Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

WENGER ALICHEMKA KUMTOA GIROUD DHIDI YA CHELSEA?

$
0
0

Olivier

Kocha Arsene Wenger alimtoa mshambuliaji wake Oliver Giroud katika dakika ya 22 ya mchezo na kumuingiza beki Gabriel Paulista ili kuziba nafasi sehemu iliyoachwa wazi na beki Paul Mertesacker ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 18 ya mchezo mara baada ya kucheza faulo ya ‘kiueledi’ dhidi ya Diego Costa wa Chelsea.

Lakini sub hiyo ya kumtoa mshambuliaji wa kati Oliver Giroud imekosolewa na wachambuzi mbalimbali wa soka nchini England wakiwemo gwiji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry na kiungo wa zamani wa Tottenham Hotspur Jermain Jenas.

Jenas amesema kuwa hajawahi kuona substitution kama hiyo aliyoifanya Arsene Wenger ya kumtoa mshambuliaji na badala yake anasema Wenger alitakiwa kumtoa mchezaji ‘luxury’ uwanjani na kumuacha Oliver Giroud ambaye pia ilikua muhimu kwa Giroud kubakia uwanjani kwa faida ya urefu wake hasa ikizingatiwa kuwa Per Mertesacker aliyeoneshwa kadi nyekundu, ndiye aliyekua mchezaji mrefu zaidi kwa upande wa Arsenal.

Aidha, Jenas anasema ingekua kitu kizuri kwa Arsenal kumtoa Joel Campbell ama Mesut Ozil, huku akisema kuwa Alexis Sanchez alikua ni faida nyingine nje ya kiwanja.

Thierry na Jenas wote ni wachambuzi wa soka nchini England wakifanya uchambuzi katika kituo cha televisheni ya Sky Sports nchini humo, na wamekua wakiwavutia mashabiki duniani kote kutokana na ueledi wao katika uchambuzi huo wa soka.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles