Silvio Berlusconi ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani wa Italia ameweka wazi kuwa ametumia pauni bilioni 1 katika kipindi chake cha urais katika klabu yake ya AC Milan ya Italia.
“Kama nitajiwekea mwenyewe maksi kwenye 10/10, basi nitajiwekea 11. Imekuwa miaka 30 ya maajabu. Tumeshinda kuliko yeyote yule. Tumepata mashabiki wapya milioni 363 dunia nzima. Zaidi ya yote,mapenzi yetu kwa ajili ya Milan yamelipa na kutufanya kuwa na furaha kubwa.”
Kati ya sajili za kukumbwa San Siro zilizowahi kufanywa na Berlusconi ni wakati alipofanya usajili wa rekodi ya dunia kwa kumsaini staa wa zamani wa Holland, Ruud Gullit kutoka PSV Eindhoven kwa ada ya pauni milioni 5.6, na pauni nyingine milioni 13 kwa winga.
Mtaliam, Gianluigi Lentini kutoka timu ya Torino. Manuel Rui Costa ndiye mchezaji ghali zaidi klabuni Milan. Berlusconi alilipa pauni milioni 34 kwa Fiorentina mwaka 2001 ili kupata huduma ya kiungo huyo ‘maestro’ wa zamani raia wa Ureno.
Mholland, Marco van Basteni aligharimu mamilioni ya pauni wakati aliposajiliwa na Milan mwaka 1987. Van Basten ni kati ya sajili za mwanzo ghali katika utawala wa Berluscon. Fillipo Inzaghi ‘Super Pippo’ ndiye mchezaji ghali zaidi wa pili katika historia ya Milan.
Mtaliano huyo alimgharimu Berluscon pauni milioni 29.7 ili kumuhamisha Juventus mwaka 2001. Beki wa kati na mmoja kati ya mabeki mahiri kuwahi kutokea duniani alisajiliwa na Milan akitokea SS Lazio kwa ada ya pauni milioni 24.2 mwaka 2002.
Nesta ndiye mchezaji wa tatu klabuni hapo. Ronaldinho Gaucho, Alberto Gilardino kila mmoja alisajiliwa kwa pauni milioni 19.5 katika nyakati tofauti kutoka klabu za FC Barcelona na Parma. Hao ni baadhi tu ya wachezaji waliosaidia kupatikana kwa mataji matano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka 30 ya urais wa Berlusconi katika timu ya AC Milan. Berlusconi pia ndiye mmiliki wa klabu hiyo.