VILABU mahasimu wa jiji la Madrid, nchini Hispania – Real Madrid and Atlético Madrid wamekumbana na adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji wapya kwa kipindi cha vipindi viwili vijavyo vya dirisha la usajili barani ulaya.
Jambo hili limezua maswali mengi juu ya vitu wanavyoweza kufanya na ambavyo hawaruhusiwi kufanya kutokana na adhabu hiyo waliyopewa.
Kutokana na mkanganyiko huo, hapa nitaweka wazi vitu vinaruhusiwa na visivyoruhusiwa kisheria wakati Madrid na Atletico watakapoanza kuitumikia adhabu yao.
1. Je wanaweza kuwarudisha wachezaji waliopo Kwenye timu nyingine kwa Mkopo?
Yes. Real Madrid na Atlético wanaweza kuwaita wachezaji wao waliopo kwa mkopo katika vilabu vingine – lakini suala hili lisihusishe mabadilishano ya fedha baina ya vilabu.
2. Je wanaruhusiwa kuuza wachezaji?
Yes, kifungo hakiwazuii Real Madrid au Atlético kuuza wachezaji wao.
3. Kifungo hiki kitawazuia makocha kubadilishwa au kuhamia timu nyingine?
No, makocha hawahusiki na adhabu ya FIFA. Real na Atletico wanaweza kufanya mabadiliko ya makocha muda wowote wanaojisikia kufanya hivyo.
4. Je wataruhusiwa kuingiza wachezaji wa kutoka zao kikosi B?
Yes, adhabu ya FIFA haivizuii vilabu hivyo viwili kuingiza wachezaji wao wa vikosi vya pili ili kuimarisha timu zao.
5. Wachezaji(Watoto) waliohusika na usajili uliopelekea adhabu hii wataruhusiwa kucheza?
Vilabu vikianza kuitumikia rasmi adhabu hii, watoto waliosajiliwa na Vilabu hivi viwili mpaka kupelekea timu hizi kufunguwa, hawatoruhusiwa kutumika mpaka watakapofikisha miaka 18.
6. Ikiwa rufaa za vikabu zikafeli na kesi zikaenda mahakama ya CAS, Je vilabu vinaweza kusaini wachezaji dirisha lijalo la usajili?
Sheria itawaruhusu vilabu hivyo kuendelea kusajili mpaka adhabu itakapoanza kutumika rasmi. Ikiwa kesi zitaenda mpaka CAS basi kuna uwezekano mkubwa mpaka kufikia June 2016, maamuzi rasmi yatakuwa hayajafanyika. Hili pia lilitokea kwa Barcelona – walikata rufaa na kesi ikaendelea mpaka wakati wa usajili ulipofika wakafanikiwa kuwasaji Luis Suarez na Ivan Rakitic.