Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

CHELSEA VS PSG: TAKWIMU NA VIDEO YA MAGOLI

$
0
0

Chelsea vs PSG

PSG imezima ndoto za Chelsea kusonga mbele kwenye michuano ya mabingwa Ulaya kwa mara nyingine tena baada ya Zlatan Ibrahimovich kuifungia bao la ushindi timu yake kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

PSG walianza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Adrien Rabiot aliyeunganisha vyema krosi ya Ibrahimovic dakika ya 16 kipindi cha kwanza.

Diego Costa aliisawazishia Chelea kabla ya kwenda mapumziko lakini Ibrahimovic alifunga goli lililoipa uhakika PSG kutinga hatua ya robo fainali ya Champions League.

PSG ndiyo waliitoa Chelsea kwenye michuano ya Ulaya msimu uliopita kwenye hatua kama hiyo.

Chelsea sasa ipo nafasi ya 10 kwenye Premier League ikiwa haina matumaini ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao huku Costa na Eden Hazard wakiwa majeruhi watakuwa na kibarua cha kucheza robo fainali ya FA Cup dhidi ya Everton Jumamosi ijayo.

Takwimu muhimu

  • PSG ni timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya Champions League kutoka Ufaransa katika kipindi cha miaka minne mfululizo.
  • PSG ni timu ya nne kutoka katika ligi tano kubwa Ulaya kufunga magoli 100 katika mashindano yote msimu huu, timu nyingine ni Barcelona (132), Real Madrid (107) pamoja na Borussia Dortmund (103).
  • Diego Costa amefunga au ku-assist magoli 17 kwenye mechi 15 zilizopita za michuano yote Chelsea iliyoshiriki. (amefunga magoli 11 na ku-assist magoli 6).
  • Costa amefunga goli kwenye kila mechi katika mechi tano zilizopita kwenye uwanja wa Stanford Brigde.
  • Zlatan Ibrahimovic amehusika moja kwa moja kwenye magoli 29 ya PSG kwenye michuano ya Champions League tangu mwaka 2012 (amefunga magoli 19 na kusaidia magoli 10), 17 zaidi ya mchezaji yeyote.

Video ya magoli yote ya Chelsea vs PSG


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>