Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amekubali kuwa klabu yake ipo katika wakati mgumu katika mbio za kunyakua ubingwa wa England.
Kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya na gazeti la Daily mail la nchini England Wenger amesema: “Tutaona mwisho wa msimu huu. Nimapema sana kusema hivyo”.
“Ni wazi tumekuwa na mwaka mbaya hasa kuanzia ile mechi ya kwanza dhidi ya Liverpool na ile mechi dhidi ya Stoke ambayo kimsingi tumekuwa na tofauti kubwa sana katika michezo yetu miwili”, alisema Wenger.
Kuhusu suala la usajili wa mshambuliaji ambalo ndiyo lilionekana ni pengo kubwa katika safu ya ushambualiaji wa timu hiyo Mfaransa huyo amesema washambuliaji hawatafutwi mtaani bali kila mshambuliaji mkubwa ni kwenye timu yake na ana mkataba kwahiyo hawakuwepo sokoni.