Bacary Sagna alikua anatambulika kirahisi kwa rasta zake ambazo zilikua na rangi. Sasa akiwa kwenye mapumziko ya likizo baada ya msimu uliopita alinyoa rasta zake na picha yake kusambaa sana kwenye socia media.
Sasa akiwa kwenye session ya maswali na majibu kati ya Manchester City Tv, moja ya swali lililoulizwa na mashabiki wengi ni kuhusu kwanini amenyoa rasta zake.
Jibu lake ni kwamba yeye binafsi alikua na mpango wa kuzinyoa muda wowote, lakini sababu ya msingi iliyomfanya anyoe zile rasta ni sherehe ya asili aliyoshiriki kwao Senegal ambayo ilikua lazima anyoe nywere zake.