Na Dastan Nehemia
Ilikuwa ni kawaida enzi za Sir Alex Ferguson akiwa anaifundisha Manchester United kushuhudia akishinda mataji kwa kutumia wachezaji wenye thamani ndogo sokoni hata wengine kuwa na viwango vidogo kulinganisha na timu nyingine pale katika ligi ya England lakini aliweza kuongoza na kushinda Premier league.
Sir Ferguson alikua sio muumini sana wa kupenda wachezaji wenye majina na wenye gharama kubwa, alifanya hivyo mara chache sana, tena nyakati za mwisho akikaribia kustaafu ndipo alijaribu kusajili wachezaji wenye majina makubwa, lakini mara nyingi alipenda kuchukua vijana wadogo na kuwatengeza mwenyewe.
Kijana kama Cristiano Ronaldo ambaye alikua asajiliwe na Arsene Wenger lakini baada ya Wenger kujishauri-shauri, Ferguson akamchukua kwa matumaini ya baadae, nadhani sisi sote ni mashidi wa kipi kilichotokea baadaye, Ronaldo kuibuka kuwa mchezaji bora duniani.
Kuna kipindi Sir Alex Furguson alikasirika sana, na hii ilikua baaada ya kumtaka kinda kutoka nchini Brazil Lucas Moura, na akajikuta amepigwa kikumbo na matajiri wa Ufaransa PSG ambao walitumia zaidi ya Euro million 30 kumsajili kinda huyu.
Ferguson alikasirishwa sana na hili jambo na kusema ni ajabu sana kuona timu inatoa pesa nyingi kumsajili mchezaji mwenye umri mdogo halafu bado hana uzoefu wowote wa kucheza Ulaya, Ferguson aliamini kuwatengeneza wachezaji kwa kuwapa hamasa na kuwafunza nidhamu ya nje na ndani ya uwanja inatosha kuwa na matokeo mazuri.
Baada ya Ferguson kuondoka na Moyo wake ukaondoka pale Old Trafford kwani timu ikabadilika kiuchezaji na kilichowashangaza wengi, wachezaji walikua walewale aliowaacha Ferguson na kuongezeka wachezaji wapya wenye majina lakini bado timu imeshindwa kufanya vizuri.
Jibu liko wazi ule moyo wa Ferguson haupo tena, wacheazaji hawajiamini na wamepoteza ari uwanjawani.
Leicester City msimu huu imeishangaza dunia kwa kuvizidi vilabu vikubwa vya Chelsea, Arsenal, Liverpool, Manchester City, Totenham na Manchester United kwa kushikilia usukani wa ligi mpaka kufikia wakati huu, ukweli unaoumiza ni kwamba Leicester City hawana wachezaji wenye thamani na viwango kama vya wachezaji wa vilabu hivyo vikubwa vya Uingereza, wanawachezaji wa kawaida sana tena wengi wao wamewatoa ligi ya Championship na vilabu vidogovidogo.
Kinachofanya Leicester City wafanye vizuri mpaka sahivi ni nidhamu ya wachezaji, kutambua majukumu yao uwanjani na morali ya ushindi huku wakiwa wameaminishwa na kocha wao Claudio Ranieri kuwa wachezaji wote ni sawa ila kinachowatofautisha ni juhudi za mazoezi na katika mechi.
Mchezaji kama Jamie Vady kutikisa nyavu zaidi ya Aguero, Diego Costa na Wyne Rooney lazima likushangaze kwani Vardy hafikii hata nusu ya mishahara wanayolipwa hao wachezaji, au viungo wao kama Kante na Mahrez kuiongoza timu yao kufanya vizuri zaidi ya Yaya Toure, Cesc Fabregas, mabeki Huth na Morgan kutengeneza safu nzuri ya ulinzi zaidi ya vilabu vikubwa vyenye walinzi walionunuliwa kwa gharama na kulipwa mishahara mikubwa lazima ujiulize na ushangazwe kwa hili.
Hakuna haja ya kushangaa kwani ukweli ni juhudi, morali, hamasa na nidhamu ndivyo vinavyoisaidia Leicester City kupata matokeo mazuri uwanjani, Kwani misingi hii ya Leicester City ndio Sir Alex Ferguson aliyokuwa akiifanya pale Old Trafford akiwa na Manchester United, Na ndiyo maana nasema, Leicester City wanatembea na moyo wa Sir Alex Ferguson.
0655995405