Golikipa wa zamani wa klabu ya Simba SC, Abel Dhaira ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya IBV Vestmannaeyjar na timu ya taifa ya Uganda – anakabiriwa na mtihani mgumu unaoweza kuhatarisha maisha yake.
Dhaira ambaye aliitumikia Simba msimu wa 2013/14 amegundulika kuwa ana ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Golikipa huyo wa zamani wa vilabu vya Express FC, Uganda Revenue Authority na As Vita afya yake ilianza kuzorota mwanzoni mwa mwaka huu na ikapelekea kulazwa hospitali kwa mwezi na nusu jijini Kampala.
Abel Dhaira hajaichezea timu yake huko Iceland tangu mwezi October 2015 baada ya hali yake kuwa mbaya.
Abel anatarajia kuanza matibabu nchini Iceland mapema wiki ijayo.