Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

AZAM YATOA DOZI FA CUP

$
0
0
Farid Musa (kulia) akichuana na Wiliam Otong wa African Lyon
Farid Musa (kulia) akichuana na Wiliam Otong wa Africa Lyon

Timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara bado zimeendelea kutoa dozi kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya leo Azam FC kutoa kichapo cha magoli 4-0 kwa Africa Lyon FC mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Golikipa wa African Lyon Hamad Juma akiondosha mpira kwenye eneo la hatari mbele ya Ame Ally
Golikipa wa African Lyon Hamad Juma akiondosha mpira kwenye eneo la hatari mbele ya Ame Ally

Magoli ya Azam FC yamefungwa na Mudathir Yahya aliyefunga bao la kwanza dakika ya kwanza ya mchezo kisha Farid Musa akapachika bao mbili wavuni dakika ya 8 na 37 kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko huku Azam wakiwa mbele kwa bao 3-0 dhidi ya Africa Lyon.

Nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Boco 'Adebayor' akitia krosi langoni mwa African Lyon
Nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Boco ‘Adebayor’ akitia krosi langoni mwa Africa Lyon

Kipindi cha pili Azam waliendeleza kisago kwa Africa Lyon baada ya Ame Ally kuifungia timu yake bao la nne na kukamilisha ushindi wa Azam kwenye mchezo huo.

Shomari Kapombe wa Azam FC (katikati) akiwa amekusanya 'kijiji' cha African Lyon akitmea nacho
Shomari Kapombe wa Azam FC (katikati) akiwa amekusanya ‘kijiji’ cha Africa Lyon akitmea nacho

Azam inaungana na timu nyingine  kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora kwenye michuano ya FA ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.

Wiliam Otong wa African Lyon (kushoto) akimkabili Farid Musa wa Azam FC
Wiliam Otong wa Africa Lyon (kushoto) akimkabili Farid Musa wa Azam FC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>