloa, Diego Maradona amekumbukwa na mshtuko kutokana na matatizo ya kifamilia. Mshtuko huo umemfanya ashindwe kuhudhuria mazoezi ya klabu yake huko nchini Mexico.
Zola amesema anatamani kumuona kinda wa klabu hiyo Hudson-Odoi kubakia darajani.
Kocha mkuu wa Man United Ole Gunnar amesema kuwa anatarajia kukutana na bosi wake Ed Woodward kuhusiana na usajili wa mwezi huu januari.”Nitamtafuta bosi, najua wana mpango na dirisha hili la usajili” Ole Gunnar.
“Hakuna sababu ya Kupaniki” Van Djik. Kila mtu alijua mchezo utakuwa mgumu, hakuna haja ya kupoteza muda wa kujadili kilichotokea. Kila kitu kilikuwa wazi. Ligi haijaisha bado tuna mechi nyingi sana” Van Djik
Mario Baloteli anatarajia kurudi tena ligi kuu England. Zamu hii inasemekana kuwa Baloteli anatarajia kujiunga na klabu ya Newcastle
Paul Pogba atakosekana kwenye mchezo wa kombe la FA hapo kesho dhidi ya Reeding baada ya kukumbwa na majeraha.Wachezaji wengine ambao hawatakuwepo katika mchezo huo ni Cris Smalling, Marcus Rojo ambao bado hawajacheza mchezo wowote kwenye kikosi cha Ole Gunnar.
Nathaniel Clyne amemshindwa Arnold Alexandra na ameamua kutimkia AFC Bournemouth kwa mkopo.
Klabu Stoke City imekamikisha usajili wa Benik Afobe kutoka Wolves na Ryan Woods kutoka BrentfordFC
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>