
Juma Kaseja (wa kwanza kushoto) wakati akikabidhiwa jezi ya Mbeya City mara baara ya kusaini mkataba mfupi wa kuitumikia klabu hiyo mwaishoni mwa dirisha la usajili
Leo utapigwa mchezo kati ya Mbeya City dhdi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo timu zote mbili ni za mkoa mmoja na kuufanya mchezo huo kuitwa ‘Mbeya Darby’ kwani kumekuwa na upinzani mkubwa timu hizo zinapokutana kwenye mechi za ligi.
Juma Kaseja ni mlinda mlango mpya katika kikosi cha Mbeya City, uzoefu wake wa kucheza mechi kubwa za Simba na Yanga ndio umeufanya mtandao huu kupiga story na kipa huyo mkongwe ili kujua mambo kadhaa kuelekea pambano hilo ambalo kama akipewa nafasi atakuwa anacheza kwa mara ya kwanza Mbeya Derby.
Shaffihdauda.com: Kama ukipewa nafasi kwenye mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons itakuwa ni mechi yako ya kwanza kwenye Mbeya Derby unautazamaje mchezo huu unaonekana kuwa mgumu kutokana na historia ya timu hizi?
Kaseja: Malengo yetu kwa sasa ni kushinda kila mechi, mimi najua umuhimu wa Derby jinsi ulivyo lakini naamini kwa ushirikiano na mandalizi ya timu, tutapambana kupata alama tatu.
Shaffihdauda.com: Unazungumziaje maisha ya Mbeya City na timu nyingine ambazo umeshawahi kuzitumikia kama Simba na Yanga
Kikubwa sitaki kuzungumzia sehemu ambapo sipo kwa sasa, ninazungumzia sehemu ambayo nipo. Kwa sasa mimi ni mchezaji wa Mbeya City naishi kwenye jiji la Mbeya na maisha ya Mbeya City nashukuru Mungu yanakwenda vizuri, tunaishi vizuri kama ndugu hiyo ndio naweza kuzungumza lakini siwezi kuzungumzia timu nyingine.
Kwa maisha kama haya nilishaishi kwasababu mimi sikuzaliwa Dar es Salaam, nilizaliwa Kigoma nilikuja Dar es Salaam nikiwa naakili zangu timamu. Mimi naona maisha yangu niliyokuwa naishi Kigoma na Mbeya ni yaleyale hayana tofauti, kwahiyo mimi naona ni kawaida kwangu.
Shaffihdauda.com: Mbeya City ni timu ambayo tunaona sasahivi inavijana wengi, na wewe umekuwa ukisifiwa kuwa kiongozi bora unaiona wapi timu yako mwishoni mwa msimu huu?
Kaseja: Mimi nadhani hata hao mastaa walianza kama chipukizi mpaka wakafikia huko walipo, kwa hiyo mimi naamini uwepo wa wacheaji wengi kwenye kikosi cha Mbeya City italeta changamoto kwasababu kilamtu anatamani kufikia malengo yake katika safari yake ya kucheza mpira.
Kikosi kimechanganyika, tupo sisi ambao mnatuita wakongwe vilevile wapo chipukizi kwahiyo sisi tutawasapoti chipukizi waweze kufikia malengo yao.
Shaffihdauda.com: Unazungumziaje morali ya mashabiki wa Mbeya City
Kaseja: Kwa bahati nzuri toka Mbeya City ipande daraja, sijawahi kucheza game against Mbeya City, kwahiyo nimekuja Mbeya City naona mashabiki wanamwamko mbubwa na wanaisapoti timu.
Shaffihdauda.com: Ulishawahi kufikiria kuna siku utakuja kucheza Mbeya City?
Kaseja: Mimi ni mchezaji na maisha ya mpira ni safari ndefu, kwahiyo huwezi kujipangia wewe utakuwa unacheza timun gani. Mimi ni mchezaji na sio Mbeya City tu naweza kucheza timu yoyote kwasababu kabla ya kucheza hizo timu kubwa nilianza kucheza Moro United, nikacheza Mtibwa kwahiyo mimi nitacheza timu yoyote.