
Kocha mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm amemzungumzia gwiji wa soka wa Uholanzi na Barcelona Johah Cruyff kuwa ni mtu wa pekee kuwahi kutokea na Uholanzi imepoteza nembo ya soka lake.
Van Pluijm aliwahi kucheza na Cruyff kwenye ligi ya Uholanzi wakati huo Pluijm akiwa kama golikipa wa timu ya FC Den Bosch amezungumza mambo mengi sana kuhusu Cruyff ambaye amefariki March 24 mwaka huu.
Kiukweli atabaki kuwa alama ya soka la Uholanzi, mchezaji bora kabisa tuliyepata kumshuhudia katika mpira wetu wa Uholanza na ghafla mtu anafariki, vitu vingi vinakuja kichwani unakumbuka mambo mengi sana. Nimekutana naye akiwa kama mchezaji na pia nikakutana naye akiwa kama mwalimu nikapata wasaa mzuri sana wakujadiliana naye mambo mengi yanayo husu soka.
Kiukweli yupo tofauti sana na walimu wengine kwa namna ambavyo anauzungumza na kuufafanua mpira na ni wakipekee, angalia alifanikiwa kumuiga mwalimu Rinus Michels ambaye alikuwa kocha wa Ajax na nafikiri hata akiwa na umri mdogo sana hakuwa tu na kipaji kikubwa, bali alikuwa tayari kiongozi imara. Aliweza kuwa kocha ndani ya uwanja na alimsadia kwa kiasi kikubwa Michels.
Nimeweza kwenda kumtazama na timu yake uwanjani pia akiwa anacheza na walikuwa na kikosi bora na uwezo mkubwa sana. Nakumbuka goli bora alilofunga dhidi ya timu ambayo sasahivi inafahamika kama ADO Den Haag lakini kabla ilikuwa inaitwa FC Den Haag. Alikuwa akisimama anatazama viatu vyake mara ukaja mpira mrefu kutoka kwa beki, kipa wa Den Haag alikuwa kasimama mbele kidogo ya lango mpira ukaja kwake na haraka akapiga shuti akiwa kama mita 40 au 50 hivi na akafunga goli.
Lakini pia goli alilowafunga Brazil akiupeleka mpira post ya mbali kabisa. Kuna wakati nilikuwa na timu yangu, wakati huo alikuwa na timu ya Barcelona wachezaji wangu wakapata nafasi ya kumuona na alikuwa anafundisha soka la kumiliki mpira kitu ambacho kimekuja kuwa nembo ya Barcelona na namuona Pep Guardiola kama mtu aliyemrithi Cruyff na kuchua mengi kutoka kwa Cruyff.
Tazama Michels, alikuwa mtu sana na huyu Cruyff alikuwa mtu mgumu sana ambaye ungeweza kucheza dhidi yake sasa kama ni kocha au mchezaji na ukapata kuwaona watu hawa lazima upate mambo mengi sana ya kuchukua kutoka kwao.
Nilikuwa kipa kipindi hicho tunakutana nao nilikuwa navaa namba 18 ninapicha kadhaa nikiwa naye pia, ni kitu kizuri pia na ukicheza dhidi ya mchezaji wa kariba yake na baadaye nikakutana naye kwenye camp ya timu ya taifa kiukweli ni mtu wa kipekee lakini unaweza ukatazama hisia za watu tofautitofauti alikuwa ni mtu na mchezaji tofauti sana.
Unaweza kumuweka mahala pamoja na Pele na wachezaji bora wengine wa muda wote. Kile kizazi chao kilikuwa bora kupindukia na ndiyo maana Michels alipata umaarufu mkubwa hadi kuitwa General.