Baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi cha goli 7-0 kutoka kwa FC Barcelona kocha wa Valencia Garry Neville amewaambia waandishi wa Habari kuwa hafikirii kujiuzuru na ataendelea kuwa kocha wa Valencia mpaka pale mkataba wake utakapoisha.
Valencia ilipokea kichapo hicho cha goli 7-0 jana katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano ya Copa del Rey huku magoli ya Barcelona yakifungwa na na Luis Suarez aliyefunga magoli manne na Lionel Messi aliyefunga magoli matatu
Valencia hawajashinda mchezo wowote kati ya michezo nane waliyocheza La Liga na Neville alipoulizwa kuhusu mustakabali wake katika timu alijibu kifupi “hapana” alipoulizwa kama anahofu ya kufukuzwa alijibu “swali linalofuata”.
“Ilikuwa ni moja ya matokeo mabaya kuwahi kutokea katika maisha yangu ya soka kama mchezaji lakini pia kama meneja, Tulifanya makosa mengi sana ambayo huwezi ukayafanya dhidi ya timu kama hii’, Garry Neville.
Kwa matokeo hayo Garry Neville na timu yake ya Valencia wana kibarua kizito cha kuifunga Fc Barcelona magoli 8-0 katika nusu fainali ya pili ili kutinga fainali ya Copa Del Rey.