Wiki iliyopita Jose Mourinho aliumia kwa mara nyingine ila kipindi hiki aliumizwa kwa staili ya aina yake baada ya mwanaume mmoja ambaye ukimtazama kwa haraka haraka unaweza kudhani jamaa ana ulemavu wa ngozi japokuwa yeye ni Mzungu. Baada ya kupiga magoli 3 dhidi ya Chelsea pale Godson Park, Steven Naismith ameonekana kuwa gumzo sana mitaani. Leo hii nimekuwekea vitu adimu ambavyo pengine hukuwahi kuzani kuhusu mchezaji huyu hatari.
Steven John Naismith ni mzaliwa wa Scotland na mchezaji wa zamani wa Rangers, kwa sasa ana miaka 29. Ana asili ya Uingereza na Wales japokuwa ni Mscotland
Ni mchezaji wa kwanza kuifunga Chelsea ‘hat-trick’ ikiwa chini ya Jose Mourinho. Steven Naismith pia ni amekuwa mchezaji wa kwanza kumfunga Mourinho mara tatu katika michezo tofauti.
Naismith ana uwezo wa kucheza nafasi mbili uwanjani, moja ni kama kiungo mshabuliaji na nyingine ni kama namba 9 (Center Foward).
Akiwa kwenye klabu ya Kilmarnock mwaka 2005 alichukua tuzo ya mchezajin bora chipukizi wa mwaka kwenye ligi kuu ya Scotland. Mwaka mmoja baadae pia alitwaa tuzo ya mwaka (PFA)
Licha ya kuionea Chelsea mara kwa mara, ni vigumu kuamini kwamba huyu jamaa alisajiliwa bure na Everton.
Ni mchezaji wa pili kufunga ‘hattrick’ dhidi ya Chelsea kwenye EPL tangu Robin Van Persie afanye hivo mwaka 2011. Mama yake Steven Naismith anafanya kazi supermarket.
Goli lake la kwanza akiwa Everton aliwafunga Liverpool mwezi October 2012 pale Godson Park. Mchezo huo uliisha kwa sare ya 2-2.
Sio mara ya kwanza kuionea Chelsea kwani asilimia 33 ya magoli yake kwenye EPL yanatokea kwenye vipigo anavyowapa Chelsea.
Pia ‘hat trick’ ya msimu huu aliowafunga Chelsea alitumia miguu yote, wa kulia na kushoto pamoja na kichwa kufunga magoli yote.
Wales ilimuomba Naismith aichezee timu yao ya taifa ila jamaa aligoma na kucheza Scotland.
Mbali na uwezo wake wa kucheza kama kiungo na mshambuliaji, pia Naismith alipokuwa Rangers aliweza kutumika kama winga wa kushoto na kulia.
Naismith alisajiliwa na Rangers mwezi August mwaka 2007 zikiwa zimesalia sekunde 19 kabla ya dirisha kufungwa. Kumbuka alitokea Kilmarnock kwa ada ya £1.9m