Haikuwa mara ya kwanza kwa Leicester City msimu huu, Jumamosi ya March 5, 2016 ilikuwa ni super day kwa upande wao.
Hiyo ni baada ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa EPL kutoka sare ya kufungana bao 2-2. Tottenham na Arsenal wamejikuta wakitoa mwanya mwngine kwa Leicester kuongeza wigo wa pointi baada ya kumalizika kwa mchezo wa London derby huku vijana wa Ranieri wakiikuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Watford.
Kikosi cha Ranieri kilipambana kwenye mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya timu ambayo imekuwa haina mfululizo wa matokeo mazuri.
Leicester ilitengeneza nafasi nzuri za kufunga wakati wa kipindi cha kwanza lakini walishinda mechi hiyo kipindi cha pili kwa goli lililopachikwa kambani na Riyad Mahrez.
Watford walijaribu kupambana kusawazisha goli hilo lakini Leicester walikuwa vizuri kwenye safu yao ya ulinzi iliyoongozwa na Kasper Schmeichel ambaye alizima mashambulizi kadhaa ya Watford.
Bado kuna kundi la mashabiki wa soka ambalo haliamini hadi sasa kwamba Leicester City wanaweza kunyakua ndoo ya EPL msimu huu.
Sasa inabidi kuthibitisha kwa data kwamba Leicester inanafasi kubwa ya kutwaa taji hilo msimu huu baada ya Chelsea ambao ndiyo watetezi kulitema tangu mwanzoni mwa msimu.
Leicester hawabanwi sana na ratiba ya ligi kwa michezo yao ijayo, bashiri nyingi zimekuwa zikiwatabiria kutwaa ubingwa.
Angalia Tweets ambazo huenda zikakufanya ukubali Leicester wanaweza wakatwaa taji la Premier League msimu huu.