Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano vilabu viwili vya English Premier League vinakutana kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya ulaya. Ni robo fainali ya UEFA Europa League.
Wababe wa Top 4 ya zamani ya Premier League wameshakutana mara 10 kwenye hatua za mtoano za michuano ya ulaya kuanzia mwaka 2004 mpaka 2011.
Chelsea na Arsenal walikutana mara ya kwanza – The Blues wakawafunga Gunners ‘The Invincibles’ kwenye mechi mbili ya robo fainali ya Champions League.
Mwaka mmoja uliofuatia Gunners wakakutana na Liverpool kwenye nusu fainali – mchezo wa kwanza uliowakutanisha waingereza kati ya minne ya mfululizo.
Kabla ya Liverpool kuumana na The Blues mwaka 2008, walicheza na Arsenal na kuiondoa Gunners kwenye mashindano.
Na safari ya Chelsea baada ya kuiondoa Liverpool, ikaishia kukutana na Manchester United fainali – na mashetani wekundu wakashinda.
Mwaka mmoja uliofuatia, vijana wa Sir Alex Ferguson wakawaondoa Gunners, wakati wababe hao walipokutana kwa mara ya kwanza kwenye UCL.
Miaka miwili baadae, United wakawaandoa vijana wa Carlo Ancelotti katika robo fainali.
Kuna michezo mingi ya kukumbukwa ya namna hii, lakini hii ndio michezo mitano ya kukumbukwa zaidi ya waingereza walipokutana wenyewe kwa wenyewe kwenye Champions League.
1. Robo Fainali 2003-04
Chelsea 1 Arsenal 1
Arsenal 1 Chelsea 2
Ilikuwa siri nzito iliyofichwa kwamba Claudio Ranieri angefukuzwa mwishoni mwa msimu huo – lakini alijitahidi kupambana aondoke akiwa na mafanikio.
Rekodi ya Chelsea dhidi ya Arsenal katika mechi za michuano ya ndani ilikuwa mbovu – na hivyo Gunners walipewa nafasi kubwa.
Lakini hii ilikuwa michuano ya ulaya.
Vijana wa Arsene Wenger walikuwa kwenye fomu nzuri, na walionekana kama tayari wameshaingiza mguu mmoja ndani ya nusu fainali wakati Jose Antonio Reyes alipofunga goli la kuongoza kabla ya mapunziko katika dimba la Highbury.
Hata hivyo, Frank Lampard akasawazisha dakika 6 baadae, dakika 3 kabla ya mchezo kuisha Wayne Bridge akafunga goli la ushindi na kumpa Ranieri zawadi nzuri ya kuondokea.
Nusu Fainali 2004-05
Chelsea 0 Liverpool 0
Liverpool 1 Chelsea 0
Goli la Mzimu – mechi iliyokuwa na utata zaidi baina ya vilabu vya England katika UCL.
Kikosi cha Rafa Benitez cha Liverpool kilikuwa nyuma ya Chelsea waliokuwa on fire – na walishapoteza fainali ya kombe la ligi.
Lakini ilikuwa story tofauti kabisa kwenye michuano ya ulaya.
Baada ya dakika 90 za sare @Stamford Bridge, mechi iliyofuatia pale Anfield ilipata maamuzi ndani ya sekunde 60 za kwanza za mchezo.
Luis Garcia alipiga mpira uliompita Petr Cech. William Gallas alionekana kufanikiwa kuuondoa mpira kabla haujavuka mstari wa goli, lakini mwamuzi akaweka kati.
Mpaka kufikia leo hii, Jose Mourinho ameendelea kupinga lile halikuwa goli.
Chelsea 1 Manchester United 1 aet: pens 5-6
RED DEVILS walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Premier league kutoka kwa Chelsea – na wakafanikiwa kuuchukua ubingwa wa ulaya mikononi mwao.
United waliuanza mchezo vyema kwa goli la
dakika ya 26 la Cristiano Ronaldo.
Vijana wa Sir Alex Ferguson walikuwa on fire – na kama sio ushujaa wa Cech kuokoa michomo ya Michael Carrick na Carlos Tevez mechi ingekuwa imeisha mapema.
Hata hivyo, Lampard akasawazisha mpaka kufikia mapumziko.
