Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) tayari wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa.
Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars kesho Ijumaa asubuhi, timu itafanya mazoezi mepesi kwnye uwanja wa Taifa.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa na Said Mohamed, walinzi ni Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.