Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

#Uefalona: Je Barca Hupendelewa Na Waamuzi? Huu Hapa Uchambuzi Wa Kina Juu Ya Malalamiko Ya Kupendelewa Kwao

$
0
0

Beki wa Atletico Madrid Filipe Luis ameituhumu UEFA kuilinda Barcelona baada ya mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya ambao walifungwa katika dimba la Nou Camp na pia akafikia hatua ya ‘Wachezaji wa Barcelona wafanye nini ili waweze kupewa kadi na refa.’

 
  
 Luis na wachezaji wenzake wa Atletico walikasirishwa na Luis suarez kuruhusiwa kuendelea kuwepo uwanjani baada ya kumpiga teke Juafran akiwa hana mpira kipindi cha kwanza wakati Atletico waliona nafasi yao ya kuendelea mbele kwenye nusu fainali ikiwa finyu baada ya Fernando Torres kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35. 

“Kutolewa nje ya uwanja kwa Torres haikuwa haki kabisa na kulibadilisha mchezo. Barcelona wanalindsa. Unapocheza nao unagundua ni klabu yenye nguvu sana,” alisema Luis. 

“Unagundua hilo pale kunapokuwepo na mazingira ya Barcelona kuweza kutolewa. Unapatwa na hisia labda itawaumiza UEFA sana Barca akitolewa. Sijui labda mchezaji wa Barcelona afanye kitu gani ili refa aweze kumtoa nje ya uwanja.” 
Baada ya kusoma alichosema Luis, tuangalie labda ni kitu wanachofanya au wasichofanya ambacho kinawafanya wachezaji wa Barcelona kutoadhibiwa na Je wapo juu ya sheria. 
Kadi nyekundu upande wao. 

Wachezaji wawili tu wa Barcelona ndio wametolewa nje kwa kadi nyekundu msimu huu na wote walitolewa kwa makosa ya lugha chafu. Gerard Pique alitolewa nje kwa kumsemea mbovu refa msaidizi katika mchezo wa  pili wa Spanish Super Cup vs  Athletic Bilbao August 2015 – Pique alipewa adhabu ya kufungiwa mechi 4 na Barca wakafungwa kwa jumla 5-1.

Pique huyu huyu ndio aliepuka kupewa kadi ya pili ya njano kwa kitendo cha makusudi katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya UCL vs Arsenal. Pique alionekana akiwa na mazungumzo yaliyotia mashaka na Luis Enrique na dakika moja baadae akamfanyia rafu ya makusudi Danny Welbeck ili apewe kadi ya pili ya njano na akafanikiwa. 

 

Uefa lakini wakaamua kutochukua hatua za ziada za kumuadhibu mlinzi huyo wa kihispania. 

Javier Mascherano ndio mchezaji mwingine pekee wa Barca alionyeshwa nyekundu kwa kauli chafu kwa refa mnamo October 2015 katika mechi ya La Liga vs Eibar.

Inasemekana Muargentina huyo aliktukana matusi ya nguoni refa msaidizi katika mechi ya ushindi wao wa 3-1 nyumbani. Boss wa La Liga Javier Tebas alimtetea Mascherano kwa kusema matusi hayo hayakuwa mazito sana. .

Barcelona kwa upande mwingine wamenufaika na kuwasababishia wachezaji 12 kutolewa nje katika mechi 9 msimu huu – kadi 4 zilihusisha madhambi makubwa – na pia Barca walibahatika kuona wapinzani wao wakimaliza mechi na wachezaji 9 uwanjani katika mechi 3 tofauti – dhidi ya Atletico, Espanyol na Rayo Vallecano.

Kwa ujumla kadi nyekundu 90 zimetolewa katika La Liga msimu huu huku Rayo Vallecano wakiongoza kwa kupata kadi nyingi – kadi 10 wakati Barca wakishika nafasi ya mwisho kwa kupata kadi 1. 
 
Barcelona pia wapo katika nafasi ya mwisho kwa timu ambazo zinaongoza kwa wachezaji wake kuonywa na kadi za njano. Barca wamepata kadi za njano 53 baada ya michezo 31 ya La Liga msimu huu – nusu ya idadi ya kadi walizopata Granada. 

Kadi za Njano 
  

Kadi ambazo hawakuadhibiwa

Barcelona sio kwamba wao wana usafi dimbani kuliko wachezaji wa timu nyingine, la hasha. Wakati wanamsajili Suarez walijua pamoja na kipaji alichonacho lakini pia alikuwa na nidhamu mbovu. Inawezekana amepunguza mapepe yake lakini mshambuliaji amekuwa akionewa haya na waamuzi wengi msimu kama ilivyokuwa mchezo wa juzi vs Atletico. 

 Suarez amepokea kadi za njano 8 msimu huu na alipaswa kuonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Atletico. Barcelona walikuwa na mchezaji mmoja wa ziada mpaka kufikia wakati anampiga teke Juafran na kama refa angeona basi mchezo ungeisha timu zina idadi sawa ya wachezaji uwanjani. LakininSuarez aliepuka adhabu na akaenda kufunga magoli mawili yaliyoipa ushindi timu yake. Akizungumzia tukio hilo mtangazaji wa BT Sport, Rip Ferdinand alieleza kwamba Suarez bado anaweza kuadhibiwa na UEFA kwa kuangalia mkanda wa mchezo.   

Lionel Messi vs Real Madrid 

Lionel Messi huwa hakabiki wakati anapokuwa kwenye ubora wake, lakini dhidi ya Real Madrid wikiendi iliyopita alisahau kucheza mchezo wake na kuamua kucheza kihuni kwa kumfanyia madhambi Pepe. Hata hivyo mwamuzi hakumpa adhabu yoyote. 
Jordi Alba v Arsenal

Udanganyifu kwa marefa na wachezaji wa Barca ni jambo moja lakini lini marefa wataona udanganyifu ni kosa linalostahili adhabu kwa wachezaji wa Barca? 

Jordi Alba alifanya kila mbinu kuhakikisha inaonekana kwamba Oliver Giroud alimpiga kiwiko wakati wa mchezo wa 16 bora vs Arsenal – lakini tukio hilo ukiliangakia kwa makini unaona Alba alimuongopea mwamuzi ili  Giroud atolewe nje. 

Baada ya kujiangusha Alba alichukua muda kidogo sana na kuinuka baada ya kuona refa aligundua ujanja wake – refa aliona lakini hakuchukua hatua zozote za kumuadhibu mchezaji huyo. 


Utetezi wa Barcelona
Barcelona wanaonekana na wengi kuwa sio timu bora tu duniani lakini pia ni timu yenye wachezaji wengi mno bora kuliko wengi. Wachezaji wake wana mbinu nyingi na uwezo mkubwa wa kuchezea mpira na hivyo kwa kawaida huwa ni timu inayoongoza kwa kuchezewa rafu. Hata kwenye michuano ya ulaya Barcelona ndio timu inayoongoza kusababishia wachezaji wa timu pinzani kupata kadi nyekundu nyingi kma inavyoonekana kwenye picha 👇  

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>