Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MAGULI ACHA KULIA, KOMAA UFANYE KAZI YAKO

$
0
0
Elias Maguri (kushoto) mchezaji wa Stand United ya Shinyanga
Elias Maguri (kushoto) mchezaji wa Stand United ya Shinyanga

Na Baraka Mbolembole

Straika wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Elius Maguli alianza msimu huu kwa kasi kubwa katika ufungaji lakini tangu mzunguko wa tisa mshambulizi huyo wa Stand United ya Shinyanga hajafanikiwa kufunga goli lolote.

Katika michezo 9 ya mwanzo ya msimu, Maguli alifunga magoli 9 na kushikilia chati ya wafungaji katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kiwango chake hicho kilimfanya kocha wa Stars, Charles Boniface Mkwassa kumjumuhisha katika kikosi ambacho kilicheza na Algeria katika michezo miwili ya mtoano kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia, 2018-Kanda ya Afrika.

Alifunga goli la kuongoza katika sare ya 2-2 jijini Dar es Salaam. Baada ya Stars kutolewa kwa jumla ya magoli 9-2 na ‘Mbwa mwitu wa Jangwani’ mwezi Novemba mwaka uliopita, kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) Abdallah ‘King’ Kibadeni alimjumuhisha, Maguli katika kikosi chake kilichotolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Challenge iliyofanyika nchini Ethiopia.

Maguli alifunga magoli mawili katika michuano hiyo. Kiwango chake kati ya August-November, 2015 kilikuwa juu. Alitawala vyombo vya habari na kuibeba timu yake katika ligi. Al Ahly ya Misri ilimpa nafasi ya kufanya majaribio mshambuliaji huyo. Inasemekana mchezaji huyo hakukidhi viwango vilivyotakiwa hivyo alishindwa kuwavutia Wamisri hao.

“Baadaya kurudi kwenye mapumziko ndoto zangu zilianza kufifia kwani ilitokea kutoelewana na mwalimu wangu na kufikia hatua ya kutonipa nafasi ya kucheza. Viongozi pamoja na kocha walikuwa wanaifahamu safari yangu ya Misri, waliniruhusu. Si peke yangu ni wachezaji wengi wanalalamikia hilo na wamekuwa wakiulizwa kwanini hatuchezi”, ni sehemu ya maneno ya Maguli akielezea kwanini hapati nafasi.

Maguli anapaswa ajizungumzie yeye kwanza ni kwanini hachezi. Amepoteza makali, amekuwa mzito zaidi. Kama atajibidiisha tena sina shaka kuwa kocha Mfaransa, Patrick Liewig atampa nafasi kwa mara nyingine lakini kama ataendelea kuzunguka katika vyombo vya habari na kusema kuwa haelewani na kocha wake hakina maana.

Liewig si kocha muoga wala si mtu anayepapatikia majina makubwa zaidi ya uwezo wa mchezaji katika wakati husika.

Kweli aliisaidia sana Stand kupanda katika nafasi 5 za juu katika ligi lakini alipewa nafasi  baada ya kuonyesha uwezo mazoezini lakini baada ya kuwa nje ya timu kwa siku zisizopungua 20 huku kocha akiwa katika programu zake na wachezaji wengine ni sababu ya kwanza ambayo ilimnyima nafasi ya kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza.

Alichopaswa kufanya ni kufanya mazoezi kwa nguvu, ikiwezekana mazoezi binafsi ya ziada ili aendane na kasi aliyoikuta kwa wenzake. Lakini inaonekana wazi kuwa Maguli akijenga ‘chuki’ na kuweka imani mbaya kwa Liewig na kumchukulia kama kikwazo cha kutimiza malengo yake ya kuwa mfungaji bora msimu huu ataendelea kukwama.

Alikosea, kwa maana katika timu kwanza ni kuhakikisha malengo ya pamoja yanatimia na si yale ya mchezaji mmoja mmoja. Maguli haujachelewa, licha ya kwamba amepitwa magoli 7 na kiongozi wa chati hiyo, Mganda, Hamis Kizza ambaye tayari amekwisha funga magoli 16 hadi sasa.

Maguli aache kulia kwamba kutoelewana kwake na Liewig ndiyo sababu ya kukosa nafasi katika timu yake, anachotakiwa kufanya ni kukomaa kwa kujituma na kupiga mazoezi ya maana ili awe mwepesi na kurejea kwenye form yake ya awali.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>