Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Hii Ndio Rekodi Muhimu ya Flamini Iliyovunjwa na Diego Costa 

$
0
0

Mathieu Flamini alikuwa ni mmoja ya wachezaji waliochezea Arsenal leo wakati Gunners walipofungwa 1-0 na Chelsea katika mchezo wa raundi ya pili ya English Premier League katika dimba la Emirates.

  Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa mara nyingine alionyesha mchezo usiokuwa na nidhamu katika safu ya kiungo ya Arsenal, kitu kilichopelekea kusemwa sana na mashabiki wa timu hiyo.

Pia, Flamini alikuwa na nafasi nzuri ya kubadili matokeo mwishoni mwa kipindi cha kwanza wakati alipofeli kuitumia nafasi nzuri ya kufunga wakati timu ikiwa nyuma kwa goli 1-0, na matokeo mashabiki wengi wa timu wakaonekana kutokuridhishwa kwa kiwango cha mchezaji huyo na kuendelea na maombi ya kumuombea Francis Coquelin apone haraka, ili kuiongezea uwezo timu yao.

  Lakini pamoja na matokeo mabaya kwa Gunners, Flamini pia amepoteza rekodi yake nzuri ya kujivunia na Arsenal katika uwanja wa Emirates.
Kabla ya mchezo wa leo, Flamini alikuwa na rekodi ya kutopoteza mechi yoyote katika uwanja huo akiwa mchezaji wa Arsenal – akiwa amecheza mechi  54, akipata ushindi katika mechi 37, na sare 16 huku akiwa hajapoteza.

 
Lakini goli la Diego Costa la leo limepelekea Flamini kupoteza rekodi yake ya kutokupoteza mechi Emirates.  


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles