Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MWAMBUSI: TUNAJENGA TIMU MPYA

$
0
0
 Juma Mwambusi Kocha wa Mbeya City FC ya jijini Mbeya

Juma Mwambusi Kocha wa Mbeya City FC ya jijini Mbeya

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Mbeya City FC, Juma Mwambsi amefurahishwa na kiwango cha wachezaji wake mara baada ya kuifunga JKT Ruvu ya Pwani, Jumatano hii katika uwanja wa Sokoine, Mbeya. City ilipoteza kwa goli 1-0 mbele ya Kagera Sugar katika mchezo wa ufunguzi Jumamosi iliyopita katika uwanja wa nyumbani lakini wameisambaratisha JKT Ruvu katika namna iliyomfanya mwalimu wa timu hiyo kusema ‘vijana wake wamepambana kiume’.

“Tulishapoteza mechi ya kwanza nyumbani, hatukutaka kupoteza nyingine” anasema Mwambusi mwalimu wa zamani wa Tanzania Prisons” Wachezaji wametupa matokeo tuliyotarajia, nachoweza kusema nawapongeza wachezaji wangu. Wameweza kupambana kiume tumepata pointi 3″. City itacheza na mahasimu wao wa jiji la Mbeya, Tanzania Prisons siku ya Jumamosi, huo utakuwa ni mchezo wa kwanza wa mahasimu mji mmoja msimu huu.

“Mbeya City ni kama timu mpya, tulipoteza wachezaji wasiopungua 11 wa kikosi cha kwanza wakati wa usajili uliopita, hivyo kama mwalimu naendelea kutafuta uwiano ulio sawa kiuchezaji, kimwili na kiakili kati ya wachezaji wapya na wale waliokuwepo. Tutaendelea kufanyia kazi mapungufu yetu ili kuendelea kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>