Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

LIGI YA UBELGIJI DARASA TOSHA KWA WACHEZAJI WA KIBONGO

$
0
0
Mwana Samatta akiwa mazoezini kwenye klabu yake ya Genk, Ubelgiji
Mbwana Samatta akiwa mazoezini kwenye klabu yake ya Genk, Ubelgiji

Na Jackson Wambura

Ligi kuu ya Belgium imeanza kujizolea mashabiki baada ya Watanzania wengi kufatilia kile anachokifanya Mbwana Sammata katika club ya Genk pia wachezaji wengi wa club hii pia na timu kwa ujumla imekua ikipata followers wengi kutoka Tanzania katika mitandao ya kijamii hii yote ni kuonesha kuwa Watanzania wanapenda kufatilia kila hatua anayopiga Mtanzania mwenzao Mbwana Samatta.

Swali la kujiuliza wachezaji wetu wanajifunza nini kutoka kwa Mbwana samatta? ni motisha gani wanapata kutoka kwa Samatta? Tanzania bado tunaweza kutoa kina Samatta wengine kutokana na aina ya wachezaji tulionao kama wataongeza juhudi na kutolemewa na ustaa wa Bongo na kelele za mashabiki jukwaani.

Unamkumbuka Msuva wa msimu uliopita? kijana alikua tishio sana huku akiwa mfungaji bora wa ligi kuu ikafikia hatua ya kwenda kufanya majaribio nchini Africa kusini lakini naona kama Msuva alikosa washauri wa kumweka sawa kisaikolojia baada ya kulewa mafanikio na kuzoea kelele za mashabiki jukwaani waliofikia hadi kujichangisha fedha na kumpatia Msuva.

Leo hii Msuva kaanza kupotea kwenye kiwango chake siyo Msuva wa msimu uliopita kama angetulia na kucheza kwa vision kuliko kucheza kwa hobby leo hii tungekua tunamwona katika kiwango kikubwa na hata kufikia hatua ya kucheza nje ni mara chache sana kwa mfungaji bora na mchezaji bora wa msimu kutemwa kwenye timu ya taifa.

Siwezi mlaumu Msuva bali nawaangalia washauri wake. Kwa sasa kuna vijana wanafanya vizuri msimu huu kama Ibrahim Ajib wa Simba, Maguli Elias wa Stand, Kichuya wa Mtibwa Farid Mussa wa Azam na wengineo kama kina Chanongo vijana hawa kama wakicheza mpira kwa malengo kuliko kelele na ushabiki wa majukwaani tunauhakika tukaona wakina Samatta wengine.

Pia naweza vilaumu vilabu vyetu kuwa moja ya sababu ya kuwakatisha tamaa vijana hawa kujaribu bahati yao nje nani anajua kinachoendelea kati ya Ubwa na Chanongo kuhusu kwenda TP Mazembe taarifa zilikuja wamefanya vizuri lakini mpaka sasa hatuoni nini kinaendelea.

Pale Simba kuna mchezaji anafanya vizuri kwa sasa Ajibu Ibrahim Migomba kama atatulia na kuwa na washauri wazuri wanaomzunguka namwona akifata nyayo za Samatta anapaswa kucheza kwa malengo kuliko kuona msimbazi kama mwisho wa safari yake kwa kulewa sifa za mashabiki wa Msimbazi.

Ana kila sifa na sababu za kucheza nje kama ataendelea kuonesha juhudi anazoonesha sasa. Wachezaji wengi wakibongo wamekuwa wakiona kama Simba, Yanga au Azam kama ndiyo mwisho wa safari zao.

Binafsi bado naamini Msuva ananafasi kubwa ya kurudi kwenye fomu kama ataacha kucheza na jukwaa pia kutambua umri unakwenda na umri walio nao ndiyo sahihi kwenda kucheza nje.

Tusiridhike kwa kuangalia ligi moja tu ya Belgium wakati tupo zaidi ya watanzania million 40 tunamwangalia mchezaji mmoja tu nje. Wachezaji wetu wana somo kubwa la kujifunza kutoka kwa Mbwana Samatta.

Je vilabu vyetu vinatoa sapoti gani katika kuwa-promote wachezaji hawa nje? wengi wamekua wakienda nje na kurudi Bongo kuchezea timu hizi za Simba, Yanga, Azam kwa kukosa uvumilivu leo hii Haruna Moshi angekuwa na uvumilivu.

Tungekua tunamwangalia kwa upande wa pili kama Samatta vile vile Shomari Kapombe leo hii angekua mbali kulingana na kipaji chake japo yeye bado ananafasi kubwa ya kucheza nje kama atatulia na kuendelea kucheza katika malengo.

Ukimwangalia Farid Mussa, Singano na Chanongo bado wana umri mdogo ambao ndiyo sahihi kwao kucheza nje, wanapaswa kujituma zaidi na kuona bado wana safari ndefu ya kisoka.

Kikubwa ni wao kujituma kuwa na nidhamu na malengo leo hii tungekua tunamwangalia Samatta VPL kama angechukulia Simba kama mwisho wa safari yake pia kama asingekua na uvumilivu pale Congo na kurudi Bongo.

Leo hii tunamwangalia na kufatilia kila hatua anayopiga kutokana na matunda ya uvumilivu, nidhamu na malengo mfano leo hii ukimuuliza Samatta malengo yake atakwambia bado hayajatimia mpaka acheze timu kubwa moja wapo za Ulaya.

Wachezaji wetu wanamengi ya kujifunza pia kutumia safari ya Samatta kama motivation kwao kuliko kuona wamefika kwa kelele za jukwaani.

wamburajacksonw@gmail.com

0753962578


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>