Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

UCHAMBUZI WA KINA MECHI KATI YA MANCHESTER VS LIVERPOOL

$
0
0

Manchester-utd-vs-Liverpool

Na Nicasius Nicholaus Agwanda (Nicasius Coutinho Suso)

Mchambuzi wako Nicasius anakuletea kona tano za kila upande zitakaoamua mchezo huu. kwa kuanza na Manchester United zifuatazo ni njia tano zinazoweza kuwapa matokeo mbele ya Liverpoolkwenye mchezo wa leo.

1. Vunja Daraja analopita James Milner

Njia ya awali kabisa ni Manchester United kumnyima muda Milner kwenye kumiliki mpira au kuanzisha mashambulizi. Kumkosa Coutinho inawamaliza Liverpool katika nyanja ya kuwa na mchezaji mbunifu anayeweza kuisukuma Liverpool mbele pasipo kusita na kuchoka na kuifungua ngome ya ulinzi. Firmino hajapata fomu yake ya timu ya taifa na kule katika Bundesliga katika klabu ya Hoffenheim, wakati Emre Can hata timu ya Taifa baada ya kuitwa kacheza kama beki, ni mchezaji mzuri lakini bado hajahodhi eneo la kiungo.

2. Mpe nafasi Fellain

Mchezeshe Marouane Fellain. Anapata magoli sasa katika  timu ya taifa ambayo naamini yamemjenga. Ana attribute/sifa kubwa ambayo Liverpool wanaikosa sana na hilo ni uwezo wake mkubwa wa kushinda mipira ya juu, kwahiyo hapa unategemea mipira ya juu ataishinda kwa wastani walau zaidi ya nusu. Hapa unapata upenyo dhidi ya Liverpool, na kumpunguzia Pressure Wayne Rooney, pia huyu vurugu zake zinaweza kukupa uraisi wa kuvunja daraja la Milner kwani anaweza kuhimili nguvu za James Milner.

3. Van Gaal heshimu nafasi ya Michael Carrick

Mchezeshe Michael Carrick kama yupo fiti. Ukimkosa Coutinho, maana yake Liverpool haina mchezaji mbunifu mwingine mwenye uzoefu na mechi hii. Hivyo huhitaji nguvu kubwa ya uzuiaji ila unahitaji mchezaji mtulivu anaeweza kuifanya timu ikae katika mlinganyo wenye utulivu kuanzia nyuma na sio uvurugaji zaidi na hii ni kwa sababu inawezekana kwa kiasi kikubwa Liverpool ikaendelea kuwa na Can, Lucas, Milner. Viungo watatu ambao hawana ubunifu mkubwa

4. Mpatie mpira Juan Mata

Ukiwa na Juan Mata unakuwa na uhakika wa mchezaji ambaye atapeleka mpira sehemu sahihi kila muda anapoupata. Anajua kucheza ‘big games’, na ataipa kwa kiasi kikubwa muunganiko United kwa kila mchezaji kitu ambacho bado united wanakikosa kutokana na namna yao ya kujipanga na kucheza.

5. Depay upo wapi?

Wakati wengi wakilaumu uwezo wa Wayne Rooney na wachabuzi wengi wakilisema hilo, kwangu ni tofauti, Depay anatakiwa athibitishe thamani yake. Ligi ya Uingereza sio rafiki kama utakumbana na ukame wa magoli kwa zaidi ya michezo 6, vyombo vyao vya habari haviwapendi wageni sana. Kuna kitu kinaitwa individual brilliance (uwezo binafsi) hapa ndipo depay anatakiwa atuonyeshe wapi alipo, funga au tengeneza nafasi wakati ambao timu yako inacheza bila nidhamu. Na Liverpool inacheza kwa wembamba sana hivyo kuacha nafasi pembeni na baada ya Chamberlain na Lanzini kuonesha udhaifu huo ni wakati wa United kuutumia.

