Huyu jamaa ni maarufu sana kwa kuwadhihaki wachezaji wa Real Madrid pale ambapo watakapo fanya vibaya kwenye kitu chochote hasa cha kuhusu soka.
Gazeti la Marca limetoa taarifa kwamba Pique ni moja kati ya watu ambao wanai motivate wachezaji wa Real Madrid kutaka kuifunga Barcelona. Pique amekua bingwa wa kuchokoza Real Madrid kwenye internet mara baada ya kupoteza mechi.
Pique aliwahi kuwachokoza Real Madrid walipotolewa kwenye michuano ya Copa del Rel. Pia aliwahi kuzomewa na mashabiki wa Real Madrid alivyokua kwenye majukumu ya timu ya taifa.
Wachezaji ambao ana beef nao sana ni pamoja na Ronaldo, Sergio Ramos na Arbeloa na hawa inasemakana wamepanga sana kuhakikisha wanaifunga Barcelona.
Lakini swali juu ya hii ripoti ni kwamba Gerard Pique ndio itakua chachu pekee ya Real Madrid kushinda? Mechi itakua Live kwenye Azam TV saa 3:30 leo usiku.