Wanandoa Coleen na Wayne Rooney wametangaza kupata mtoto wao wa 3 leo jumapili.
Rooney na Coleen kwa pamoja walitumia akaunti zao za mtandao wa Twitter kuwaambia mashabiki wao juu ya taarifa hiyo, wakiandika: ‘Our gorgeous little boy arrived today. Kit Joseph Rooney. 8Ib 1oz. We are over the moon.’
Jana, Rooney alitoa ishara kwamba mkewe anakaribia kujifungua, baada ya kupost picha ya zamani iliyokuwa akimuonyesha akiwa na mtoto wake wa pili Klay muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Rooney aliandika: ‘#TBT – Picha ya familia baada ya Klay kuzaliwa. Sio muda mrefu kabla mtoto mwingine ajaongezeka kwenye familia.’ #Family.’
Mtoto wa Kwanza wa Rooney na Coleen, alipewa jina Kai, aliyemfuatia akapewa jina la Klay na sasa watatu kapewa jina la Kit.