Real Madrid wametangaza kwamba watakata rufaa juu ya kifungo cha kusajili katika vipindi viwili vijavyo vya usajili walichopewa na FIFA jana Alhamisi, kutokana na kusajili wachezaji walio chini ya umri.
Kama ilivyokuwa kwa Barcelona mwaka 2015, Real Madrid na Atletico Madrid walikutwa na hatia ya kusajili wachezaji walio chini ya umri unaoruhusiwa na matokeo yake wamepigwa marufuku kusajili mchezaji au kuuza kwa kipindi cha vipindi viwili vijavyo.
Kwa upande wa Real Madrid wenyewe watalipa kiasi cha Euro 300,000 kama faini.
Hata hivyo Real Madrid wanaweza kusajili wachezaji lakini hatoweza kucheza mpaka muda wa kifungo uishe, itakuwa kama ilivyokuwa kwa Arda Turan, ambaye alisajiliwa na Barcelona msimu uliopita, lakini ilibidi kusubiri mpaka kipindi cha kifungo chao kiishe.
Katika upande mwingine imefahamika kwamba watoto wanne wa kocha wa Madrid, Zinedine ZIDANE walikuwa wamejumuhishwa katika listi ya FIFA ya wachezaji waliosajiliwa kinyume na sheria na Real Madrid.
Enzo, Luca, Theo na Elyaz wote wanaitumikia Madrid katika ngazi tofauti ya vikosi vya klabu hiyo. Enzo tayari anaitumikia kikosi alichokuwa anafundisha baba yake cha Real Madrid B (Castilla).
Luca Zidane, ni golikipa anayeripotiwa kuwa na kipaji kikubwa, yeye pia ametajwa kwa kina kwenye ripoti ya FIFA ambayo imezua maswali. Alizaliwa jijini Marseille mnamo mwaka 1998, akaenda Madrid akiwa na miaka 4 wakati baba yake aliposajiliwa na Madrid mwaka 2001. Alianza kuitumikia Madrid akiwa na miaka 6.
Sio tu kwamba watoto wa Zidane sheria inawaruhusu kutokana na baba yao kuishi Spain, lakini pia mama yao ana uraia wa Hispania.
Real Madrid sasa wanaamini kwamba kuhusishwa kwa watoto wanne kwenye listi ya FIFA inawapa wao nafasi ya kukata rufaa, kwa sababu hawakufanya makosa kuwasajili watoto hao wanne wa ZIZOU.
Jambo hilo pia limetokea kwa mdogo wake Ezequiel Garay, mlinzi wa zamani wa Real Madrid, ambaye sasa anaitumikia Zenit St Petresburg, mdogo wake nae amehusishwa kwenye listi ya wachezaji walisajiliwa kinyume cha sheria na FIFA, Real Madrid wanaamini kwamba hawakuvunja sheria kumsajili mchezaji huyo mbele ya sheria za FIFA.
SHERIA NAMBA 19 YA FIFA INAYOHUSU USAJILI WA WACHEZAJI WALIOCHINI YA UMRI