Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

ACACIA YAMWAGA MAMILIONI YA PESA KWA TIMU YA DARAJA LA PILI

$
0
0
Meneja wa Buzwagi Assa Mwaipopo akimpa hundi katibu wa Ambasador
Meneja wa Buzwagi Assa Mwaipopo (kushoto) akimpa hundi katibu wa Ambasador

Na. Philipo Chimi, Kahama

Timu ya Ambasador FC kutoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga inayoshiriki lig daraja la pili ngazi ya mkoa, jana imepokea  hundi ya udhamini wa shilingi milioni 10.5 kutoka katika kampuni ya uchimbaji wa madini ACACIA kupitia mgodi wake wa Buzwagi uliopo  wilayani Kahama.

Akizungumza jana katika zoezi hilo la kukabidhi hundi kwa timu ya Ambasdor ambalo lilifanyika katika viwanja vya mgodi huo, Meneja wa mgodi wa Buzwagi Assa Mwaipopo alianza kwa kuwapongeza viongozi na wachezaji wa timu ya Ambasador kwa kufikia hatua hiyo na kuwasihi waimarishe uongozi ili kuijenga timu yao kutokana na timu nyingi za Tanznaia zikipata udhamini kila kiongozi hujali masilahi yake na siyo masilahi ya timu.

Meneja akisalimiana na Karume Songoro mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye ni kocha wa Ambasador
Meneja akisalimiana na Karume Songoro mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye ni kocha wa Ambasador

“Hongereni sana kwa hatua mliyofikia maana nimeongea na katibu wenu amesema tayari mmefuzu kucheza fainali mkoani, hiyo ni hatua nzuri ila kunajambo nataka kuwasihi kwamba viongozi kuweni makini katika kuongoza timu yenu na mjitoe kuisadia timu na siyo kufanya kazi kwa maslahi yenu kwakuwa timu imepata fedha”, alisema meneja.

Lakini pia meneja Mwaipopo alitoa ufafanuzi juu ya lengo na dhumuni la kutoa msaada kwa timu hiyo ambayo ipo katika wilaya ya Kahama ambapo mgodi huo unafanya kazi.

Wachezaji wa Ambasador wameshika hundi
Wachezaji wa Ambasador wameshika hundi

“Lengo letu kubwa la kutoa udhamini huu ni kutaka kuisaidia timu hii likiwa ni lengo la kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia jamii inayotuzunguka, kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya Stand Utd ya Ligi kuu na sasa tumetoa udhamini huu wa vifaa pamoja na fedha ili kuisaidia timu hii ifike mbali maana inafanya vizuri sana”, alisema meneja.

Katibu mkuu wa timu ya Ambasador Bakari Khalid aliyezungumza kwa niaba ya mkurungezi wa timu hiyo Aray Abei alitoa shukurani zake kwa kampuni hiyo ya ACACIA Buzwagi baada ya kupewa masaada huo.

Katibu wa timu ya Ambasador
Katibu wa timu ya Ambasador

“Kwanza naomba nitoe shukurani zangu za dhati kwa meneja wa mgodi wa Buzwagi na uongozi mzima kwa kupokea ombi letu kwaajili ya kutupa msaada huu, naomba kuwaahidi kwamba sisi kama Ambasador lilivyojina letu ni mabalozi tutahakikisha tunaitangaza Kahama na ACACIA katika sekta ya michezo kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa kucheza mpira na pia tunakuza vipaji vya vijana wetu wa Kahama, hivyo nawaahidi kuwa tutapanda daraja msimu huu na pia msiache kutusaidia tena tukija kuomba msaada wenu asanteni sana”, alisema Bakari.

philipo na meneja

Timu ya Ambasador FC inayofundishwa na nguli wa zamani katika soka la Tanzania aliyewika katika vilabu vya Kahama UTD ya Kahama, Pamba ya Mwanza, Moro Utd ya Morogoro, klabu ya Yanga ya Dar es salaam na hata katika timu ya taiafa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Karume Songoro, ilipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya ACACIA Buzwagi na sasa inajiandaa na fainali ya michuano hiyo ya lig daraja la pili mkoa inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni .


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>