Licha ya kumsifia sana Sir Alex Fergie ambae ni kocha mwenye mafanikio ndani ya Manchester united, lakini Klopp ametoa siri yake kubwa kwamba hakuwa na interest na Manchester united licha ya manager Fergie kuwahi kumcheki kipindi flani kwa ajili ya kazi ya United.
Klopp akimzungumzia SAF alisema, “Nina heshima kubwa sana na Sir Alex na niliongea nae kidogo tu lakini kwangu ilikua ni kikubwa sana. Yeye ni legend na ni kama John Lennon of football managers”. John Lenon ni mwanamuziki aliyepata mafanikio makubwa na alizaliwa Liverpool Englanda. Kikubwa zaidi alikua ni mmoja kati ya waanzilishi wakubwa wa bendi maarufu ya The Beatles
Akitoa story yake ya kutaka kuwa manager wa Manchester united miaka kadhaa iliyopita alisema, “Sikupata ofa kamili ya mimi kuja Manchester United lakini habari hizo zilinifikia kwa karibu. Kwa kipindi kile kama ningepata ofa ya kuja Manchester ningekataa bila kupindisha maneno kwasababu nilikua na malengo na majukumu yangu na Borussia na bado sikuyamaliza. Hivyo basi kama wangenipa nisingeikubali. Lakini pia nilipata simu ya Sir Alex Fergie labda kwenye maongezi yatu alijua dhahiri kwamba sikua tayari kwenda United kwa wakati ule ndio maana hata ofa haikutumwa.”
Mashabiki wa Manchester united, imagine that Jurgen Klopp angekua kocha wenu sasa hivi. Je, maisha yangekuaje?. English premier league inaoneka Live and exclusive kwenye Dstv.