Wakati leo ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea kwa michezo mitatu, mchezo unaopewa uzito wa juu ni kati ya Coastal Union wanaoburuza mkia kwenye ligi dhidi ya Simba vinara wa ligi hiyo.
Mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga unamrejesha nyumbani Jackson Mayanja aliyekuwa kocha wa zamani wa Coastal ambaye ni kocha wa sasa wa Simba.
Kuelelekea mchezo huo, Mayanja ametangaza kikosi cha wachezaji wafuatao ambao watachuana na ‘wagosi wa kaya’;
Kikosi kitakachoanza leo ni
1. Vicent Angban
2. Juuko Murshid
3. Novalty Lufunga
4. Emery Nimubona
5. Mohamed Hussein ‘Tshabalala’
6. Justice Majabvi
7. Jonas Mkude
8. Mwinyi Kazimoto
9. Said Ndemla
10. Hamis Kiiza
11. Danny Lyanga
Kikosi cha akiba ni
1. Peter Manyika
2. Abdi Banda
3. Awadh Juma
4. Brian Majwega
5. Raphael Kiongera
6. Ibrahim Ajib
7. Mussa Mgosi