Divock Origi ameipa Liverpool goli muhimu la ugenini kwenye mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Borussia Dortmund mchezo ambao umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Origi ameitungua timu ya zamani ya kocha wake Jurgen Klopp kwenye mchezo ambao ulimrejesha Klopp kwa mara ya kwanza kwenye dimba la Signal Iduna Park akiwa kocha wa timu pinzani na Dortmund.
Golikipa wa Dortmund Roman Weidenfeller alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Origi muda mfupi kabla ya mapumziko.
Mats Hummels aliisawazishia Borussia Dortmund lakini bado matokeo hayo ni faida kwa Liverpool.
Hadi mwisho wa mchezo matokeo ya timu hizo kufungana goli 1-1 yalikuwa si mabaya kwa kila upande licha ya Dortmund kupewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la Europa League msimu huu, Dortmund walitawala mchezo kwa asilimia nyingi lakini mbinu za Klopp ziliisaidia Liverpool kudhibiti mashambulizi ya wenyeji wao.
Jambo la kuvutia kwenye mchezo huo ni wimbo wa ‘You’ll Never Walk Alone’ ambao unatumiwa na vilabu vyote viwili kama wimbo wao wa uwanjani. Kabla ya pambano hilo kuanza wimbo huo uliimbwa na mashabiki wa timu zote mbili kwa pamoja na kuibua hisia kali kati yao.
Mchezo wa marudianno utapigwa April 14 kwenye uwanja wa Anfield.
Angalia viedo ya magoli Dortmund vs Liverpool