Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

AS Roma VS Inter Milan…battle ya kucheza UEFA live on Startimes.

$
0
0

cov

Boss wa Inter Milan Roberto Mancini anaamini kwamba mechi yao dhidi ya Roma kwenye uwanja wa Stadio Olimpico inawrza kuleta matumaini mazuri kwa club yao kucheza UEFA msimu ujao.

Inter inaweza kufikika hadi namba tatu kama wakishinda mechi ya kesho dhidi ya Roma ambayo ipo namba 3. Lakini Mancini amesisitiza kwamba mechi hiyo siyo kwamba itaamua wao kucheza UEFA lakini itaamsha matumaini.

Mancini amesema, “Najua wachezaji wanajua hii ni mechi kubwa, sidhani kama hii ni mechi ya kufanya maamuzi ya mwisho kwasababu kuna mechi nyingi bado zipo hazijachezwa. Lakini itakua ni muhimu kushinda hii mechi ili kupunguza pengo la points zilizopo”.

Akiizungumzia Roma amesema, “Wana wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa na wamecheza pamoja kwa muda mrefu sana kitu ambacho kina wamaisha. Chochote kinaweza kutokea ndani ya dakika 90 kwasababu najua watajitoa kwa asilimia 100”

Mechi hii na nyingine zote za Serie A zinaonekana live kwenye king’amuzi cha Startimes. Mechi hii itaonekana kupitia channel ya World Football kesho saa 4:45 usiku. Unatakiwa kuwa na kifurishi cha Sports Plus na Sports Play ili uweze kuangalia.

Hii pia ni ratiba ya mechi nyingine za Serie A kwenye Startimes.

star


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>