LIVERPOOL 

1. Gegenpressing 

Manchester bado haina muunganiko kati ya kiungo cha kukaba na ushambuliaji na ndio maana sio haba kuona wana rekodi nzuri katika beki. Muda huu ambao hawajatulia jambo sahihi ni kufanya kitu kinachoitwa counter pressing au gegenpressing katika lugha ya kitaalamu ya mpira. Hapa maana yake ni kuwawahi katika eneo lao kabla hawajasogeza mpira mbele, hapo unaweza ukashinda mipira na kuwasukumakatika eneo lao kwa sababu wanapenda kumiliki mpira.

2. Mpe nafasi Danny Ings

Muanzishe Ings acheze na Smalling, anajua kucheza na mpira ukiwa au usipokuwepo miguuni kwake (on and off the ball). Hii itamfanya Benteke kumpa wakati mgumu Blind ambaye kimsingi ni kiraka tu, na kwa rekodi yao Benteke atakuwa na advantage/kipaumbele. Atashinda mipira mingi ya juu ambayo ikidondoka Ings atatakiwa aipokee ili kuweza kuunganisha upacha wa ushambuliaji. Kwa dakika chache alizocheza dhidi ya West Ham Ings alionyesha ana pipa lenye hifadhi ya maji kuinywesha Liverpool pindi ikiwa na kiu. Kuna Muda nawaza anaweza kupata magoli mengi kwa staili ya Liverpool kuliko atakavyokuwa au kwa ukaribu na Benteke na pia Benteke anaweza kuwa sababu muhimu ya kupatikana magoli hayo kama watacheza pamoja.

3. Free Role?

Mwachie Firmino jukumu la free role. Huyu atachukua muda sana kama ataendelea kuwekwa apambane pembeni huko. Maana hajazoea kucheza bila nafasi au na changamoto ya vurugu za mwili. Kwa dakika chache alizocheza ndio mchezaji aliyetengeneza nafasi nyingi zaidi, hii inaweza kukuonyesha ni mchezaji wa aina gani. Liverpool itahitaji kupata mtu wa kupiga kutokea mbali na kukosekana Coutinho, Firmino ndio mwanaume wa kazi hiyo.

4. Cheza kamari sahihi

Brendan Rodgers anaweza kuamua kumuacha Lovren kwa maana atataka kuaminisha watu kuwa atarudi fiti baada ya kosa dhidi ya West ham lakini inabidi akumbuke kuwa, Rooney hata kama hajawa na msimu mzuri lakini huyu anahitaji beki mmoja atakayefanya makosa arudishe kujiamini/confidence yake. Lakini pia hata Sakho hii inaweza kuwa mechi kubwa kutokana na kukosa kitu kinaitwa game time. Hivyo hapa inahitajika kamari sahihi sana na kamari hii ndio inaweza kuamua mchezo. Lakini kwa roho yangu Sakho angeanza mchezo huu, pengine kama Rooney anaweza asiwe fiti, Martial ambaye ni mnyumbulifu atahitaji mtu ambaye akili yake ipo mchezoni muda wote na anaweza kufanya physical battle.

5. Brendan Rodgers na dakika 45

Huyu ni mgonjwa wa kitu kimoja, hajawahi kuwa kocha mzuri katika mabadiliko/substitutions. Kikosi chake sahihi huwa ni kile kinachoanza, hata kama kitazidiwa mara nyingi hata kosa lake la mwanzo huwa sahihi kuliko pale atakapofanya mabadiliko. Kwa ufinyu wa kikosi kutokana na majeraha anatakiwa kuwa makini sana. Mabadiliko yake yanatakiwa kuwa na tija vinginevyo nina kila hisia mechi inaweza kumalizika kipindi cha pili.

CHAGUO LANGU LA MECHI

United Man of the Match: Mata/Smalling *Depay

United Flop of the Math: Blind

Liverpool man of the Match: Benteke/Firmino*Ings

Flop of the Match: Emre Can

Niliowawekea nyota wanaweza kuwa ingizo katika eneo lolote hapo kwa maana pia wataathiri mchezo.

Utabiri 

Kutakuwa na magoli mawili au Zaidi

Kutakuwa na penalty na kadi nyekundu

Goli kutoka kwa beki.

Ahsanteni 

Usisahau kuniffollow Instagram kwenye @Nicas_Coutinho


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>