Soka limetumika sana kusambaza upendo kwenye ishu ya wakimbizi wa Syria ambayo imetoka wiki chache zilizopita. Story ya mkimbizi huyu Osama Abdul Mohsen ambapo video yake ilisambaa akiwa amembeba mwanae anakimbia huku mpiga picha mmoja mwanamke akimpiga mateke na kudondoka chini.
Baada ya video hiyo kusambaa watu wakaanza kutafuta story kuhusu bwana Osama na kugundua kwamba yeye ni kocha wa level za juu nchini kwao Syria. Hapo ndipo chama cha makocha nchini Spain walimpa nafasi ya kazi.
Baadae Rais wa Real Madrid Florntino Perez alimpa mualiko kwenda kutembelea ofisi za Real Madrid akiwa na mwanae. Pia wamempa mualiko wa kwenda kuangalia mechi ya Real Madrid dhidi ya Granada.
Wakimbizi wa Syria waliingia kwenye vichwa vya habari sana wakiwa kwenye harakati zao za kujaribu kuingia nchi za Ulaya wakiwa kwenye kundi kubwa.
Angalia video jinsi mpiga picha huyo akimpiga mateke coach Osama.