Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

UGANDA KUTUMIA KIFO CHA DHAIRA KUFUZU AFCON 2017

$
0
0

Dhaira

Wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Uganda wanataka kumuenzi golikipa wao Dhaira kwa kuhakikisha wanafuzu kwenye fainali za Africa Cup of Nations mwaka 2017 ambazo zitafanyika Gabon.

Shughuli za mazishi zimefanyika Jumatatu kwenye jiji la Kampala, Dhaira, 28, alifariki juma lililopita akiwa nchini Iceland kutokana na ugonjwa wa cancer

Tutapambana sana kuhakikisha tunafuzu kwenye fainali zitakazofanyika Gabon kwa ajili ya heshima ya Dhaira”, Moses Magogo ambaye ni rais wa FA ya Uganda aliiambia BBC.

Uganda kwa sasa ipo kundi D ikiwa na pointi 7 sawa na Burkina Faso huku timu hizo zikiwa zimelingana kwa kila kitu kwenye kundi hilo lakini Burkina Faso inakaa kileleni mwa kundi kulingana na mpangilio wa ‘alphabet’.

Group G-Uganda

Tonny Mawejje ambaye ni mchezaji mwenzake na Dhaira kwenye timu ya taifa pia akiwa amewahi kucheza Iceland ameunga mkono kauli iliyotolewa na Magogo.

“Ni vigumu kuzungumzia mchezo wa mpira wa miguu halafu usilitaje jina la Dhaira, alikuwa anamchango mkubwa kwenye nchi hii”, Magogo aliendelea kusema.

Kocha wa sasa wa Uganda Milutin Sredojevic ‘Micho’ pia amemzungumzia golikipa huyo ambaye aliwahi kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akiwa na klabu ya Simba SC.

“Abel was a close friend to many of the Uganda Cranes players we are devasteted by his unexpected passing,” he explained.

“Abel alikuwa ni rafiki wa wachezaji wengi wa Uganda Cranes kifo chake kisichotarajiwa kimetuachia machungu ,” amesema.

Tunapoelekea michezo yetu miwili ya mwisho ya kufuzu Mataifa ya Afrika, tutakuwa na sababu kubwa ya kufuzu kwenye fainali hizo baada ya miaka 39 kwa ajili ya Abel Dhaira”.

“Uganda imepoteza golikipa muhimu na siku zote tutaendelea kumkumbuka”

Dhaira atazikwa  leo (Jumanne) kwenye wilaya ya Mayuge, Mashariki mwa Uganda.

Alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya taifa mwaka 2009 na kuisaidia The Cranes kutwaa ubingwa wa CECAFA Senior Challenge Cup mwaka 2012 mashindano yaliyofanyika kwenye ardhi ya Uganda.

Licha ya kucheza nchini Iceland, enzi za uhai wake aliwahi kuvitumika vilau kadhaa kama Express na URA za Uganda, kisha akaelekea AS Vita ya DR Congo na baadaye Simba SC ya Tanzania.

Inaelezwa kuwa, mchezaji mwingine wa zamani wa Uganda Mathias Kaweesa anapambana na ugonjwa wa cancer.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>