Uongozi wa klabu ya Chelsea umemfukuza kazi mfanyakazi wa uwanja wao baada ya mfanyakazi huyo kumkejeli nahodha wa zamani wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas kwa kumwita ‘snake’.
Video ya tukio hilo lililotokea kwenye uwanja wa Stamford Bridge mwanzoni mwa msimu huu imeonekana mtandaoni siku ya Ijumaa na klabu ya Chelsea imethibitisha kuchukua hatua dhidi ya mfanyakazi huyo.
‘You’re a snake, you’re Arsenal, what happened to you?’ mfanyakazi huyo ameonekana na kusikika akimwambia maneno hayo kiungo huyo wa Hispania kupitia video fupi ya sekunde nane ambayo imeenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
Mshindi huyo wa kombe la dunia atakutana na klabu yake ya zamani siku ya Jumapili wakati Chelsea itakapokuwa ikiumana na Arsenal kwenye mhezo wa ligi.
Fabregas, 28, alifanikiwa kucheza mechi 503 akiwa na the Gunners baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea academy ya Barcelona mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 15.
Alipewa unahodha ndani ya Arsenal klaba ya kuamua kutimkia kwenye klabu yake ya utotoni kipindi cha majira ya joto mwaka 2011.
Baada ya kujikuta kwenye wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi ha Barcelona, mwaka 2014 aliamua kujiunga na Chelea ambao ni wapinzani wa jadi wa Arsenal.
Alikuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Jose Mourinho kilichotwaa taji la ligi msimu uliopita akifanikiwa kucheza mechi 47 kwenye michuano yote.
Kiwango chake kimeshuka msimu huu na amekuwa akikosolewa na mashabiki wa Stamford Bridge kutokana na kutimuliwa kwa Mourinho December mwaka jana.