Chelsea wakaanza kurudisha mashambulizi katika usiku wa mvua jijini Moscow na walifanikiwa kugongesha mwamba mara mbili – lakini wakashindwa kufunga.
Didier Drogba akapewa kadi nyekundu kwa kumpiga kibao Nemanja Vidic.
Na mzigo ukahamia kwenye mikwaju ya penati.
Penati aliyokosa Ronaldo ilimpa John Terry nafasi ya kuipa timu yake ubingwa lakini akateleza na kukosa.
Edwin van Sar akaokoa mkwaju wa Nicolas Anelka na United wakashinda taji la 3 la ulaya.
Robo Fainali 2008-09
Liverpool 1 Chelsea 3
Magoli mawili ya Branislav Ivanovic yaliwapa The Blues uongozi katika mechi ya kwanza kuelekea Stamford Bridge. Lakini Liverpool wanajua namna ya kupambana katika usiku wa ulaya.
Fabio Aurelio alimfunga Cech kwa free kick nzuri dakika ya 19 – kabla ya penati ya Xabi Alonso kufanya matokeo kuwa 2-0.
Guus Hiddink akalazimika mabadiliko ya kiufundi kabla ya mapumziko, mabadiliko yakazaa matunda baada ya kupatikana kwa magoli kutoka Didier Drogba, Alex, na Lampard ambayo yalionyesha game imeisha.
Lakini Liverpool wakapata magoli mawili ambayo yaliwarudisha mchezo na hivyo na kwa bahati Lampard akazima ndoto zao kabisa kwa goli la mwisho kwenye mchezo huo.
Nusu Fainali 2008-09
Manchester United 1 Arsenal 0
Arsenal 1 Manchester United 3
Mechi ya kwanza Old Trafford haikutosha kuihakikishia United nafasi ya kufuzu na ushindi wa 1-0.
Ushajaa wa Manuel Almunia uliwasaidia kutoka OT na kipigo kidogo na waingereza walianza kampeni abadili uraia awe muingereza ili aweze kuchezea England.
Kampeni hizo ziliisha baada ya kiwango alichoonyesha Almunia @Emirates – wakati United walipoonyesha moja ya kiwango chao bora kabisa katika michuano ya ulaya.
Kuteleza kwa Keiran Gibbs kumruhusu Park Ji-Sung kuiongezea United idadi ya magoli ya uongozi dakika 8 ndani ya mchezo.
Sekunde 180 baadae Almunia akapiga hesabu mbovu juu ya mpira wa adhabu wa Ronaldo na kuruhusu lingine kwa United. Wayne Rooney akafunga la 3 muda mfupi kabla Darren Fletcher hajapewa kadi nyekundu ya utata na matokeo yake Van Persie akafunga goli la
kufutia machozi kwa Arsenal kwa mkwaju wa penati.
MECHI NYINGINE ZA WAINGEREZA VS WAINGEREZA KWENYE MICHUANO YA ULAYA
Cup Winner’s Cup first round 1963-64
Tottenham 2 Manchester United 0
Manchester United 4 Tottenham 1
Fairs Cup third round 1964-65
Manchester United 1 Everton 1
Everton 1 Manchester United 2
Fairs Cup third 1969-70
Newcastle 0 Southampton 0
Southampton 1 Newcastle 1
Cup Winners’ Cup semi-final 1970-71
Chelsea 1 Manchester City 0
Manchester City 0 Chelsea 1
Fairs Cup semi-final 1970-71
Liverpool 0 Leeds 1
Leeds 0 Liverpool 0
Uefa Cup final 1971-72
Wolves 1 Tottenham 2
Tottenham 1 Wolves 1
Uefa Cup semi-final 1972-73
Liverpool 1 Tottenham 0
Tottenham 2 Liverpool 1
European Cup last-32 1978-79
Nottingham Forest 2 Liverpool 0
Liverpool 0 Nottingham Forest 0
Champs Lge group stage: 2005-06
Liverpool 0 Chelsea 0
Chelsea 0 Liverpool 0
Champs Lge semi-final: 2006-07
Chelsea 1 Liverpool 0
Liverpool 1 Chelsea 0 aet: 4-1 pens
Champs Lge quarter-final 2007-08
Arsenal 1 Liverpool 1
Liverpool 4 Arsenal 2
Champs Lge quarter-final 2010-11
Chelsea 0 Manchester United 1
Manchester United 2 Chelsea 1